Mimi sina shida na mali ya wazee wangu lakini najua kuwa mali za wazee inabidi wapewe wenye uwezo wa kuziendeleza(siyo uwezo wa kielimu bali fedha). Kuna watu hawatakiwi kupewa ijapokuwa wana haki ninajitafutia maisha lakini hata nikifa mali zangu nitawarithisha watoto wangu kadri ya uwezo wao. Siwezi kumpa mtoto ambaye hajawahi hata kujenga choo ghorofa, mtoto hajui hata tabu ya kugombana na mafundi na gharama za ujenzi. Utakuja kuamka huko kuzimu ndani ya miezi michache vitu vinauzwa vyote. Kama mzazi hajaacha wosia nashauri busara itumike waachiwe wenye uwezo wa kifedha waziendeleze ukipata gawio lako wekeza. Usijifanye kimbele mbele ili uonekane utangukia pua vibayya sana.
Kibaki ana mke mmoja na watoto watano na sio mlimaji sana akawa yeye na watoto wake analima kama ekari 30,
Kaputi ambaye ana wake wawili na watoto 15 akawa analima sehemu kubwa ya shamba kama ekari 70
Hili ni wazo zuri ukizingatia hakuna wosia wowote wa maandishiWatoto wa Kaputi wanadai ekari 70 ni mali yao wajukuu 15 na iliobaki ekari 30 ni watoto wa Kibaki, yaani ibaki kama ilivyokua mazoe kulima
Watoto wa kibaki nyie ndo mtaleta balaa 😃, kubalini mpate hizo heka 6@ waachieni hao 15 wagawane heka 4@Watoto wa Kibaki nao wanadai shamba ligawanywe katika kwakuwa babu yao Bingili alikua na watoto wawili tu hivyo shamba ligawanywe kwa muktadha wa Kibaki nusu na Kaputi nusu
Mimi sina shida na mali ya wazee wangu lakini najua kuwa mali za wazee inabidi wapewe wenye uwezo wa kuziendeleza(siyo uwezo wa kielimu bali fedha). Kuna watu hawatakiwi kupewa ijapokuwa wana haki ninajitafutia maisha lakini hata nikifa mali zangu nitawarithisha watoto wangu kadri ya uwezo wao. Siwezi kumpa mtoto ambaye hajawahi hata kujenga choo ghorofa, mtoto hajui hata tabu ya kugombana na mafundi na gharama za ujenzi. Utakuja kuamka huko kuzimu ndani ya miezi michache vitu vinauzwa vyote. Kama mzazi hajaacha wosia nashauri busara itumike waachiwe wenye uwezo wa kifedha waziendeleze ukipata gawio lako wekeza. Usijifanye kimbele mbele ili uonekane utangukia pua vibayya sana.
mo wamekwambia kuna ukakasi kwenye mgawanyo wa mali zao?Nyie ndo mnasababisha watu wadhulumiwe shida ni kitafuta vyao AU MIRADHI ZA WAZAZI WAO?yaani uache Mali kisa unasema unataka utafute zako?una uchizi?mo dewji Anglesea hivyo leo angekuwa hivyo?
Ila nakuhakikishia ndugu Bingili mkikubali mali iuzwe Kisha igawanywe kwa wajukuu 20 sawa kwa sawa nyie mliokua watano lazima mpunjike pakubwa
Heka 100 x 2,000,000/=@ =200m
Sasa chukua hiyo 200m gawanya kwa wajukuu 20 kila mmoja apate 10m
Kumbuka mngekubali mgao wa shamba mngepata heka 6@ na hao 15 wangepata heka 4@
Sasa chukua 10m/ heka 6
Kisha chukua 10m/heka 4
Mliotakiwa kupata heka 6 mtakua mmedhulumika pakubwa sana [emoji2][emoji2]
Mkuu kwa ujumla wote tunakubaliana shamba lisiuzwe bali ligawanywe kwasababu kwa sehemu kubwa wakubwa zangu pande zote mbili wanapata riziki kwa kulima kupitia mashamba hayo
Ila mahakama inaweza kuamua itakavyoona kama tutafika huko
Mimi nilikua nataka tu kupata mwanga ndio maana nikaleta hapa jukwaani
So hoja yetu ya kugawa shamba kwa minajiri ya watoto wawili inaweza kukosa mashiko kisheria mkuu?
Sisi pia tuliona kwamba kama mahakama itaamua kugawa shamba sawa kwa wajukuu wote bado itakua kama mzani umelalia kwao maana wao wako wengi
Kama utaratibu utakua ni kugawa kwa wajukuu wote hatunabudi kukubaliana na utaratibu huo ambao utakua ndio huo tulio ukataa wa wao kuchukua 70 sis 30
Unajua sheria na kudhania ni tofauti sana
Ishi sio haki, haki najua unayo lakini uwezo huna. Bora mkubaliane mwenye uwezo azisimamie upewe gawio.Hapa tunaongelea MIRATHI mkuu
Kwamba mwenye mali kafariki na kisheria wanarithi watoto
Nakuuliza kama Baba alikua na makampuni na mdogo wako alifanikiwa kuanzisha kampuni zake zikafanikiwa lakini wewe ukawa mwalimu mpintimbi primary school
Utapoteza haki zako kwasababu mdogo wako anahela na makampuni wakati wewe unahangaika na mikopo ya kausha damu kila mwezi
Usichanganye HAKI na uwezo wa kuendesha
Hakuna sheria inayosema mtu asipewe haki yake kisa ni masikini
Ishi sio haki, haki najua unayo lakini uwezo huna. Bora mkubaliane mwenye uwezo azisimamie upewe gawio.
uzenimgawane mtauwana
Unasema mali zako ulizitafuta ? Kuna mengi yamejificha katika mali za mtu ? Kila la heri mimi nilikuwa nakupa ushauri kutokana na niliyoshuhudia katika maisha yangu. Maisha ni zawadi uliyopewa na Mungu, sio lazima uchukue ushauri wangu ishi unavyotaka wewe.Ukiwa na haki yako ya mali ya urithi HAKUNA anayeweza kukupangia uifanyeje
Hiyo unayoita “uwezo” ni dhana yako tu mkuu, uwezo ni nini kwenye mali yangu ya urithi? Kwani ni lazima niendeleze? Hata nikiamua kulewa na kuhonga zote si ni mali zangu?
Unasema mali zako ulizitafuta ? Kuna mengi yamejificha katika mali za mtu ? Kila la heri mimi nilikuwa nakupa ushauri kutokana na niliyoshuhudia katika maisha yangu. Maisha ni zawadi uliyopewa na Mungu, sio lazima uchukue ushauri wangu ishi unavyotaka wewe.
Namuonea huruma huyu kijana, mwishoni nimemwachia achague maisha anayoyataka.Mkuu unaingiza emotional kwenye issue za kisheria
Mali kuwa zako sio lazima uzitafute wewe..... kuna haki ya mali ya URITHI
Ni mali yako halali kabisa
Kuna ndugu yangu baba yao alikufa na alikua na mali nyingi na alikua na watoto watatu, wakike mkubwa na wakiume wawili hawapatani kabisa
Aliacha nyumba, kampuni mashamba na mifugo
Baada ya mshua kufariki dogo akataka mali zigawanywe na kila mtu apewe chake Mahakama ikaridhia sababu ni haki yake.
Kampuni ikathaminishwa kisha thamani ikagawanywa mara tatu na dogo akapewa fungu lake huku kaka na dada yake wakakubaliana kuendelea na kampuni bila dogo
Mashamba, nyumba, mifugo na assets zingine zigawanywa sawa kwa kila mmoja
Dogo kalewea zote nyumba kauza saa hii kawa dalali wa viwanja tu wakati wenzake wanaendelea na kampuni fresh na majumba yao
Hii inamaana HAKI yako haipangiwi namna ya kuitumia
Ukimpangia mrithi namna unayotaka nje ya matakwa yake anakuburuza mahakamani na anapewa haki yake akaichezee anavyotaka