Wakuu wanasheria
Mzee Bingili alikuwa na watoto wawili wa kiume, Kibaki na Kaputi. Akafariki na kuacha mashamba ekari 100 lakini hakuwahi kugawa mashamba kwa watoto wake Kibaki na Kaputi ila waliendele kulitumia shamba kila mmoja akawa analima anavyojisikia.
Kibaki ana mke mmoja na watoto watano na sio mlimaji sana akawa yeye na watoto wake analima kama ekari 30. Kaputi ambaye ana wake wawili na watoto 15 akawa analima sehemu kubwa ya shamba kama ekari 70
Miaka ikapita Kibaki na Kaputi na wake zao wakafariki, baada ya muda kivumbi kikaanza kwa wajukuu wa Bingili yaani watoto wa Kibaki na Kaputi
Watoto wa Kaputi wanadai ekari 70 ni mali yao wajukuu 15 na iliobaki ekari 30 ni watoto wa Kibaki, yaani ibaki kama ilivyokuwa mazoea kulima.
Watoto wa Kibaki nao wanadai shamba ligawanywe katikati kwakuwa babu yao Bingili alikuwa na watoto wawili tu hivyo shamba ligawanywe kwa muktadha wa Kibaki nusu na Kaputi nusu.
Ikumbukwe kwamba Kibaki na Kaputi walikuwa wanapendana sana kama Ndugu hadi kufa kwao hawakuwahi kugombana kisa shamba ukizingatia shamba lilikuwa kubwa sana na walidhani kugawa mashamba ya baba yao ni kama kuleta utengano.
Sasa walipokufa watoto wao wamekuwa watu wazima na ardhi imekuwa na thamani na uhitaji zaidi wa kulima kila mmoja ndio maana vita ikalipuka
Mimi nipo upande wa Kibaki mwezi wa 12 tunakutana kijijini kikaeleweke maana uadui umekuwa mkubwa mno hadi ni hatari.
Naombeni ushauri wenu kisheria imekaaje maana wengine tunatoka mjini Dslamu tunategemewa ndio vichwa na wajuaji wa kumaliza kesi 😂
Nisije kusimamia vitu kumbe havipo kisheria nikaonekana kituko
Ushauri wenu please
Imekaaje hii kisheria