Msaada: Mbinu hii itawezekana vipi kwenye kilimo changu?

nitatoboa kweli

Senior Member
Jul 15, 2023
137
452
Wakuu, nimenunua shamba milimani huko, shida yake hili shamba ni maji, ukitaka kulima mazao lazima usubirie msimu wamvua.

Sasa nataka nilipande mazao ya muda mrefu ambayo yanahitaji kumwagilia kwamiezi kadhaa, bondeni ya hili shamba kuna maji mengi tu.

Je, itawezekana kutumia mbinu gani niweze kuyapandisha juu kwa kutumia rola na umbali wakutoka juu shambani hadi huko bondeni nikama rola kumi hivi.

Wataalamu wa kilimo na maji naombeni majibu ili nijue nafanyaje.
 
Mkuu hili swali ulipaswa utuulize kabla hujawa na shamba mlimani...

Hapo sasa pagumu, kama unataka zao la kumwagilia toka huko kilimani njoo bondeni
.
20230512_232616.jpg
 
Usifanye kosa unaponunua shamba.
Mimi nimefanya kosa moja napo nunua shamba.
Umbali kutoka barabara kuu ni km40 . Mto unapita hapo, hapo. Kama gharama za kuvuta maji ni kubwa panda miti ya mbao tafuta la bondeni.
 
Wakuu, nimenunua shamba milimani huko, shida yake hili shamba ni maji, ukitaka kulima mazao lazima usubirie msimu wamvua.

Sasa nataka nilipande mazao ya muda mrefu ambayo yanahitaji kumwagilia kwamiezi kadhaa, bondeni ya hili shamba kuna maji mengi tu.

Je, itawezekana kutumia mbinu gani niweze kuyapandisha juu kwa kutumia rola na umbali wakutoka juu shambani hadi huko bondeni nikama rola kumi hivi.

Wataalamu wa kilimo na maji naombeni majibu ili nijue nafanyaje.

Fanya hesabu, kati ya utaratibu wa kutumia rola na kununua mota ya kutumia solar. Kipi kitakuwa nafuu kukufanyia kazi kwa eneo husika.

Pia unaweza kuangalia uwezekano wa mimea inayostahimili ukame.
 
Back
Top Bottom