MSAADA: Mama kabadilika baada ya kuwa Mlokole

Ofukozi popote wanapoweza saidiwa ku-reason pamoja panafaa kwa muda huu

Ila asianze kunyooshea mtu kidole, Kaunga ndoa ngumu jamani

Bora kwa wanawake wa sasa waliojiwezesha, ila wale wa kale akikumbana na abyusi hasa za kihisia walikuwa wanakufa nazo kimya kimya. Anaogopa kulalamika jamii haitamwelewa, utasikia wanasema 'yaani mmeo anakukumbuka kwa kila kitu afu unalalamika? una lako jambo'

Sijui kama nafasi ya kuridhishana(kufeel uwepo wa mwenzako ndoani) ilikuwa inapewa kipaumbele kivile, mie naona iko complicated sana hii. Haihitaji haraka wala majibu ya juu juu.

Na point ambayo mama ameshafikia anahitaji uelewa zaidi kuliko hukumu, wakimsumbua wanaweza jikuta mama kahama nyumbani anaenda kuishi chumba kimoja, hii ni kiakili zaidi.

 
Last edited by a moderator:
Pole Sokwe.. Mama yako anahitaji msaada wa haraka hiyo aina ya ulokole sio kabsaa Mungu hatafutwi kwa vitimbwi hivyo.. Chunguza hilo kanisa, mchungaji, waumin jinsi wanavyo endesha mambo ili ujue pakuanzia kumshaur
 

Nakubaliana na wewe kabisa Iron. Imani haiji kwa sababu ya mtu fulani au mchungaji au padre au sijui mtume, imani inakuja kwa njia ya kumwani Kristo. Na ukiristo siku zote unahubiri upendo. Haitoshi tu kudai kwamba mtu ana imani. Imani ya kweli huambatana na matendo. Yakobo aliandika: “Imani bila matendo imekufa.” (Yakobo 2:26). Mtu anapotenda kwa imani akiwa katika majaribu, anasitawisha sifa ya uvumilivu. Ili kufanikiwa, Mkristo anahitaji kumwomba Mungu ampe hekima, akiwa na imani kwamba Mungu atampa. Uvumilivu humfanya mtu akubaliwe na Mungu. Kama unavyosema ndugu yetu mama alikuwa Mkatoliki basi ningekushauri nenda kama uko Dar es Salaam waone EMMAUS CENTER UBUNGO, DAR ES SALAAM, BEHIND UBUNGO BUS TEMINAL VIA UBUNGO DARAJANI. P. O. Box 76255, Dar Es Salaam. Au anaweza kumwona Fr Baptse Mapunda (Tunda la Kanisa) sina uhakika na spelling la jina lake la kwanza
 
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa!!!! Mungu hapendi utengano wa familia na inawezekana anapata mafundisho sio ambayo inamfanya ana act kama anavyofundishwa, ila anahitaji amwombe Roho Mtakatifu amwongoze na asome biblia mara kwa mara kwa uongozo wa Roho wa Mungu.
 
Kama ni makanisa haya mapya ya Efatha, Ufufuo na Uzima,mzee wa upako,mito ya baraka na Gwajima mzee wa misukule yaani ni balaa tupu.Kuna mama jirani yetu ameachana na mume wake kwa sababu eti yeye amepewa kuombea nyumba ya Nabii na Mtume Mwingira kwa hiyo huyo mama anaamka asubuhi na mapema kwenda kuhudumia nyumba ya mchungaji anarudi usiku wa manane na siku nyingine analala huko.Kwa hiyo mume wake ameamua kumpiga chini maana sasa kwa kifupi ni kwamba mume wake anaona mke yupo responsible kwa Mwingira kuliko kwa mume wake.Haya makanisa haya mapyamapya yana mambo ndugu zanguni yaani muwe macho sana.
 

Tuko umeeleza vizuri kabisa. Kwa kuongezea kwenye red, makanisa haya yanayojiita ya kiroho yenye watu wanaojiita mitume na manabii yanatumia matatizo ya watu kujiendeleza. Amini usiamini, mtu mzima kuamua kuokoka ujue kuna kitu kiko nye ya uwezo wake kukisolve na anafikiria kanisa ndo kimbilio la mwisho. Hapa kutakuwa na mgogoro wa kifamilia kati ya baba na mama ambao umekuwa na kupelekea mama kuwa frustrated na kutafuta tulizo kanisa. Pia, inaonekana mama hawaamini hata watoto wake kwani matatizo ya wazazi angewaeleza kwa kiai fulani. Sisi tunatua migogoro ya wazazi wetu kwa sababu ni wa wazi kwetu.
 
Nashukuru kwa ushauri wenu wapendwa ila Nina mtihani mgumu, mama yangu alikuwa muumini wa kawaida sana! Sasa tangu ameingia makanisa hayo anarudi vumbi tupu, nikiongea nae kwa simu ni jina la yesu mwanzo mpaka mwisho wa maongezi, hata sielewi kwa kweli, ila nashukuru sana kwa kunitia moyo.
 
Mama yangu Ana miaka 58, inawezekana Ana frustration kwenye ndoa yake siwezi kataa japo sina ushaidi , ila ktk maisha yangu yote sijawahi kuona wazazi wangu wakigombana kwa kweli, sijawahi kuona baba yangu akirudi nyumbani usiku wa manane, amechelewa ni saa 2 usiku na Sio mlevi, ni mtu anayesaidia sana wenye shida na ni mwepesi kusamehe, japokuwa naishi mbali na nyumbani sidhani Kama amebadilika na amekuwa akinisisitiza sana nirudi nyumbani Ili niweze kumsaidia biashara zake kwani amechoka kusafiri.
 

Asante sana Mwana Mtoka Pabaya kwa maelezo yako mazuri na ya kujenga kiimani. Maana huyu mwenzetu alianza kutuposha kwa imani zake za kuamini RC si kanisa la kweli na imani zake za kila kitu ni uchawi au mashetani. Sina maelezo zaidi bali kumwomba mtoa hoja hasifuate maelezo ya huyu Mbetwa
 
Ndugu hilo tu ndo linakupa pressure wala usiwaze sana..mbona..kimsingi huyo bi mkubwa wako..anasumbuliwa na kitu kinaitwa wokovu wa mwanzoni..yani kile kiraruraru cha baada ya kuokoka nin na viru kama hivyo ila namsikitikia kimtindo maana kwa jinsi scenario zainavyokwenda obviously ameingia kwenye kanisa chaka..siku hizi imani imekua hatari sana makanisa mengi na design kama vile wameshamteka hivi maaana kama hata ukihudhuria hayo makanisa point ya msingi ni kutoa sadaka na kupanda mbegu..toa pesa inayokuuma etc etc nkt Yesu baba yake ni Mungu lkn alikua anafanya vitu bure..we kama vipi shikilia imani yako haya kila lenye mwanzo lina mwisho..wa mama wengine kumbe wanatafutaga matatizo wenyenyewe sasa..saa 11 alfajiri hadi usiku ndo kusali gani..tafikiri wanataka kuhamisha mlima..!!!
 
watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa
 
Yaani inahuzunisha sana kuna mama mmoja alikua anaacha mtotto wa miaka 3 na kwenda kwenye maombi kuanzia asubui mpaka usiku. Na anaporudi anakua hana muda na familia, maana anaingia tena kwenye sala binafsi hapo humtoi. Yaani taratibu nyumba inaanza kufanya ufa . Ni ngumu sana kudeal na watu wa namna hii lkn kama ulivyosema king'asti huu ndio muda wa kuchukuliana mizigo sasa kama familia inabidi wamsaidie kwa upendo.
 
mLETA UZI WEWE NI MUONGO TENA MUONGO MKUBWA, ETI ANATOKA SAA 11 ALFAJIRI NA KURUDI USIKU????!!!! PIA ILI TUWEZE KUKUSAIDIA TAJA NA HILO KANISA MF.KWA MAMA RWAKATARE, GWAJIMA, LUSEKELO, KAKOBE,MTUME NYAGA, GAMANYWA, KATUNZI, NABII FLORA etc.
 
eTI BABA YAKO HAWEZI KUWA MCHAWI KWA KUWA NI MFANYABIASHARA MKUBWA SANA????!!!! ANAFANYA BIASHARA ULAYA, MIDLE EAST NA MAREKANI SO HAWEZI KUWA MCHAWI!!!.
 
bABA YAKO ALIACHA KAZI JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI MIAKA YA 8O, FOR YOUR INFORMATION JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKA ILIVUNJIKA MIAKA YA 7O ENZI NA KENYATA, NYERERE NA NDULI IDD AMINI.
 
sEMA TU HUUPENDI ULOKOLE KWA SABABU HUJUI CHOCHOTE KUHUSU WOKOVU A.K.A KUMPOKEA BWANA YESU KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO. WE UNGEULIZA TU NN MAANA YA ULOKOLE, UNGEPATA MAJIBU KWA KIREFU!!
 
 
Ni kweli mkuu una kazi kubwa, maana unaweza ukawa unadili na moshi na kuuacha moto kwingine. Kitendo cha mama kudiriki kumhusisha baba na "mapepo" ya "mwanae" kinaongea mengi sana kuhusu mahusiano yao. Kwa watu ambao wangekuwa wanaishi kwa amani na upendo, mama angekuwa mtu wa mwisho kumshuku baba kwa mambo ya kushetani. Wewe kama mtoto itakuwia vigumu sana kuchunguza na kujua ukweli ingawa ukitulia ukatumia mbinu 'Sophisticated' kidogo utaupata ukweli. Nina wasiwasi amani uliyokuwa unaiona ilikuwa kwa nje, but kwa ndani kulikuwa na "kansa" ilikuwa inawatafuna kimya kimya, na sasa imefika mahali where mother can't hold it any more!!!
 
Pole na matatizo ukirudi kaa na mama yako usimuogope muulize kiini cha tatizo kilianza lini

Imani zingini ni za kutaka mali ya baba yako

Mwisho ulokole mwingine hamna tofauti na uganga wa jadi
 
mm sina cha kuongeza hapo kwani best umeongea mambo muhimu sana kuhusu huyu ndugu yetu sokwe anachotakiwa akae karibu mama yake, na amhoji lakini kabla hajamhoji afanye uchunguzi kwanza kuwa mama yake ameingia dhehebu la namna gani usijejua kuwa anaabudu mashetani au kajiingiza freemason ikiaina pasipo kujua yeye, kwa sababu wengi wa manabii, mitume wa siku hizi wanatafuta pesa na sio kulisha kondoo wa Bwana, na weingi wao hawana wito wowote wamekaa kimaslahi zaidi hivyo awe makini kwa suala hili kisha ndo aanze mazungumzo na mama yake kwa upendo, natumaini atafanikiwa kama atafuata haya. pole
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…