Msaada: Malezi bora kwa wanangu

Msaada: Malezi bora kwa wanangu

Majigo

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
5,519
Reaction score
1,832
Heshima kwenu machief wangu.

Kama mnavyoelewa changamoto za ulezi hasa kwa Kizazi cha hivi Sasa.
Nimekuwa nikitafakari Sana, namna ya kuwapa Malezi bora wanangu, isiwe tu kukidhi mahitaji yao muhimu, bali pia kuwajenga Kiakili na Kimwili,wakawe Vijana werevu , wenye Hekima/Busara Katika Maisha, Ujasiri Na Kujiamini. Kubwa zaidi wawe na hofu ya Mungu
.Jamii bora ni matokeo ya malezi mazuri.

Nitumie mbinu au mfumo gani wa Malezi.

Asante Jigo
 
Weka ukaribu.....mfanye kuwa na urafiki na mtoto wako, itakuwa rahisi kujua yanayomsibu au kuwepo na wepesi wa kukueleza ya kwake. Punguza kutoa amri nyingi...pia ajue limit ya heshma juu yako

Above all, spend more time with them. ukirudi kazini kaa nao ujue kazi zao za school kama unaweza saidia have fun time together.

all the best
 
Kwa Maoni yangu

1. Usiwe unaishi maeneo ya Uswahilini... haya ni maeneo ambayo ni hatari sana wakati mtoto anakuwa.. Kama ni mtoto wa kike Na hili nimeliona Sana na kulishangaa nilipokuwa naenda kutembelea watu.. unakuta mtoto wa kike anakkushika Zipo ya Suruali n.k inabidi umchape na kumkanya kwa hasira

2. Jaribu kuishi mahali ambapo hakuna msongamano wa Watu wengi na Patulivu.. mahali patulivu ni sehemu nzuri sana ya kulelea watoto

3. Weka Limit katika TV ya Nyumbani na Ukiona Kuna Vipindi vibaya vya kimaadili Jaribu kuvicontrol au Weka Password kabisa kama watumia DSTV... yaani kwa kifupi weka Parent Control

4. Kama Watoto wanasoma Hakikisha wanazingatia masomo kwa Wewe mwenyewe kuwa karibu nao na kuwafundisha.. mfano unaweza kumwambia alete daftari lake na unaangalia alipokosa then Unakaa naye na Kuanza kumfundisha..

5. Angalia ni kina nani hasa anacheza nao... mfano unaweza kukuta anacheza na watoto amabo ni watukutu na wakorofi.. tafadhali vunja uhusiano huo.. maana unaleta madhara kwa Watoto wako.. wanaweza kuiga Matendo yao..

6. Mtoto akifikia miaka Miwili Usilale naye yaani wewe na mkeo msilale naye kitanda kimoja.. tafuteni utaratibu alale na wenzake.. maana watoto huanza kujifunza mambo mengi wakifikia umri huo...

7. Kuna wazazi huwa wanaona sifa sana kuwapeleka watoto wao Sehemu za starehe na mkusanyiko wa watu ili wapate raha... mfano kumbi za starehe, swimming n.k.

Mi naona sidhani kama unamjenga mtoto kiakili bali unamfunza Maovu maana anaona Watu wakiwa Nusu Uchi na Wakati wewe huwa unamfundisha ajisitiri na aone Aibu akiwa Uchi ila Unakuwa wa kwanza Kumpeleka Maeneo ambayo Watu wapo nusu uchi kabisa...

8. Usimbane sana mtoto maana hili linaleta madhara baadae.. siku nyingine muache afanye Mwenyewe na anapokuwa anaelekea pabaya mkanye na umwambie Kuwa si vizuri kufanya jambo fulani.. mfano sometimes anaweza akawa ana Graduate shuleni kwao na Siku hiyo kuna Disco baadae Usimkataze kwenda kwenye Disco la Gratuation yao bali mwambie Awahi kurudi Nyumbani asichelewe...

Ila Mtoto anapoanza Kuwa na Tabia ya Kuenda disco mara kwa mara Na unaanza kuona Si kawaida mkataze na mkane asiwe anaenda kabisa.......

HIVYO NDIVYO NILIVYOLELEWA HATA MIMI...
 
Kama ni R.C waunganishe kwenye kikundi cha utoto mtakatifu na kutumikia,walete CD za mafunzo wapende with limitation.
 
ahsante sana chief! Maana naogopa hasa ninapoona vijana wengi wanakosa maamuzi ya njia sahihi ,hata wengine kuamua kuwa mashoga

pia nataka mwanangu mwenye kupenda kujisomea na akili nyingi darasani..yaani awe na akili ya kuweza kujitegemea!

Ahsante kwa nondo zako makin
 
Usisahau mazingira, unaweza ukawa mzazi mzuri lakini mazingira unayoishi....yakaharibu kizazi chako.
 
wapeleke the best school you can afford....wasisitize ibada.....wape vitabu viingi vya ziada vya kusoma including newspapers....washirikishe mipango ya familia.....kula nao chakula kila siku....
 
Kwa Maoni yangu

1. Usiwe unaishi maeneo ya Uswahilini... haya ni maeneo ambayo ni hatari sana wakati mtoto anakuwa.. Kama ni mtoto wa kike Na hili nimeliona Sana na kulishangaa nilipokuwa naenda kutembelea watu.. unakuta mtoto wa kike anakkushika Zipo ya Suruali n.k inabidi umchape na kumkanya kwa hasira

2. Jaribu kuishi mahali ambapo hakuna msongamano wa Watu wengi na Patulivu.. mahali patulivu ni sehemu nzuri sana ya kulelea watoto

3. Weka Limit katika TV ya Nyumbani na Ukiona Kuna Vipindi vibaya vya kimaadili Jaribu kuvicontrol au Weka Password kabisa kama watumia DSTV... yaani kwa kifupi weka Parent Control

4. Kama Watoto wanasoma Hakikisha wanazingatia masomo kwa Wewe mwenyewe kuwa karibu nao na kuwafundisha.. mfano unaweza kumwambia alete daftari lake na unaangalia alipokosa then Unakaa naye na Kuanza kumfundisha..

5. Angalia ni kina nani hasa anacheza nao... mfano unaweza kukuta anacheza na watoto amabo ni watukutu na wakorofi.. tafadhali vunja uhusiano huo.. maana unaleta madhara kwa Watoto wako.. wanaweza kuiga Matendo yao..

6. Mtoto akifikia miaka Miwili Usilale naye yaani wewe na mkeo msilale naye kitanda kimoja.. tafuteni utaratibu alale na wenzake.. maana watoto huanza kujifunza mambo mengi wakifikia umri huo...

7. Kuna wazazi huwa wanaona sifa sana kuwapeleka watoto wao Sehemu za starehe na mkusanyiko wa watu ili wapate raha... mfano kumbi za starehe, swimming n.k.

Mi naona sidhani kama unamjenga mtoto kiakili bali unamfunza Maovu maana anaona Watu wakiwa Nusu Uchi na Wakati wewe huwa unamfundisha ajisitiri na aone Aibu akiwa Uchi ila Unakuwa wa kwanza Kumpeleka Maeneo ambayo Watu wapo nusu uchi kabisa...

8. Usimbane sana mtoto maana hili linaleta madhara baadae.. siku nyingine muache afanye Mwenyewe na anapokuwa anaelekea pabaya mkanye na umwambie Kuwa si vizuri kufanya jambo fulani.. mfano sometimes anaweza akawa ana Graduate shuleni kwao na Siku hiyo kuna Disco baadae Usimkataze kwenda kwenye Disco la Gratuation yao bali mwambie Awahi kurudi Nyumbani asichelewe...

Ila Mtoto anapoanza Kuwa na Tabia ya Kuenda disco mara kwa mara Na unaanza kuona Si kawaida mkataze na mkane asiwe anaenda kabisa.......

HIVYO NDIVYO NILIVYOLELEWA HATA MIMI...

Ahsante Sana Chief
umezungumzia suala la urafiki usio bora!..je inaweza kuwa sahihi kutafuta watoto ninaoona wanafaa na kuwaunganisha na mwanangu ili wawe marafiki?

Pia umedokeza kumpeleka mwanangu sehem za starehe!...Je ni maeneo gani naweza mpeleka mwanangu?..kama unavyojua nae anahitaji kulifresh mind!

Nakupa hongera mkuu maana inaonesha namna gani malezi ya wazazi wako , yanavyokusaidia ktk maisha yako

ahsante Sana Chief
 
Kama ni R.C waunganishe kwenye kikundi cha utoto mtakatifu na kutumikia,walete CD za mafunzo wapende with limitation.

Ahsante Sana Chief! Bila shaka Wanatoa Mafunzo ya kiroho huko!:.bahati mbaya iman yangu hainiongozi huko
 
Usisahau mazingira, unaweza ukawa mzazi mzuri lakini mazingira unayoishi....yakaharibu kizazi chako.

hapo nimekuelewa chief!...nazani hata RGforever alilenga hii point kwa kunishauri kutojichanganya maeneo ya uswahilini na yenye muingiliano mkubwa wa watu
 
Last edited by a moderator:
Wadau wengi hapo juu wametiririka ipasavyo ila jambo la kukazia ni DINI=watengenezee mazingira ya kumuabudu MUNGU!
 
Ahsante Sana Chief
umezungumzia suala la urafiki usio bora!..je inaweza kuwa sahihi kutafuta watoto ninaoona wanafaa na kuwaunganisha na mwanangu ili wawe marafiki?

Hapana si vizuri kumtafutia Marafiki wa kucheza nao mwache Atafute mwenyewe...maana mtoto hawezi kuwa na rafiki mmoja tu wapo wengi na miongoni mwao wapo Wazuri... ila angalia hao Marafiki aliowatafuta je wana maadili.. mfano mzuri ni mdogo wangu mwenyewe. Alikuwa na rafiki ambaye alikuwa na tabia mbaya.. alipofika O level mama akamkanya kutokuwa na Mazoea na Huyo Rafiki yake maana Huyo rafiki yake Alifikia Kipindi anavuta Sigara na bangi na kwenda Sehemu chafu za starehe kila wiki.. mama alipoona hayo akamkanya... maana mama yangu ni rafiki wa baba wa mtoto huyo aliyeshindikana..

Ila mama Akamwambia mdogo wangu kuwa Ana rafiki wengi asome na rafiki yake fulani maana yule anapenda kusoma na anajitambua...

Nakuambia kweli.. mdogo wangu aliaacha na huyo jamaa na Baadae huwezi amini.. Yule mtoto alikuja kuchomwa kisu na kufariki mwaka Jana 2014 na tushamzika .....

Kwahiyo usinyang'anye marafiki ila mchagulie aliyebora..

Pia umedokeza kumpeleka mwanangu sehem za starehe!...Je ni maeneo gani naweza mpeleka mwanangu?..kama unavyojua nae anahitaji kulifresh mind!

Nakupa hongera mkuu maana inaonesha namna gani malezi ya wazazi wako , yanavyokusaidia ktk maisha yako

ahsante Sana Chief

Kuna sehemu kwa Ajili ya Watoto mfano Picnic za Watoto unakuta ni watoto wamekusanyika na wazazi wao wanafurahi... au unakuta kuna Tamasha kwa ajili ya watoto mpeleke maeneo hayo akakutane na wenzake...

Ila Mimi nilikuwa nazungumzia kuna baadhi ya wazazi wanawapeleka watoto wao sehemu za machanganyiko wa Watu.. mfano Hapa watu wazima Wanafanya mambo yao.. mara wana kissiana mara hili mara lile vyote vya kiutu uzima na Mtoto anaangalia ukiuliza unaambiwa Utandawazi...

Sasa kwa mtoto Inamuharibu kisaikolojia na baadae ndo wageni wa heshima wakija Nyumbani kwako mtoto anakuahibisha kwa kuongea Maneno machafu n.k n.k
 
Sijaelewa vigezo vilitumika mpaka @mods ...kuitenga hii topic toka jukwaa la MMU!....au ndio matokeo ya malezi uliyopewa na wazazi wako?...naongea na @mods
 
Back
Top Bottom