Msaada: Mabosi wawili kazini, yupi wa kumfuata. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada: Mabosi wawili kazini, yupi wa kumfuata.

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by kisu, Dec 15, 2011.

 1. kisu

  kisu JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 803
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Salam wana JF. Mimi ni mhasibu katika kampuni ya kimataifa hapa ughaibuni. Kabla hajaja bosi wa pili, huyu bosi wa kwanza (Resident Manager) na pia anamiliki 35% ya local branch na ana power of attorney (anaweza kusaini cheki na mambo mengine) nilikuwa nampelekea Ripoti za kila mwezi (outstanding invoices na Income Statement). Alipokuja bosi wa pili hata yeye ana power of attorney (March 2011) ku replace nafasi ya bosi wa kwanza (Resident Manager) na bosi wa kwanza kuwa (Advisor) kwa mapendekezo ya partners, mimi niliendelea kuwapa ripoti za mwezi wote wawili. Karibu miezi miwili iliyopita bosi wa pili alinikataza kumpa ripoti za mwezi bosi wa kwanza na ripoti zote zipitie kwake, lakini bosi wa kwanza hataki na anataka nimpe ripoti directly (anasema company law inamruhusu) bila kupitia bosi wa pili. Nna waheshimu mabosi wote wawili, na inaonyesha wana uhasimu hapo kazini. Tafadhalini msaada kwa anaejua sheria. Asanteni.
   
 2. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Kwa mujibu wa barua yako ya ajira, masharti ya kazi wamekuelekeza kuripoti kwa nani? Unatakiwa kuripoti kulingana na barua yako ya ajira na hiyo ndiyo utaitumia kama kinga ikitokea jambo lolote la kisheria. Pamoja na hayo, unatakiwa upeleke report kwa "immediate bosi". Bosi ambaye wewe unaripoti kwake katika utendaji wako wa kila siku. Advisor wa kampuni hawezi kuwa immediate boss. Tafuta sheria au standing orders za hiyo kampuni uzisome. Organization structure ya hiyo kampuni imekaaje?
   
 3. kisu

  kisu JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 803
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Wabeja (Asante) Ngeleja.

  Kuhusu barua yangu ya ajira ni ya zamani (kabla bosi No 2.) na inasema niripoti kwa bosi No 1. Standing orders hakuna, kazi/shughuli ni kwa mazoea tuu. Hii ni kampuni ya kimataifa inayojishughulisha na mambo ya ushauri wa ujenzi (Consultancy Architects & Engineers) ina Head Office Beirut na imesambaa Middle East, Europe na USA. Hapa kwetu ni branch ndogo na Design Services zinafanywa katika regional branches ambazo ni kubwa na ina staff wengi, branch nyingi zipo semi autonomous.
   
Loading...