Hii kitu ninakutana nayo sana. Hawa mobogenie wameweka web ads ambazo ukiclick automatically unakua umetrigger download yake.
Kwa Opera Mini users hatuna shida kwa sababu client side download dialog inatokea before any download, inayokuruhusu kubadilisha target directory ya kupakua faili.
Kwa browsers nyingine zisizo na hiyo option, kama ya android, ujanza ambao ningeweza kutumia ni kuiruhusu idownload mara ya kwanza na kuiacha kwenye default directory ya 'sdcard/Downloads'. Usiidelete.
Itakapotokea ukakutana na hiyo link tena, kabla ya kudownload itashtukia kuwa hilo faili (lenye jina hilo) tayari lipo kwenye hiyo directory hivyo lazima itakuuliza kama unataka kucover the path. Huo ndo upenyo wa kucancel.
Pia nimetumia UC browser, na kwenye pitapita zangu nadhani unaweza fanya hivi:
Kwenye settings za downloads za uc browser kuna mahali unaselect kurename file before download. Enable hii option, ili kila unapotrigger download yoyote ikuletee jina lake na kukupa option ya kubadilisha jina prior to download. Kwahyo hawa mobogenie wakijileta unawastukia.
Kwa fasta fasta ndo nlichoweza kufikiria. If this works, rep me up!
Mrejesho tafadhali.
Summary: tafuta mechanism yoyote ya kuinterrupt downloads kabla hazijaanza.
PS: Sidhani kama ad blockers zitazuia hii kitu.