Msaada: Kwa waliowahi kufunga ndoa ya Serikali

Msaada: Kwa waliowahi kufunga ndoa ya Serikali

Habari za jioni wakuu, awali natoa pole kwa pilika za kutwa kwa ujumla wake.

Kama mada inavyojieleza hapo juu.

Naomba kufahamishwa kuhusu vigezo na masharti ya kufunga ndoa ya kiserikali.

Zaidi ya yote naomba kujua nani anaifungisha ndoa hizo na ni wapi then unahitaji nini ili uweze kufunga ndoa hiyo.

Natanguliza shukrani
Anayefungisha: Msajili wa Ndoa
Masharti:
1. Asiwe ndugu yako,
2. Asiwe mke wa mtu,
3. Isiwe ndoa ya mkataba, au ya muda mfupi
4. Asiwe mtoto. Kama unamke lazima ajulishwe na atasign kwenye mkataba wenu wa ndoa
5. Ndoa itatangazwa kwa siku 21
6. Ni lazima uwe na wasimamizi wakati wa ndoa
Wengine waongeze..
 
Nenda Na mwenzi wako Ofisi ya Mkuu wa wilaya ambayo mnategemea kufunga ndoa yenu mkifika pale mtapewa maelekezo yote Na msajiri wa ndoa.
 
Mkuu kwanza tafuta barua za kukutambulisha kutoka serikali za mtaa. Barua iwe na picha yako na ya mwenza wako. Majina yenu halisi ni muhimu. Gharama inategemea haraka yako . Kama unataka tangazo lifanywe Mara 3 basi gharama ni 50000 ( hii nadhani inaweza kupanda au kushuka kutokana na wilaya au thamani ya shilingi sins uhakika). Kisha unapeleka halmashauri huko utaambiwa nani ni muhusika. Siku ya ndoa utatakiwa kuwa na mashahidi ( wewe moja na mkeo moja).

Ndoa ya serikalini ni rahisi na husaidia sana hasa kwenye bima kama moja wenu kaajiriwa na mwingine hana ajira. Au kama mkeo Ana ujauzito bima inaokoa sana
Ndoa zote ni za serekari mchungaji au shehe wanapewa dhamana ya kuiwakilisha serekari kwenye Ndoa hizo mkuu
 
Hii ya serikali ntafunga kumbe ni simple tu
Tena mkiamua mnabeba mtu yeyote yule mtaani kwenu na sio lazima iwe public, unaambiwa ukitaka ndoa ya haraka unalipia 100,000/= tu ndoa inafungishwa baada ya kulipa.
 
Kumbe hizi nazo matangazo mpaka siku 21 kama kanisani? Mi nikajua unalipia 50000 then unafunga ndoa!
Mchungaji au shehe anafungisha ndoa kwa niaba ya serikali, na anae toa cheti cha ndoa ni serikali yenyewe.

Tunaenda kanisani/msikitini kwa sababu za imani zetu tulizo nazo. Maana ukifunga ndoa ya serikali kwenye dini hiyo ndoa haitambuliki.
 
Ndoa zote ni za serikali, na ndio maana cheti kimeandikwa Jamhuri.........na nembo ya Taifa Tanzania......sema ni nyie mnataka kufunga kwa namna gani , Bomani, Masjid au Kanisani........taratibu zote zinafanana.........kumbuka iwe kanisani au masjid......tangazo lazima litoke kwenye ubao wa matangazo wilayani (Bomani)
 
Anayefungisha: Msajili wa Ndoa
Masharti:
1. Asiwe ndugu yako,
2. Asiwe mke wa mtu,
3. Isiwe ndoa ya mkataba, au ya muda mfupi
4. Asiwe mtoto. Kama unamke lazima ajulishwe na atasign kwenye mkataba wenu wa ndoa
5. Ndoa itatangazwa kwa siku 21
6. Ni lazima uwe na wasimamizi wakati wa ndoa
Wengine waongeze..
Mkuu Mtui kwenye process ya kufunga hii ndoa ya bomani, kuna kuvishana pete?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom