Msaada kwa wale wataalamu wa iphone, napakuaje mp3

Ukiwa na simu yenye android unakuwa upo kwenye upande wa convenience na ukiwa na iphone unakuwa upande wa inconvenience.
 
Hivyo ndivyo inakuwa mkuu ila utazoea na kuona kawaida baada ya muda.

nilijua ukiwa umedownload nyimbo zinakuja kwenye simu mojakwamoja kumbe zinakaaa kwenye app husika ukiihitaji ni mpk ufungue tena app apo ndio naona mazoez kwan lile file lao la music lina kazi gani
 
nilijua ukiwa umedownload nyimbo zinakuja kwenye simu mojakwamoja kumbe zinakaaa kwenye app husika ukiihitaji ni mpk ufungue tena app apo ndio naona mazoez kwan lile file lao la music lina kazi gani

Umenichekesha iPhone music sio bure ,unalipia huduma so file hilo la music kama unataka music subscribers ni usd kwa mwezi
 
Umenichekesha iPhone music sio bure ,unalipia huduma so file hilo la music kama unataka music subscribers ni usd kwa mwezi
Hiyo ni apple music..jamaa anayosemea ni music player app inayokuja kama default app,ambayo inacheza nyimbo zilizopo kwenye simu baada ya kuamishwa kutoka device moja via itunes
 
Hakuna simu rahisi kudownload music kama iPhone. In fact hauhitaji kudownload apps yoyote kwa ajili ya kufanya hivyo. Fuata hatua zifuatazo then utaninunulia pepsi baridi siku yoyote tukionana.

1. Nenda kwenye iphone yako bofya app inayoitwa music.

2. Nenda kwenye sehemu iliyoandikwa Search

3. Andika jina la msanii au wimbo unaotaka kumbuka kubofya button ya apple music wakati unafanya search.

4. Ukishafunguka huo wimbo au kama msanii atakuja na orodha ya nyimbo zake. Kwa upande wa kulia utaona plus icon. Ukibofya hiyo icon itakuletea alama ya tick kwamba umeshaichukua hiyo nyimbo na itakua kwenye library yako. Ila kama unataka kuipakua unaweza kuendelea kubofya alama itakayotokea baada ya kubofya ile plus icon.

Uzuri wa music apps ya iphone inakupangia folders kwa namna mbali mbali, mfano kwa msanii, nyimbo, albums, etc.

NB. Kama msanii hayupo kwenye Apple Music platform au nyimbo hiyo hajaupload huko basi hutoweza kuikuta. So usitegemee kupata kila nyimbo haswa hizi za kwetu africa
 
Wengi wenu mnaipinga iphone lakini, simu hii inahitaji, uwe mtu mwenye shauku nayo na mdadisi ndiyo utaifurahia, lakini kama unaitumia, ukitegemea ifanane na Android itakuwia vigumu kuendana na mazingira yake.

Mimi ni mtumiaji wa Android kwa miaka mingi, lakini iphone pia nimetumia kupitia friends, wakipata changamoto kwenye matumizi. Nachoweza kusema ni kwamba,kila OS ina ladha na utofauti wake lakini usitegemee mazingira ya Android yakafanana kivyovyote na iOS, kila OS ina utofauti wake na huo utofauti ndiyo unaifanya OS hiyo i-stand out.

Kwa kuongezea kidogo, kuna kipindi ambacho Windows phone ilikuwa popular kwenye soko, watumiaji wengi walilalamika Windows Mobile OS ni ngumu sana, bora "Andrioid" lakini mlikosa bahati kubwa sana ya kufurahia OS iliyokuwa kwenye prime yake, mpaka ikapotea sokoni wengi wetu walisema Windows Mobile ngumu lakini hawakuwa na shauku ya kuifurahia labda kutokana na matarajio waliyotoka nayo Android, na kipindi hicho android haikuwa polished kihivyo.
 
naombeni msaada wa jinsi ya kupakuwa nyimbo yani mp3 na video nina kaiphone 6 kangu hapa nataka kufahamu juu ya hilo asanteni......

Tumia hii ndo the best kwa iphone
Documents

 
Back
Top Bottom