Msaada kwa mkaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada kwa mkaka

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by chetuntu, Mar 30, 2011.

 1. c

  chetuntu R I P

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hamjambo wapendwa, hope wote mmeamka bien, kwa wagonjwa na matatizo mbalimbali poleni. Leo nimepata kisa kimenitatiza kidogo naomba kushare nanyi wapendwa tumsaidie huyu ndugu. Huyu mkaka amezaa na mke wa mtu bila mume kujua na wote wanaendelea kumtunza mtoto sasa ana umri wa miaka mitano. Tatizo mdada anaogopa kusema ukweli kulinda ndoa yake, na mkaka (mwizi) anataka atambulike kwa mwanae japo na yeye ana mke.Mke wa mwizi keshaelezwa kuna mtoto nje kakubaliana na hilo japo hajui ni wapi/ kwa nani. Na familia ya mdada inajua kila kitu.Familia ya kiume na mke wa mwizi imekomaa inataka kumuona huyo mtoto. Mume wa dada hana ajualo. Nisaidieni kaka aanzie wapi, na familia ya mkaka mwizi na mdada ni marafiki toka udogoni..

  Nawasilisha.
   
 2. N

  Ntali Member

  #2
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkaka mwizi akatae kuonyesha ndugu zake huyo mtoto vinginevyo ndoa ya mdada mwizi itavunjika!
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mwambie warudi nyuma wakaUNDO madudu yao...wote wawili!
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Kama familia ya huyo dada inajua kila kitu, jambo la muhimu ni huyo dada kumueleza mume wake ukweli akishirikiana na ndugu zake, ila awe tayari kwa lolote litakalotokea.
  Kwa huyo kaka nae awe jasiri ashirikiane na huyo dada aliyezaa nae kumueleza mume wake kuhusu mtoto....
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Haya ndio matokeo yenyewe yanayotarajiwa..
   
 6. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  Imekaa vibaya
  mwanamke anayezaa nje ya ndoa kupata msamaha kwa mumewe ni ngumu
  nahisi harufu ya talaka hapo
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Kuna uwezekano wa kuUNDO kweli!!! Wawe tayari kupambana na matokeo...
   
 8. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  WataUNDO vipi
  halafu nashangaa huyo mume hajagundua chochote miaka yote
   
 9. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #9
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Na kama mwanaume ni mwenye hasira hata mauaji yanaweza kutokea.
   
 10. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  Katavi
  ingekuwa wewe ungefanyaje
   
 11. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  mbona mkaka tu ndo anaitwa mwizi kwenye hii post? huu ni ubaguzi wa kijinsia.

  ushauri zaidi nitatoa baadae.
   
 12. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #12
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  duuuuh! Hayo ndo maisha! Cna cha kuchangia.
   
 13. c

  chetuntu R I P

  #13
  Mar 30, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  baada ya wazazi wa mdada kujua waliazimia kufanya siri kwa pamoja na mtoto ni kafanana na mamake .
   
 14. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #14
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  haya wote wevi, ila kwanin wakwibe?
   
 15. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #15
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  kabla ya kuketi kitako kumweleza mumewe inabidi afunge na kusali sana
  kumwombea mumewe aondekana na hasira itakayomakabili
   
 16. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #16
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Inakuwa ngumu sana kwa mwanaume kugundua hasa kama anamwamini sana mke wake. Wanawake wana siri nyingi sana hasa zinazohusu watoto, kuna dada yetu mmoja alipofariki yeye na mume wake, tulishangaa alipokuja jamaa mwingine kudai mtoto kuwa ni wake. Tulikosa la kusema maana mtoto alikuwa ni fotokopi ya yule jamaa, lakini yule mtoto alikuwa anapendwa sana na baba yake aliefariki, sipati picha yule baba angekuwa hai!!
   
 17. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #17
  Mar 30, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Duh!
  Hii movie mbona kali hivi.
  Steringi lazma adedi.
  Mwambie mkaka mwizi asing'ang'anie kufanya hivyo. Huyo mtoto ni mdogo na ikitokea mdada mwizi ndoa yake imevunjika mtoto anaweza kuwa katika wakati mgumu.
  Inawezekana mke wa jamaa hana mapenzi kutoka moyoni na huyo mtoto na angeletewa alee sidhani kama angekubali.
  Wanachekelea kwasababu wanajua mtoto anahudumiwa huko aliko.
  Waache unafki wao kujifanya wana mapenzi na huyo mtoto.
  Dada mwizi nae hajatulia. Khaa!
   
 18. Obuntu

  Obuntu JF-Expert Member

  #18
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mume B*w*e*g*e*!
   
 19. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #19
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Ningekubali matokeo, ningemsamehe mke na maisha yangeendelea kama kawaida lakini uaminifu ungepungua...
   
 20. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #20
  Mar 30, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  nakukaribisha kwenye jukwaa la lugha.
   
Loading...