Msaada kwa mkaka

mke mwizi ajitaarishe tu kwa lolote
itamfikia 2 bwn wake cz ndugu na jamaa wanajua
dirty
 
kabla ya kuketi kitako kumweleza mumewe inabidi afunge na kusali sana
kumwombea mumewe aondekana na hasira itakayomakabili
Hapo maombi yanahusika, na ikibidi viongozi wa dini wahusishwe wakati wa kumueleza mume ukweli.
 
Hamjambo wapendwa, hope wote mmeamka bien, kwa wagonjwa na matatizo mbalimbali poleni. Leo nimepata kisa kimenitatiza kidogo naomba kushare nanyi wapendwa tumsaidie huyu ndugu. Huyu mkaka amezaa na mke wa mtu bila mume kujua na wote wanaendelea kumtunza mtoto sasa ana umri wa miaka mitano. Tatizo mdada anaogopa kusema ukweli kulinda ndoa yake, na mkaka (mwizi) anataka atambulike kwa mwanae japo na yeye ana mke.Mke wa mwizi keshaelezwa kuna mtoto nje kakubaliana na hilo japo hajui ni wapi/ kwa nani. Na familia ya mdada inajua kila kitu.Familia ya kiume na mke wa mwizi imekomaa inataka kumuona huyo mtoto. Mume wa dada hana ajualo. Nisaidieni kaka aanzie wapi, na familia ya mkaka mwizi na mdada ni marafiki toka udogoni..

Nawasilisha.

huwa najiuliza sana hili swali,
hivi inakuwaje mnafanya uzinzi mpaka kufikia kuzaa nje ya ndoa,
kule kuzini tu ni tatizo na dhambi kubwa, sasa ndo iwe mpaka kuzaa jamani?
Hii kitu huwa siielewi kabisa!!!!!!!!!!!
 
baada ya wazazi wa mdada kujua waliazimia kufanya siri kwa pamoja na mtoto ni kafanana na mamake .

Huyo kaka atakasirika sana kwa kujua hata wakwe, shemeji walikuwa wanajua
jambo hilo kwa muda mrefu.
inanikumbusha story ya wazee wa zamani wa uchagani
kulikuwa na tabia ya kuzaa nje ya ndoa mtoto mmoja
ili ikijatokea tambiko au laani mbaya kwa familia kuwepo na
mtoto atakaye kuwa mrithi
labda hao ndugu wa huyo mdada wametumia kigezo hiki cha kale

Ahahahaaaaah!!! Si unajua kila baya lolote linalotokea katika jamii yetu tunalaumiwa wanaume!![/QUOTE]

Kumfukuza mkeo wa ndoa na kwenda kuoa mke mwingine ni lawama kwa wanaume
au kumpa msichana mimba na kukata nayo ni lawama usisahau kuzaa nje ya ndoa na kuja kumweleza mkeo akakusamehe
 
WataUNDO vipi
Ukisikia watu wa aina hiyo wanaomba ushauri maana yake wanataka mbinu ya kuepuka sakata la talaka na kuonekana wabaya!Hapa hawawezi kufanikisha hilo ndo maana nikasema waUNDO maana kama wasingefanya madudu yao wasingekua njia panda!Wamewasha redio sasa wasikilize mziki wake!Mwanamke ajiandae kwa talaka na aibu juu..na huyo mwizi mwenzake aliyeepuka talaka ajiandae kushea aibu ya mwenzake na kumsaidia kubeba talaka!FULLSTOP!
 
Huyo mdada amefanya makosa makubwa sana. Kwanini amesubiri mtoto mpaka amefikia umri wa miaka mitano? Mume wake amemzoea na anajua ni mtoto wake na pia amemuhudumia kwa kila kitu. Leo ghafla aambiwe kuwa mtoto si wako hapo ni mauaji tu!!!!! Hakuna muamana hapo. Kingine hata mtoto mwenyewe naye aambiwe huyu si baba yako ila baba yako ni huyu, kwa kweli kisaikolojia mtoto ataadhirika. Katika hali ya kiubinadamu mtu utakayekuwa naye tangu mdogo kwa ukaribu hata kama si ndugu yako lakini tangu utoto mlikuwa pamoja, mkasoma wote hadi chuo, kiukweli mnakuwa na upendo mkubwa sana kuliko ukioneshwa ndugu yako ukubwani, inakuwa vigumu kuwa na upendo kama yule rafiki yako uliyekuwa naye tangu utotoni.

ushauri:
wazazi wa mke wakutane na wazazi wa mume wazungumze kwanza; nina hakika hakitaharibika kitu watalumbana, lakini hatimaye watafikia muafaka. Baada ya muafaka wa wazazi, hapo ndipo wazazi wa mume wakae waongee na mwanao wamfahamishe hali halisi ya kuwa mtoto si wake, najua atapaniki lakini lazima hatimaye atafikia muafaka na wazazi wake. Hayo yote yakifanyika hakutatokea madhara ya mauaji bali talaka inawezekana ikatokea.

Huyo mke naye aache ukware, yeye ameolewa anahangaika nini? Na wewe kijana nawe una mke ukware wa nini?
 
Hamjambo wapendwa, hope wote mmeamka bien, kwa wagonjwa na matatizo mbalimbali poleni. Leo nimepata kisa kimenitatiza kidogo naomba kushare nanyi wapendwa tumsaidie huyu ndugu. Huyu mkaka amezaa na mke wa mtu bila mume kujua na wote wanaendelea kumtunza mtoto sasa ana umri wa miaka mitano. Tatizo mdada anaogopa kusema ukweli kulinda ndoa yake, na mkaka (mwizi) anataka atambulike kwa mwanae japo na yeye ana mke.Mke wa mwizi keshaelezwa kuna mtoto nje kakubaliana na hilo japo hajui ni wapi/ kwa nani. Na familia ya mdada inajua kila kitu.Familia ya kiume na mke wa mwizi imekomaa inataka kumuona huyo mtoto. Mume wa dada hana ajualo. Nisaidieni kaka aanzie wapi, na familia ya mkaka mwizi na mdada ni marafiki toka udogoni..

Nawasilisha.
CHETU,
Nawajibika kumpa ushauri huyu Mkaka, Asahau kuhusu huyo mtoto kama kweli anampenda huyu mdada, Na kwa kuwa mkaka mwizi ana ndoa yake na ni nzuri tu, Aendelee kuongeza watoto kwa mke Halali, Kitendo anachotaka kufanya kitamsaidia nini? Anataka idadi ya watoto au anamtaka huyo mtoto aliyezaa na mke wa mtu? Je anajua nini kitatokea kwa huyu Mdada? Kama anampenda kweli aachane kabisa na wazo la kumtaka huyu mtoto, isitoshe ni mtoto katika ndoa ya mtu! Unawezaje kudai mtoto katika ndoa ya Mtu?
 
Ukisikia watu wa aina hiyo wanaomba ushauri maana yake wanataka mbinu ya kuepuka sakata la talaka na kuonekana wabaya!Hapa hawawezi kufanikisha hilo ndo maana nikasema waUNDO maana kama wasingefanya madudu yao wasingekua njia panda!Wamewasha redio sasa wasikilize mziki wake!Mwanamke ajiandae kwa talaka na aibu juu..na huyo mwizi mwenzake aliyeepuka talaka ajiandae kushea aibu ya mwenzake na kumsaidia kubeba talaka!FULLSTOP!

Kwa sababu na mke wa huyo mwizi ameridhika sio mbaya akikubali uke wenza pia
 
Huyo kaka atakasirika sana kwa kujua hata wakwe, shemeji walikuwa wanajua
jambo hilo kwa muda mrefu.
inanikumbusha story ya wazee wa zamani wa uchagani
kulikuwa na tabia ya kuzaa nje ya ndoa mtoto mmoja
ili ikijatokea tambiko au laani mbaya kwa familia kuwepo na
mtoto atakaye kuwa mrithi
labda hao ndugu wa huyo mdada wametumia kigezo hiki cha kale

umegonga ikulu mkuu,
 
Jamani let us be serious!!! Yaani wewe umetoka na mbegu zako ziwe mtama, uwele au mahindi na ukaamua kuja kuziotesha kwenye shambe la mtu mwingine ukiwa na akili zako timamu, utamdai mwenye shamba kwamba hayo mazao ni ya kwako? Huyu jamaa MWIZI ingawaje wengine hawataki na jamaa zake wakubali matokeo kwamba mtoto ni wa jamaa ambaye hajabaini mabo yaliyojiri shambani kwake. Kwenda kudai mtoto namna yeyote ile bifu lake litakuwa kali sana. Kwanza ataona kama amedhalilishwa!!! Vinginevyo jamaa naye anaweza kulipa kisasi kwa style hiyohiyo je, huyu mwizi atakuwa tayari? Jambo la namna hii lilishatokea mahali fulani. Jamaa aliyeibiwa aliye ibiwa alijifanya hajui lakini kumbe ilikuwa janja yake. Akaamua kuzaa na mke wa mwizi na mke alipojifungua alienda hospitali kumpongeza na akataka jamaa ajue kwamba naye amejibu mapigo
 
Back
Top Bottom