Msaada kwa Athuman Hamis

mwaJ

JF-Expert Member
Sep 27, 2007
4,074
2,947
Wanajukwaa la Sheria, hii ni thread toka jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko, nimeona niilete huku:

Kuna ndugu yetu anaitwa Athumani Hamisi. Sasa ni miaka minne tokea apate ajali, Septemba 12, 2008 eneo la Kibiti Mkoani Pwani akiwa na wenzanke, wakiwa njiani kwenda kazini Kilwa mkoani Lindi kikazi.Katika ajali ile, alivunjika shingo naku-damage spinal cord iliyopelekea kupooza mwili wote kuanzia shingoni. Ailipata msaada wa moja kwa moja toka Ikulu (Mhe Jakaya Kikwete), Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kampuni alio kua akifanyia kazi ya magazeti ya serikali (TSN).

Sasa tatizo lake kubwa ni kukabiliana na gharama za maisha zinazo sababishwa kwa kiasi kikubwa na ulemavu alio upata baada ya ajali. Anahitaji pesa ya matibabu, pesa ya kuwalipa wahudumu, pesa ya kuwasomesha wanae watatu na pesa ya matumizi mbali mbali ya nyumbani, ikiongozwa na gharama za kodi ya nyumba pamoja na chakula mbazo kazikadiria kufika laki tisa kwa mwezi (900,00 Tsh).

Kwa bahati mbaya, leo miaka minne baada ya kupata ajali hiyo inaonekana TSN na wafadhili wengine wameanza kuonesha dalili ya kugeuka wajibu wao wa kumsaidia mfanyakazi wao huyu, aliejeruhiwa katika safari ya kikazi. Nadhani hali hii inarahisishwa na kutokuwepo kwa makubaliano ya msingi (na ya kuandikwa) kati ya Ndugu Athumani na tajiri wake (TSN). Leo amekua omba omba na msaada uliokua ukitoka kwa urahisi sasa unatoka kwa tabu.

Msaada anao hitaji ni wa kisheria (for a sustainable life, in the long term), na wa kifedha (to implement the legal advices and to cope with the daily expenses as he works on the long term plan)
Msaada wa kisheria unao hitajika:
  1. Ufafanuzi wa haki zake kama mfanya kazi alie pata ajali akiwa kazini
  2. Ufafanuzi wa uwajibikaji wa TSN kama tajiri wake (ukizingatia walianza kulipia huduma na sasa wanaacha)
  3. Hatua za kuchukua ili haki na uwajibikaji vizingatiwe kwenda mbele
  4. Ufafanuzi wa compensation scheme inayo weza kutumika hapa (monthly allowances au one off package)
  5. Msaada wa kisheria (free of charge or at very accessible cost given the situation)
  6. Msaada wa kimawazo au kifedha toka kwa msomaji wowote atakae guswa na habari hii.

Kwa walio tayari kuchangia kimawazo/kisheria, tafadhali weka mawazo yako kwenye thread hii au tembelea http://www.8020fashions.blogspot.com/

kwa walio tayari kuchangia kifedha, misaada ipitie katika


  • account No 01J2027048800 ya CRDB na
  • Account No 010-00090488 ya Postal Bank


​Kwa wanaotumia mitandao ya simu, wanaweza kutumia


  • M-pesa 0757 825 737,
  • Tigopesa 0655 531 188 na
  • Airtel Money 0784 531118;
  • M-Pesa 0767 298 888 ya Chris Mahundi na
  • Airtel Money 0686 710 977 ya Ephraim Mafuru.

​
Asanteni kwa michango.
 
Mods tafadhali msiziunganishe hizi threads. Tunahitaji michango mingi zaidi kutoka majukwaa yote mawili.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom