Sina hakika mahala ulipo,ila Kwa jinsi ninavyofahamu mimi, mara nyingi bidhaa zinazouzwa eBay huwa hazisafirishwi kuelekea maeneo mengi ya Africa,isipokuwa endapo muuzaji ameeleza wazi kwamba anaweza kuship to Africa.
Kwamaana hii, unaweza kuangalia kwenya account yako ya eBay kama hiyo bidhaa inaonekana imeshakuwa shipped, kama imeandikwa ipo shipped unaweza pia kucheki ni kampuni gani inayosafirisha huo mzigo na pia cheki tracking code ya huo mzigo wako, kisha uwasiliane na kampuni inayosafirisha kwa kuwapa tracking code kisha watakwambia huo mzigo ulipo.
Endapo huo mzigo haujakuwa shipped, au hakuna tracking code basi unaweza kumuuliza muuzaji atakwambia mzigo wako ulipo.
Endapo muuzaji hakupi ushirikiano wa kutosha,ndio unaweza kwenda stage ingine kwa kufungua malalamiko kwa eBay.
Inabidi ufahamu kwamba, kama ulifanya malipo kwa PayPal kuna uwezekano mkubwa sana kurudishiwa hela yako endapo utakuwa hujapata mzigo wako.ila kma umelipa kwa njia zingine huwa kuna kuwa na matatizo sana unapohitaji kurudishiwa hela.