manka1
Member
- Nov 4, 2014
- 11
- 23
Habari wana JF,
Mimi ni mwanamke mwenye ulemavu na nina umri wa miaka 45 sasa, nimeolewa nina watoto wawili. Nina miaka 15 sasa tangu niingie kwenye ndoa naona kila siku inavyosonga magumu ya maisha yananizidia.
Mume aliyenioa yeye huwa hayuko tayari kunisaidia shughuli yoyote iwe ya nyumbani au ya kijamii kama kwenda kwenye misiba au shughuli yeyote inayonihusu mimi
Mume huyu ana kazi ya kuajiriwa na mm pia nimeajiriwa siku yote yy husema kazi za nyumbani ni za wanawake naweka mtumishi wa kunisaidia lkn yeye hukataa kumlpa. Pindi akiwa hayupo inaniwia vigumu mno kwani kazi zote inabidi nifanye mimi na nina mguu mmoja mwingine umepooza.
Nimekuja kwenu kuomba msaada wa mawayo kwani hapa nilipo tuna kibanda ambacho nimekijenga mm ika kiwanja kinasoma majina mawili kwa vile niliona ni heshima kuandika jina langu na la mume wangu kwenye hati niliyoitafuta mwenyewe.
Natamani kwa mateso ninayopata niondoke tu nimuachie kila kitu ila nina madeni mengi niliyokopa kujenga na kusomesha watoto ambao hadi ss mmoja yuko sekondari na wa pili msingi.
Nikimtaka atoe hela kwa chochote madai yake hana hela ana madeni mengi ambayo ati amekopa kuamzisha miradi ambayo mimi siijui.Mimi nimesoma nina shahada ya ualimu ktk sayansi pia nina shahada ya uzamili ktk mambo ya ustawi wa jamii.
Natamani nipate kazi mahali fulani mbali nhame na watoto tumwache kwani wanangu wanaishi kwa mkazo rana wakimuomba hela ya matumizi yeyote anawatukana nikimwambia mm ananitukna, anarudi usiku anakula, kuoga na kulala hata kama hela hajatoa kwa madai kuwa ni nyumbani kwake.
Kama kuna yeyote anayeweza kunipa mchango wa mawazo. Nimeandika sasa kwani nina muda sina binti wa kazi narudi kazini nifanye kazi za nyumbani mguu unaniuma na mwenzangu halioni hilo wala hana msaada wowote kwangu.