Msaada kuthibitisha matokeo kidato cha nne

kiumbempole

JF-Expert Member
Jan 15, 2016
588
978
Wadau naomba kwa anayejua ninaweza kufuata utaratibu gani ili nifahamu matokeo halisi ya mtoto aliyehitimu kidato cha NNE Mwaka Jana.

IPO hivi: namba anayotaja mtoto inaonyesha kapata division four lakini kuna Mwalimu alimfundisha amenipigia kunipa pole kwamba mtoto amefeli kapata D moja tu,yaani kazungusha!

Tatizo mtoto anasisitiza kwamba Mwalimu anamsingizia na Mwalimu nimerudia kumpigia anasisitiza mtoto kafeli....! Nimechanganyikiwa natamani nipate matokeo yenye majina ili niweze kuamua vema.
Msaada wenu wadau
 
sh
majina si yapo shuleni yale yalotumika kuwapanga au namba ambayo alikuwa amesajiliwa nayo kwa ajili ya mtihani wa kidato cha nne ina jina ake,so unaweza kwenda shuleni kuthibitisha kwa kuangalia,yeye namba ake ilikuwa ngapi.
Kwa ujumla tupo mbali sana na shule, sisi tunaishi Shinyanga na shule aliyosoma ipo Tanga! kwa hiyo nilikuwa najaribu kupata mawazo ya wadau kama pana njia rahisi zaidi kuyapata bila kulazimika kusafiri (all the way halafu ukathibitishe ni zero :(:(:(....)
 
Wadau naomba kwa anayejua ninaweza kufuata utaratibu gani ili nifahamu matokeo halisi ya mtoto aliyehitimu kidato cha NNE Mwaka Jana.

IPO hivi: namba anayotaja mtoto inaonyesha kapata division four lakini kuna Mwalimu alimfundisha amenipigia kunipa pole kwamba mtoto amefeli kapata D moja tu,yaani kazungusha!

Tatizo mtoto anasisitiza kwamba Mwalimu anamsingizia na Mwalimu nimerudia kumpigia anasisitiza mtoto kafeli....! Nimechanganyikiwa natamani nipate matokeo yenye majina ili niweze kuamua vema.
Msaada wenu wadau
Me niko tanga, mtoto yamesoma shule gani nikusaidie kama itakuwa karibu nami.
 
sh

Kwa ujumla tupo mbali sana na shule, sisi tunaishi Shinyanga na shule aliyosoma ipo Tanga! kwa hiyo nilikuwa najaribu kupata mawazo ya wadau kama pana njia rahisi zaidi kuyapata bila kulazimika kusafiri (all the way halafu ukathibitishe ni zero :(:(:(....)
Hakuna kitu kinachoumiza kwa mtoto kama kufeli.Mara nyingi watoto wanajitahidi wawe kama wenzao wanaopasi,lakini wanashindwa,kuna matatizo mengi yanawakuta watoto wakiwa wadogo kama
1 Kukosa virutubisho muhimu wakati wa mimba akiwa tumboni
2.Kuzaliwa njiti
3.Kukosa chakula bora wakati wa makuzi nk
Usimbane sana,msaidie kama atarudia masomo aje afanye mtihani.
Mtoto aliyefeli ni zaidi ya mtu aliyefiwa na anayemtegemea kimaiasha.Nakuomba sana mfariji,asije akachukuwa hatua zisizofaa.Hakuna anayependa kufeli.Mpe moyo.
 
HAPA yawezekana hakuna ushilikiano mzuri kati mtoto./mwalimu na mzazi. Kwakuwa shule mtaaluma ana jina la Mwanafunzi na ana namba ya mwanafunzi
 
Back
Top Bottom