Msaada: Kutegua Mume toka mapenzi ya kichawi (Limbwata)

Msaada: Kutegua Mume toka mapenzi ya kichawi (Limbwata)

Mke anamdharau mumewe na anakuwa na mamlaka ndani ya nyumba. Mume kawa kama zezeta, hajali ndugu zake! Tumegundua kamuendea kwa mganga na kuroga ili awe na mamlaka juu ya mumewe na mali zake.

Msaada wakuu, kwanini mume anashindwa fanya kitu cha maana zaidi ya kuendeshwa na huyo mke?

Ahsante, Jigo.
Mkuu kosa la huyo mme ni kutowajali ndugu zake?
na kutowajali kuna uwanja mpana,
kuna ndugu wanataka hata ukiishaoa uendelee kuwabeba
achilia wazazi,na ndugu zako hata waliooa na kuolewa wanataka uwabebe
na familia zao huku wakijua fika kuwa na wewe una familia.

Mke akimshauri mmewe nao wafanye maendeleo
ndugu wanaanzisha maandamano eti ndugu yetu kalogwa.
Nadhani ninyi si sehemu ya hao waandamanaji.

Kama kweli kaoa mchawi/ mtumiaji wa limbwata
basi njia pekee ni maombi,mkienda kwa mganga mjue
huyo ndugu yenu mmemkosa,na huyo shemeji
yenu ataolewa mtaa wa pili wakati ndugu
yenu ndo ameondoka hivyo.
 
Mke anamdharau mumewe na anakuwa na mamlaka ndani ya nyumba. Mume kawa kama zezeta, hajali ndugu zake! Tumegundua kamuendea kwa mganga na kuroga ili awe na mamlaka juu ya mumewe na mali zake.

Msaada wakuu, kwanini mume anashindwa fanya kitu cha maana zaidi ya kuendeshwa na huyo mke?

Ahsante, Jigo.
"Msaada kutegua mume toka mapenzi ya kichawi" rangi nyekundu inaonesha mmegundua sababu, blue inauliza swali sasa si mtumie mbinu mlizofanya kwenye ugunduzi mtayatatua wote? bila shaka mtakuwa mmekwenda kwa waganga na kuroga pia
 
Mchapeni bakora tu huyo mwanamke au la kwavile nyie hamjawekewa ili limbwata mtimueni kabla hajawatengeneza na nyie
 
soma vizuri , sio unakurupuka Rohombaya
Khaa!! Sijakurupuka bana. Wewe ndiyo unagawa madaraka nyumbani kwa mtu? Unajua mkataba wao wa maisha? Kusaidia ndugu ni hiyari tu wala si lazima. Bado nakuuliza unajua anachokipata wakiwa faragha? Acha hizo fanyeni kazi kwa bidii mtafute vyenu mle na wake zenu siyo kupenda vya burebure. Mnajua aivipataje?? Mtegemea cha ndugu hufa masikini :msela:
 
Namfahamu jamaa mmoja, yeye akimuona mke wake yaan anatetemeka kabisa utadhan mwanafunzi kamuona mwalimu mkali.Kama alikuwa anaongea sauti mpaka inaanza kutoa kigugumizi, unamuona kabisa moyo wake unaenda mbio kwa homu utafikiri kaona Simba, maisha haya!!.Mke akikohoa tu jamaa anaitikia naam, akiambiwa fabya haraka sana nenda dukani kachukue kitu fulani walai jamaa anakimbia mbio kama msukule live.Watu wana dhambi mbaya sana.


Mke mpaka anapeleka mpaka wanaume wake nyumbani na akiwa na hao wanaume anamtuma jamaa ebu kamnunulie mgeni wangu soda, na jamaa anaenda, ukikutana nae ukamwambia ebu tupige story kidogo atakwambia aisee nitachelewa home, ngoja nikimbie kwanza wife atachukia maana kanituma nimpelekee mgeni wake soda.yaan wanawake wengine ni nuksi.


Jamaa kabla alikuwa mtu makini sana, lakin ata kiuchumi sasa anaporomoka tu maana ni kama ana kitu ndani kafungwa, sio yule tena.Hivyo uliposema hii walai naelewa unamaanisha nin.
 
Back
Top Bottom