Msaada; Kuondoa Pipes Kwenye Kisima Kirefu

Mkuu kesi kama hizi ni nyingi sana watu wamekua hawana uaminifu katika kazi wanaharibia hadi wanao fanya kazi zao kwa uaminifu usimamizi katika hili ni lazima
 
Mkuu kama haukuwepo pengine hakikufika mita ulizotaka ilitakiwa uwepo ujue bomba ngapi zimeingia kila bomba 1 ina mita 3 au jaribu kutafuta kitu ambacho unaweza kupima ili ujue kama kwel walitimiza hizo mita 60
Walichimbia stiki za Mita 2 nilizihesabu 30, wakati wanachimbia nilikua Kibiti Mjini lakini niliporudi shamba nilihesabu pipes zilizobaki. Sawa ntazipima nikienda, ntatafuta tape measure ndefu.

By the way hata nikigundua haikufika 60 sijui kama itasaidia. Manake haya mambo bana mnalipana tu na kazi inafanyika, hakuna any binded written contract.
 
Wakuu kwema??

Ninalo shamba mahali ambako nilipanga nichimbe kisima kirefu kwa ajili ya Kuweka Drip Irrigations System ambako ningekitumia hicho Kisima. Sasa kuna Rafiki yangu mmoja yuko kama kilometer 1 hivi kutoka hapo kwangu alinitangulia kuchimba kisima chake kama miezi 6 hivi kabla yangu, Ye alichimba kwake na aliishia Mita 60 akawa anapata maji safi tu muda wote na hayakatiki.

Mimi kuja kuchimba changu sikufanya survey bali nilimwambia mchimbaji achimbe tu hizo hizo 60 kama za jamaa tuone, na tukapata maji kweli masafi na mengi tu tukaamua kuishia hapo na kuchimbia/kudumbukiza Bomba za Plastic (PVC).

Sasa shida imekuja, kumaliza wiki tu maji yamekata hakuna maji tena. Nimewaza nizichomoe zile Bomba ili niendelee kuchimba zaidi pengine mpaka mita 80 au hata 100. Wale walionichimbia mwanzo wamenishauri niingie tu Gharama kuchimba upya kingine kirefu zaidi kwani haiwezekani tena kuchomoa zile Bomba.

Sasa hapa naomba ushauri tu kwa wazoefu wa haya mambo, je ni kweli haiwezekani kuchomoa bomba? Au Altenatively naweza kufanya nini hapa? Karibuni
Huwezi toa casing hizo maana huwa wanazifanyia cementing nadhani, pia usifanye vitu vya gharama kubwa bila research mfano unanunua gari ya milion 700 huweki bima.
 
Walichimbia stiki za Mita 2 nilizihesabu 30, wakati wanachimbia nilikua Kibiti Mjini lakini niliporudi shamba nilihesabu pipes zilizobaki. Sawa ntazipima nikienda, ntatafuta tape measure ndefu.

By the way hata nikigundua haikufika 60 sijui kama itasaidia. Manake haya mambo bana mnalipana tu na kazi inafanyika, hakuna any binded written contract.
Kweli mkuu ushauri wangu jipange uchimbe kingine chimba hata 80 au 100 na kama unataka kwaajil ya kumwagilia yani maji mengi ueke PVC ya inch 5 au 6 utapa maji mengi sana
 
mkuu hili liliwahi nitokea kama wewe yaani exactly kama wewe. na kuanzia hapo nilijifunza kitu kaka. Fanya survey kisha chimba kingine na weka cassing upya. Mind you hapo unapokomaa yawezekana hakuna maji kabisaa. so utajiongezea gharama zisizo na tija. wewe hapo cha kufanya ni kuanza upya, pia usiogope gharama hutokuja kufanya jambo zuri na la kudumu. watafte PDPR Njombe Hawa wanafanya kazi vizuri mnoo (Japo wanaringa balaa) ila mnaweza kuongea na wakakufanyia hata kwa mkopo wa miez 4 usio na riba kama utaweza lipa 50% ya gharama nzima
 
zingatia ushauri huu mkuu...
 
Hapa Pia Mkuu nawania kuokoa kuchimba mita zingine 80 mpya, so Bomba zikitoka zote hata kama zitatoka zimepasuka mradi kwenye kuchimba nitachimba mita 20 au 30 tu kama nikiendeleza shimo lile lile
Nakushauri ufanye Survey kuepuka hasara zaidi! Maji chini ya ardhi hayafuati kila mara mkondo wa moja kwa moja, inawezekana ulichimba hapo kwa kuwa jirani alipata maji lakini ukumbuke mkondo wa maji waweza kupotea hata kama visima vyako vingepangana ndani ya mita moja.
Kuhusu hizo PVC sidhani kama utafanikiwa kwa sababu yawezekana kisima kimeshafanyiwa casing kwa kutumia gravel materials(changarawe za kuchuja maji) hivyo inaweza kuwa vigumu kuzitoa.
Lakini pia, waweza muuliza driller wako kama ataweza kuondoa PVC hizo na kuchimba hapo hapo japo anaweza akakubali kibiashara zaidi maana kama hajafanya Survey hatahusika na kukosa kwako maji.
 
Dah,
So sad,
Naona hakuna alienipa uwezekano wa kuzichomoa hizo PVC pipes na kuendelea hapo hapo nikaongeaza mita 20 labda,
Means natakiwa nimuite mtu aanze moja kuchimba upya hizo mita 80+ (baada ya Survey),
Enzi hizi za Vyuma itabidi nisubiri longer tu
 
kama bado hujafanikiwa useme nifuatilie mawasiliano nikutumie, hata mimi nilikutana na changamoto hiyo kwa kisima nilichochimba cha mita 100. Nilikutana na options mbili; ya kwanza ilikuwa ni kuchomoa hizo PVC pipes ili kuanza upya kazi lkn ya pili ilikuwa ni kwamba PDPR Njombe alisema anaweza kuongezea urefu palepale kilipochimbwa hicho kama tu survey ikidhihilisha upatikanaji wa maji hapo hapo chini zaidi, kwa kuingiza PVC pipes zenye kipenyo kidogo kwenye kina kinachoongezeka kwa gharama inayokadriwa kuwa milioni mbili kasoro kama ukiongeza mita 20; sasa niko najipanga ili nione nini nitaweza kufanya.
 
Mkuu hao PDPR ni matapeli mnoo mnoo mnooo.......

Hawa jamaa usanii mwingi sana...

Wanaweza kwambia tuko Arusha tunachimba ukiwaambia sehemu gani nije wanakwambia Ngara...ukisema unaenda kesho yake utaskia anakwambia yuko Kigoma
 
mzeee kuna mahali uliwasifia PDPR kuwa wanafanya kazi vizuri japo ulikiri wanaringa balaa, lkn mbona hapa umesema ni matapeli?

Hawakamilishi kazi na wana ujanja ujanja fulani hivi nilikuja kugunda walinipiga kisima kimoja Morogoro.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom