Njoo uchimbiwe kisima

Jul 2, 2016
26
16
Habari wana jf,sisi tunajishughulisha na uchimbaji wa visima vya maji ( water well and borehole drilling) kwa gharama nafuu sana.Bei zet ni...1: 40000 tshs kwa mita moja...bei hii ni kwa wakazi wa Dar es salaam..2: 60000 tshs kwa mita moja...bei hii ni kwa wateja wa mikoani.3: Ground water survey...hii bei yake ni shillingi 350000 laki tatu na nusu tu.Vifaa vitakavyo hitajika na bei zake...1: water pampu...sisi tunapenda kutumia Doyin na bei yake inategemeana na uwezo wa pampu kuna 0.5hp 250000tsh, 1 hp 340000 tsh,1.5 hp 380000 tsh hadi 400000 tshs n.k.2: polypipe...hii inauzwa kwa mita moja ambayo bei yake ni shillingi 1500 tsh hadi 2000 tsh kwa mita moja na roler zima linauzwa 170000 hadi 190000 tshs. 3: wire...pampu yenyewe inakuja na wire wake ambao ni mita 27...na dukani wanauza waya kwa mita moja ambayo ni shillingi 2500 kwa mita moja.4: kamba ya manila... Hili unauziwa roler zima ambalo ni shillingi 40000. 5: pvc...hizi zipo za aina mbili,moja ni pvc screen na pvc plane na bei zake zinatofautiana pia. Pvc screen za inchi 4.5 zinauzwa 38000 na pvc plane zinauzwa 36000. 6: Graves...hizi ni vijikokoto flani hivi vinatumika kuweka kwenye kisima ukishaweka pvc hizi unaweka kwa pembeni ya hizo bomba.7: connecters... Hizi kuna male connecter zinauzwa 2500 tshs,elbow connectet 2500 tsh na redusing bush inauzwa 5000 tsh.8: mfuniko...hapa kuna mfuniko mdogo unauzwa 30000 tsh na mkubwa unauzwa 50000 tshs. 9: maji ya kuchimbia... Haya yanauzwa kuanzia lita 1000 ambayo bei yake ina range 10000- 15000 tsh inategemea na eneo.Hivyo ndiyo vitu vinavyohitajika kwenye uchimbaji wa kisima. Kuna baadhi ya vitu sijaviandika kwa sababu ni vitu ambavyo vinanunuliwa na mchimbaji kisima na sio mteja. Nb: bei iliyoandikwa hapo juu ni kuchimba tu vitu vyote atanunua mteja mwenyewe.Na vitu atakavyonunua mteja ndio hivyo nilivyo viorodhesha hapo juu. Angalizo...bei hiyo ni kwa maeneo pia yaliyokuwa na miamba laini na sio migumu ina maana hapo tutatumia kuchimba kwa Mfumo wa Mud rotary na sio Hummer...Hummer ina bei zake. Kwa mahitaji ya huduma unaweza kunipigiya simu kupitia namba 0655541948...
 
Nahitaji huduma yenu ila bado sijapata shamba kwa ajili ya kilimo pindi nikipata basi tutaonana.
 
Mkuu wachimbakisima nimeona umeweja ghalama ya groundwater survey 350,000 ....swali langu je survey hiyo itatoa mkadilio wa umbali wa Maji kupatikana?

Swali lingine .... Mnahuduma ya endapo mteja kupata Maji ya chumvi akaitaji Maji baridi mnamsaidiaje ili apate anachokiitaji?
 
kwa nn survey nilipie 350000 NA bdo vifaa ninunue mm??
Survey ni kitu kingine kinajitegemea mkuu...survey ni kwa ajili ya kujua maji yapo umbali gani na je kama kuna mwamba mgumu au ni laini. Survey sio lazima ufanye kwetu sisi unaweza ukafanya kwa watu wengine then sisi tukatumia report yao then tukakuchimbia kisima chako.
 
Mkuu wachimbakisima nimeona umeweja ghalama ya groundwater survey 350,000 ....swali langu je survey hiyo itatoa mkadilio wa umbali wa Maji kupatikana?

Swali lingine .... Mnahuduma ya endapo mteja kupata Maji ya chumvi akaitaji Maji baridi mnamsaidiaje ili apate anachokiitaji?
Yap kazi ya ground water survey ni kutupa uhakika kuwa maji yapo umbali gani na pia kutupa ufahamu juu ya nature ardhi ya eneo husika kama lina miamba migumu au laa..

Kuhusu inshu ya maji ya chumvi, kiukweli sisi hatuna huduma hiyo ila kama mteja akihitaji tunaweza tuka mdirect kwa wataalamu
 
Mnasema ofisi zenu zipo Morogoro, inakuaje bei ya kuchimbia kisima Dar ni nafuu kuliko hapo kwenye Moro ambako ndiko ofisi zenu zilipo? Nipo DUMILA nahitaji huduma yenu ngoja nijipange
 
Mimi niko Dar nilipima na chuo cha maji pale Mlimani. Location ni Kimara temboni, maji 150 meters. Vipi mkitumia vipimo hivi mkakuta maji yako zaidi au pungufu ya mita 150? Na je naweza chimba tu nikaendelea kujipanga kwa pampu na vitu vingine au lazima niwe na hizo zagazaga zote Mwanzoni?
 
Bei haitokani na umbali bali ni ground formation yaani tabaka la ardhi. Dar es salaam ina ardhi laini (soft formation) wakati morogoro na mikoa mingine isipokuwa mkoa wa pwani ina ardhi ngumu (Basements). Tatizo ni jiolojia ya sehemu na sio umbali.
 
Ahsante kwa maelezo mazuri
 
Maji unaweza kukuta yapi kwa juu kidogo ila its better kama ukichimba mita hizo mkuu na pia unaweza ukachimba leo ukatia pvc kabsa then ukajipanga ukaja kuweka pampu later on
 
Bei haitokani na umbali bali ni ground formation yaani tabaka la ardhi. Dar es salaam ina ardhi laini (soft formation) wakati morogoro na mikoa mingine isipokuwa mkoa wa pwani ina ardhi ngumu (Basements). Tatizo ni jiolojia ya sehemu na sio umbali.
Umenisaidia kunijibia vyema kabisa
 
Mkuu eneo la tukio ni Serengeti, naomba kufahamu gharama za kuchimba kisima (soft rock) hilo eneo ni la chemichemi, it means maji yako Karibu. Nijulishe gharama zote mpka nianze kuchota maji
Habari wana jf,sisi tunajishughulisha na uchimbaji wa visima vya maji ( water well and borehole drilling) kwa gharama nafuu sana.Bei zet ni...1: 40000 tshs kwa mita moja...bei hii ni kwa wakazi wa Dar es salaam..2: 60000 tshs kwa mita moja...bei hii ni kwa wateja wa mikoani.3: Ground water survey...hii bei yake ni shillingi 350000 laki tatu na nusu tu.Vifaa vitakavyo hitajika na bei zake...1: water pampu...sisi tunapenda kutumia Doyin na bei yake inategemeana na uwezo wa pampu kuna 0.5hp 250000tsh, 1 hp 340000 tsh,1.5 hp 380000 tsh hadi 400000 tshs n.k.2: polypipe...hii inauzwa kwa mita moja ambayo bei yake ni shillingi 1500 tsh hadi 2000 tsh kwa mita moja na roler zima linauzwa 170000 hadi 190000 tshs. 3: wire...pampu yenyewe inakuja na wire wake ambao ni mita 27...na dukani wanauza waya kwa mita moja ambayo ni shillingi 2500 kwa mita moja.4: kamba ya manila... Hili unauziwa roler zima ambalo ni shillingi 40000. 5: pvc...hizi zipo za aina mbili,moja ni pvc screen na pvc plane na bei zake zinatofautiana pia. Pvc screen za inchi 4.5 zinauzwa 38000 na pvc plane zinauzwa 36000. 6: Graves...hizi ni vijikokoto flani hivi vinatumika kuweka kwenye kisima ukishaweka pvc hizi unaweka kwa pembeni ya hizo bomba.7: connecters... Hizi kuna male connecter zinauzwa 2500 tshs,elbow connectet 2500 tsh na redusing bush inauzwa 5000 tsh.8: mfuniko...hapa kuna mfuniko mdogo unauzwa 30000 tsh na mkubwa unauzwa 50000 tshs. 9: maji ya kuchimbia... Haya yanauzwa kuanzia lita 1000 ambayo bei yake ina range 10000- 15000 tsh inategemea na eneo.Hivyo ndiyo vitu vinavyohitajika kwenye uchimbaji wa kisima. Kuna baadhi ya vitu sijaviandika kwa sababu ni vitu ambavyo vinanunuliwa na mchimbaji kisima na sio mteja. Nb: bei iliyoandikwa hapo juu ni kuchimba tu vitu vyote atanunua mteja mwenyewe.Na vitu atakavyonunua mteja ndio hivyo nilivyo viorodhesha hapo juu. Angalizo...bei hiyo ni kwa maeneo pia yaliyokuwa na miamba laini na sio migumu ina maana hapo tutatumia kuchimba kwa Mfumo wa Mud rotary na sio Hummer...Hummer ina bei zake. Kwa mahitaji ya huduma unaweza kunipigiya simu kupitia namba 0655541948...
 
Mkuu eneo la tukio ni Serengeti, naomba kufahamu gharama za kuchimba kisima (soft rock) hilo eneo ni la chemichemi, it means maji yako Karibu. Nijulishe gharama zote mpka nianze kuchota maji
Hapo kwa mita tunachimba laki moja kila kitu kinakuwa juu yetu isipokuwa maji ya kuchimbia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom