Ninaweza kukusafirishia mzigo hadi hapa DSM. Iwapo utakubaliana na vipengele tajwa hapa chini.
1. Ghalama zote za kusafirishia utalipia pindi mzigo wako umefika Dar es Salaam
Ghalama zitatokana na uzito wa mzigo, Hivyo ni vyema ukatambua kabisa uzito wake ili nikupe hesabu ya ghalama ya kusafirishia kabla ya mzigo haujaletwa ofisini DUBAI
Hakuna malipo yoyote ya awali unayotakiwa kulipia/ kunilipa.
Utapewa Tracking number ya mzigo - Hivyo utaweza kuufuatilia vyema hatua kwa hatua hadi mzigo unafika nchini.
2. Hapa nchini: -Iwapo kutakuwa na charges Airport { Mfano (a) Swisport charges - tsh 27,000 (b) Clearance and Handling charges - TSH 60,000) } - Utawajibika kulipia.
3. Uwe tayari kulipia KODI kutokana na thamani ya mzigo - Iwapo Mamlaka ya mapato / TRA itakutaka kulipia kodi mzigo wako.
Kiwango utakacholipia kitatokana na assessment ya mzigo itakayofanya na mamlaka husika Airport.
JE NINI UNATAKIWA KUFANYA?
- Kuufikisha mzigo ofisini DUBAI - Al Quoz Industrial Area 1 Street No. 11.
- Anwani kamili nitakupa PM au kwanjia ya whatsapp iwapo utahitaji hii huduma toka kwangu
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.