Msaada kujaza fomu ya passport online

Emery Paper

JF-Expert Member
Jun 1, 2019
1,429
2,713
Habari zenu wakuu ?

Niko hapa najaza fomu ya kuomba Passport online. Nimefika hii hatua natakiwa nijaze dhumuni la safari na maelekezo yanasema ni lazima kujaza. Sina safari yoyote bali nahitaji tu kuwa na passport. Kwa wenye uzoefu natokaje hii hatua ?
Nashukuruni sana kwa msaada wenu.

MSAADA.png
 
View attachment 2914802
kama wewe ni mwanafunzi andika unaenda kusoma, kama husomi andika biashara halafu rudi hapa upate maelekezo.
 
Ni lazima uwe na safari ndio ufuatilie passport. Ila kama unaitaka na hauna safari unaweza kuipata kwa ujanja ujanja. Tofauti na ujanja ujanja ni lazima uwe na safari.
 
Yaani huna lengo la kusafiri halafu unataka uwe na pasi ya kusafiria!!?
 
Ni lazima uwe na safari ndio ufuatilie passport. Ila kama unaitaka na hauna safari unaweza kuipata kwa ujanja ujanja. Tofauti na ujanja ujanja ni lazima uwe na safari.
Nashukuru kwa msaada wako mkuu.
 
Fomu zilivyotengenezwa ni lazima ujaze sababu ya safari yako kwenye mfumo. Aliyetengeneza mfumo alitakiwa kuweka options zaidi ya mwanafunzi, mfanyabiashara au mtumishi wa Serikali... Mfano mtanzania anawaza kwenda nje ya nchi kutalii pia.

Hapo kwenye sababu ya safari jaza Biashara, fomu ikishakamilika na kupokelewa bado kuna hatua ya mahojiano ya ana kwa ana, hapo ndipo unapothibitisha kuwa una uwezo wa kifedha si kumiliki passport tu bali unaweza kumudu gharama zote za safari kama itatokea.

Lakini, kuna sababu gani ya kumiliki passport kama huna mpango wa kusafiri? Kama mpango upo basi anza na nchi zinazotuzunguka ....itakuwa rahisi zaidi.

Kila lenye kheri kwako!.
 
Passport sio pambo kama huna safari subiri ukipata safari ndio ufuatilie mbona ni siku 3 tu za kazi.
 
Fomu zilivyotengenezwa ni lazima ujaze sababu ya safari yako kwenye mfumo. Aliyetengeneza mfumo alitakiwa kuweka options zaidi ya mwanafunzi, mfanyabiashara au mtumishi wa Serikali... Mfano mtanzania anawaza kwenda nje ya nchi kutalii pia.

Hapo kwenye sababu ya safari jaza Biashara, fomu ikishakamilika na kupokelewa bado kuna hatua ya mahojiano ya ana kwa ana, hapo ndipo unapothibitisha kuwa una uwezo wa kifedha si kumiliki passport tu bali unaweza kumudu gharama zote za safari kama itatokea.

Lakini, kuna sababu gani ya kumiliki passport kama huna mpango wa kusafiri? Kama mpango upo basi anza na nchi zinazotuzunguka ....itakuwa rahisi zaidi.

Kila lenye kheri kwako!.
Ni kweli kuna sehemu wameminya baadho ya options.

Tupo kwenye maisha ya utafutaji kuna nyakati unajikuta baadhi ya fursa zinakupita kisa huna passport.
 
Habari zenu wakuu ?

Niko hapa najaza fomu ya kuomba Passport online. Nimefika hii hatua natakiwa nijaze dhumuni la safari na maelekezo yanasema ni lazima kujaza. Sina safari yoyote bali nahitaji tu kuwa na passport. Kwa wenye uzoefu natokaje hii hatua ?
Nashukuruni sana kwa msaada wenu.

View attachment 2914802
Andika tuu matembezi halafu kwenye nchi utachagua za afrika mashariki mfano Kenya
 
Back
Top Bottom