Baada ya kujaza fomu ya maombi ya namba ya NIDA unatakiwa ukae muda gani ili kupata namba yako?

vert boy

Member
Nov 29, 2023
18
23
Habarini wana Jamii,

Baada ya kujaza fomu ya maombi ya namba ya NIDA unatakiwa ukae mda gani ili kupata namba yako?

Nina mwezi wa tatu tangu nijaze taarifa za kuomba namba ya NIDA lakini mpaka sahivi sijafanikiwa kuipata.

Nikienda ofisi husika za NIDA naambiwa mtandao upo chini Tanzania nzima kwa hyo nikaangalie kwa njia ya simu (NIDA ONLINE)

Nikija kufungua online naambiwa nihakiki taarifa zangu. Nilitakiwa nika-report chuo mwaka huu lakini nimeshindwa kwa sababu ya kukosa namba ya NIDA.

Mamlaka husika naomba hili liangaliwe. Naomba kuwasilisha from SANYA JUU (SIHA) KILIMANJARO.
 
Mimi niliipata baada ya mwaka na nusu pale moshi mjini kila nikienda walikua wanajibu mtandao mara system.
 
NIDA huwa wanazingua sana. Utaratibu wao haueleweki

Unaweza kupata namba ila kupata kadi ukasubiri zaidi ya mwaka au miaka miwili

Sasa sijui huko maofisini huwa wanafanya nini na ukienda unakuta wamerelax tu kupiga stori na kwenda breakfast na lunch, hasa katika ngazi za Halmashauri
 
Back
Top Bottom