Msaada kuhusu tangazo la simu feki kufungiwa.

Msaada kuhusu tangazo la simu feki kufungiwa.

Chabo

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2011
Posts
1,098
Reaction score
1,176
Habari wana jamvi..
Leo Mamlaka ya mawasiliano (TCRA)imetangaza kuzima au kutoziwezesha simu ambazo hazina ubora kufanya kazi hapa tanzania,na zoezi hilo litaanza baada ya miezi sita kuanzia leo..swali langu ni je?hizi tecno zetu zitasalimika?
 
Fake ni simu bandia, hizo tecno ni kampuni inayojulikana? Zikifingiwa tecno % kubwa ya waTz no kua na simu
 
Hahahaha acha woga mkuu, kuna simu zinajulikana zipo kibao kkoo
 
Fake ni simu bandia, hizo tecno ni kampuni inayojulikana? Zikifingiwa tecno % kubwa ya waTz no kua na simu
Ni kweli mkuu...ukitaka kujua ni wangapi wataathirika kwenye huu mpango fanya reseach kwenye daladala uone ni wangapi wanatumia tecno.
 
Nafurahi kuwa nimerudishiwa majibu kuwa TECNO S5 yangu ni original from Tecno coperation....
 
Huawei yangu inatambulika Beijing kumbe! Xie xie!
 
Techno ni simu halisi!
Ishu ni hizi feki, iwe inaitwa iphone, samsung ama lg!
 
Hiyo inaenda sambamba na kufunga simu zote zilizoripotiwa zimepotea/ibiwa zitafungwa na zisiweze kutumika na mtandao wowote ule. Chakufanya nenda na RB pamoja na risiti yako ya kununulia simu na yenye kuonesha warranty ya mwaka 1 na imei namba.peleka kwenye kituo cha mtandao wako wa simu watakusaidia hata Leo.
 
Tuma imei yako kwenda 15090 utaletewa taarifa kama itaendana na simu yako basi iko poa .

Hajjmakwato

Mkuu kama simu yangu mimi Ni Samsung Galaxy na IMEI yake ni abcdefghjk kwa mfano. Nikituma hizo IMEI tajwa hapo juu kwenda 15090,jibu litakua irudishwe IMEI namba kama niliyowatumia au nitapewa Jina la Simu? Kitu fake nitajibiwa jibu gani? Watasema Simu yako ni fake,au IMEI itasema ni Uongo au Jina sitaletewa?! Ufafanuzi please simu fake ni jibu lipi specifically?!
 
Jina la kampunj - Brand ya simu (Model namba) - Kama IMEI haioani na simu yako wasiliana na muuzaji. Usipoweza,ibadilishe kabla ya Juni 2016 kwani yaweza kuwa BANDIA
 
Swali la kizushi:

Simu nyingi fake ni zile zinatumia Os ya Android, na kwakuwa inawezekana kubadili imei kwenye Android

Je nikibadili imei ya samsung fake na kuweka imei ya simu original itakuaje?
 
Back
Top Bottom