Msaada kuhusu simu ya Samsung

Jerry95

New Member
Dec 14, 2020
4
3
Miezi mitano iliyopita nilinunua simu aina ya Samsung S9 plus kumbe hii simu ni refurbished ina tatizo la network ukiweka laini karibia zote muda mwingine inaandika emergence mara mtandao unasoma.

Afadhali kidogo laini ya halotel ndo ina kubal ila sometime nayo mtu akikupigia naambiwa sipatikani, nikarudishadukani nikapewa nyingine nayo hivo hivo hadi leo natumia hii simu ila mtandao haupo vizur kabisa, hii simu nakubali nimepigwa,nimepoteza lak 9 na 50 hata miezi sita bado ina nikosesha mambo mengi sana muda mwingi naambiwa sipatikani.

Naomba msaada kama kuna mtu anatumia au alishawahi kutumia SAMSUNG M51 anipe feedback iko poa au nayo inazingua, maana nishapoteza pesa nyingi kwa hiyo naogopa sana, kama kuna mtu anatumia au rafiki yake anatumia au ulishawahi kutumia nisaidieni.
 
Kama uliweza kulipa laki tisa na nusu basi kipato chako ni kikubwa. Chukua laki 5 au milioni na kitu kanunue simu nyingine. Usisahau kuwa makini. Mada nyingi tu zipo humu zikionyesha jinsi ya kudetect simu feki na simu halisi.

Mimi binafsi nikicheki IMEI # tu napata jibu kuwa ninataka luingizwa mjini au la.
 
Kama uliweza kulipa laki tisa na nusu basi kipato chako ni kikubwa.
Chukua laki 5 au milioni na kitu kanunue simu nyingine. Usisahau kuwa makini. Mada nyingi tu zipo humu zikionyesha jinsi ya kudetect simu feki na simu halisi.
Duh! Punguza ukali wa maneno aisee utammaliza jamaa kwa presha wakati kuomba msaada
 
Kazi ya kulima kipande cha shamba kwa jembe la mkono ni rahisi kuliko kazi ya kutafuta simu original kwenye maduka ya Tanzania!
 
Andika Imei Number Kwenye Sehemu Ya Ujumbe
Halafu Tuma Kwenda Number 15090.
Ni Bure Utapatiwa Majibu Muda Huo Huo
 
Tatizo si model mkuu, Tatizo ni namna unavyonunua hizo simu.

M51 ni simu nzuri sana.

Jijengee mazingira kununua vitu vipya kwa kampuni yenyewe ama mawakala ambao wanatambulika
 
Back
Top Bottom