Msaada kuhusu Salary Loan

kluger

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2016
Messages
1,988
Points
2,000

kluger

JF-Expert Member
Joined Jun 16, 2016
1,988 2,000
Wakuu salama,

Nilikuwa na ajira ya kudumu serikalini, nikakopeshwa mkopo mkubwa na bank ya biashara Kama salary loan.
Ikiwa makato yote yanafanyika kila mwezi kutoka Kwnye Kwnye mshahara wangu.

Nikapata safari ya masomo nje ya nchi, mwajiri hakukubaliana na mimi kunipa ruhusa japo mwanzo niliambiwa haina shida nitapata ruhusu, hivyo niliacha maombi yangu ya ruhusa na kuanza safari.

Nikiwa safarini nje ya nchi, mwajiri kakataa ruhusa na kufuta ajira yangu.

Bank wanakuja juu ni muda sasa hawapati makato yao, moja ya makubaliano ilikuwa kuchukua mafao yangu kufidia mkopo, lakini sasa wanatishia kutangaza magazetini na kuchukua hatua zaidi.

Hakuna sehemu nimepinga kulipa, lakini pia nimewaomba muda ili niendelee kulipa kila mwezi nikiwa nje ya nchi, wakaniambia wananipa siku 14 tu nitafute kila jinsi kulipa, siku hizo zimeisha jana na hakuna jinsi nimeweza kutuma makato yaliyochelewa, nimewajulisha hali hiyo pia.

Je kuna namna gani hapa kitaalamu/ kisheria naweza weka suala hili vizuri, maana vitisho vinazidi na nia yangu ya kulipa deni ni njema.

Msaada wadau katika hili, wale vijana washule na ambao bado hamjawa na uzoefu wa mambo haya, tupisheni kidogo tujifunze kwa wazoefu wa mambo haya.

Ahsante sana, nawakilisha.
 

BEHOLD

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2013
Messages
4,932
Points
2,000

BEHOLD

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2013
4,932 2,000
Hakuna sheria ya kukwepa deni.

Rejea terms za makubaliano yenu uone cha kufanya ikibidi uwaombe kufanya re-scheduling ya marejesho japo hiyo inaweza kuongeza riba pia.
 

Forum statistics

Threads 1,344,038
Members 515,307
Posts 32,805,607
Top