Karibu sana mkuu!
Embu cheki hii thread hapa, itakusaidia:
https://www.jamiiforums.com/matangazo...uki-swift.html
Tatizo la Nissan March na Vitz ni spea. Ni gari nzuri lakini spea zake zipo juu. Unaponunua gari, kama ungependa kupata unafuu wa matengenezo, tafuta gari ambayo vifaa vyake vinaingiliana na magari mengine mengi, au hizo gari zipo nyingi hapa mjini. Vinginevyo, spea zinakua ngumu kupata na bei inakua juu.
Kwa mfano, Fan ya Vitz ni Tsh 250,000 na ya Corolla unaipata kwa Tsh 35,000. Hope unaona mwenyewe gharama ya matengenezo inavyopanda ghafla.
Tatizo la Toyota Duet ni piston 3. Gari za piston tatu zinasumbua. Na gari chache sana za Toyota zina 3 pistons engine. Hii inamaanisha spea ni chache, na ukiipata bei ipo hewani.
Ila uchaguzi wa gari unategemea na kipato pia, na maisha ya mtu binafsi. Sio kila mtu anawasiwasi na spea au ulaji wa mafuta. Wengine they are much more after lifestyle and fashion - money is not a problem.
Labda uniambie, ungetegemea kununua gari la kiasi gani, na ungependa matumizi kwa siku (kwa mizunguko ya hapa na pale, kwenda ofisini na kurudi) iwe kiasi gani. Then tuangalie options nzuri kwako.
Karibu sana mkuu!