Msaada kuhusu mabati aina ya Kiboko

Dodoma moja

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
307
177
Wakuu habari zenu na poleni na harakati za kupambana na maisha,

Naombeni msaada wenu kwa wale wazoefu katika sekta ya ujenzi kuhusu mabati ya Kiboko. Jana nimeenda kwa wakala nimekuta yanauzwa 27,000 bati moja la msouth 30G na Alaf wanauza 37,000pc 30G difference ya Tshs. 10,000 nikahoji kuhusu ubora wa chapa kiboko muuzaji akaniambia ni mazuri sana na hayapauki na watu wengi sana wamenunua kutoka maeneo mbalimbali na hawajawahi kurudi kwake kulalamika kuhusu kupauka.

Naombeni ushauri wenu tutani nisije kuingia chaka nikatamani kung'oa paa huko mbeleni.
 
Ni mazuri sana, mm nina miaka 2 hayajawahi Pauka, hivi upo Dodoma? Nataka kujua wakala Mkuu wa kiboko hapo Dodoma yupo mitaa gani?
 
Bati ni ALAF hakuna mwengine atakayemkamata kwenye ubora.

Tsh 10,000/= ni tofauti ndogo sana ikufanye ufanye kitu cha kujilaumu maisha yako yote ukiweka hizo unazopewa sifa mtaani zikapauka baada ya miaka mitano utakuja kunielewa nilichoandika hapa
 
Asante kwa ushauri
 
Wakuu habari zenu na poleni na harakati za kupambana na maisha,

Naombeni msaada wenu kwa wale wazoefu katika sekta ya ujenzi kuhusu mabati ya Kiboko. Jana nimeenda kwa wakala nimekuta yanauzwa 27,000 bati moja la msouth 30G na Alaf wanauza 37,000pc 30G difference ya Tshs. 10,000 nikahoji kuhusu ubora wa chapa kiboko muuzaji akaniambia ni mazuri sana na hayapauki na watu wengi sana wamenunua kutoka maeneo mbalimbali na hawajawahi kurudi kwake kulalamika kuhusu kupauka.

Naombeni ushauri wenu tutani nisije kuingia chaka nikatamani kung'oa paa huko mbeleni.
Nilipaua na kiboko mwaka 2019.

Hadi leo liko vile vile halijapauka hata kidogo.
 
Kwanini 12 sio 11
Ni kwa sababu kama fundi alikupa tathmini ya bati 120 hii hesabu inakuwa ni kwa bati za migongo 12. Lakini kuichukua za migongo 11 katika kila bati 12 utakuwa na upungufu wa bati 1.....hivyo kwenye bati 120 utakula loss ya bati 11.....

Kwa nini inakuwa hivi..... Inakuwa hivi kwa sababu kwenye maungio ya kila bati kwa kila upande yanaumana kwa migongo miwili na kati kubaki migongo 8....bati lenye migongo 11 litabakiwa na migongo 7....hivyo kusababisha upungufu wa bati....

Nimejitahidi kueleza nadhani kwa namna fulani hivi utakuwa umenielewa.... Asante
 
Back
Top Bottom