Msaada kuhusu kumwekea mtu dhamana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada kuhusu kumwekea mtu dhamana

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Sabung'ori, Mar 21, 2012.

 1. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  Heshima kwenu waungwana.
  Naomba msaada wenu wataalam wa sheria...mwaka jana nilimwekea kaka yangu dhamana ktk kesi ya madai inayomkabili iliyofunguliwa ktk mahakama ya mwanzo hapa Ilemela Mwanza...kabla ya kesi haijaanza kusikilizwa,kaka yangu akaona ni bora atafute mwanasheria atakayemsaidia ktk kesi hiyo...akapata wakili ambaye alimwandikia barua hakimu wa mahakama ya mwanzo akimwalifu kuwa mtejawake(ambaye ni kaka yangu) amempa kazi ya kuisimamia kesi yake...kaka yangu aliipeka barua hiyo hapo mahakani na kuikabidhi kwa karani wa mahakama,siku iliyofuata ilikuwa ni siku ya kusikilizwa hiyo kesi,hakimu baada ya kutaja kesi hii alimtaarifu mshataki kuwa kaka yangu ameweka wakili wa kiisimamia kesi yake,kwahiyo kutokana na utaratibu wa mahakama ya mwanzo kesi hiyo haitaweza kusikilizwa hapo mahakama ya mwanzo hivyo inahamishiwa mahakama ya wilaya...baada ya wiki moja wakili wa kaka yangu alienda akachukua barua mahakama ya waliya ikimwalifu kuwa ile kesi anayoisimamia sasa iko mahakama ya wilaya...
  Msaada ninaomba uko hapa...tangu kesi hii ihamishiwe mahakama ya wilaya haijawai kutajwa...jana mshataki amekuja nyumbani kwangu na kuniambia kwamba mahakama imetoa kibali nikamatwe kwani mtu niliyemwekea dhamana haonekani mahakamani...leo nilipofuatilia huko mahakama ya wilaya kesi ilipohamishiwa nikaambia hiyo kesi haijawai kufunguliwa hapo,nilipoenda mahakama ya mwanzo kujua kulikoni,nimekuta jarada la hiyo kesi bado liko hapo mahakama ya mwanzo na kesi inaendelea kusikilizwa...
  Je ndugu zangu wataalam wa sheria hivi ndo inatakiwa iwe?,Je nifanyeje sasa nisionekane nimeidharau mahakama?...je ni kweli kesi inaweza kuhamishwa kutoka mahakama ya mwanzo kwenda ya wilaya na bado ikaendelea kusikilizwa tena mahakama ya mwanzo?...
  Ninataraji ntakuwa nimeeleweka,naomba msaada wenu...
   
Loading...