Msaada kuhusiana na transfer window

Msaada kuhusiana na transfer window

Gonzalo Miguel

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2018
Posts
850
Reaction score
661
Habari za asubuhi Wakuu!

Niende moja kwa moja kwenye mada.

Mimi ni mhitimu wa kidato cha sita 2019 katika masomo ya Arts, Ivumwe High School mjini Mbeya. Shule ni ya umoja wa wazazi. (private school) japo ada kwa kiasi fulani inaeza lipwa na mtu wa hali ya chini.

Baada ya matokeo kutoka vizuri nili apply vyuo viwili cha kwanza ni IRDP Mipango Dodoma Bachelor of Urban Development and Environment Management na chuo cha mwisho kilikuwa UDSM Bachelor of Arts with Education in Chinese and English studies, na vyote nilichaguliwa kama nilivyoomba.

Baada ya kutuliza kichwa nika amua ku-confirm Mipango kwa moyo wangu wote mkunjufu. Wazo la kuhama chuo limeanza baada ya kukosa mkopo awamu zote mbili. Wazee wameshauriana kwamba niende hivyo hivyo, watajipinda kunisomesha. Dodoma sina ndugu wala mtu tunae mjua, gharama itakuwa kubwa mjini Dodoma (chumba, chakula, mahitaji ya shule sababu kozi yenyewe inamahitaji mengi).

Nataka niombe uhamisho toka Mipango kwenda UDSM Dar ambako nina uncle wangu anaishi uko pia ndugu wengi wapo huko ambapo mimi na wazee tumeona gharama ztapungua kwa kiasi fulani.

Swali ni kwamba: IRDP Mipango usajili unaanza tarehe 4 - 15 November na ratiba ya TCU transfer window linafunguliwa tarehe 5 - 15 November, kukusanya maombi ya transfer ni 16 - 30 November na majibu ya uhamisho yatatoka tarehe 7 December.

1. Je, usajili nitafanya kabisa katika Chuo cha Mipango huku nikiwa nishaomba uhamisho?

2. Ada ntakayolipa Mipango nayo itakuwa transferred katika chuo husika nilichoomba? (Sababu huwezi fanya usajili bila kulipa ada chuoni Mipango)

3. Na itagharimu pesa kiasi gani kufanya process za transfer?

Sababu kuu ya kuhama chuo ni kupunguza gharama za kimaisha kwa kiasi fulani. Wazee na uncle wameshauri hivyo na mimi nimekubaliana nao.

Pia natoa shukrani kwa wale wote mlionitia moyo na kunipa tumaini maana nianza kukata tamaa ya kusoma. Now nina nguvu mpya

Wakuu naomba msaada wenu tafadhali, Nimebakiza siku 6 tu kwenda chuoni na siku 7 kufunguliwa dirisha la uhamisho la TCU.
 
Mkuu pole sana ila naona nami nipo kama wewe nimefikiria sana kuhusu kuhama chuo nilichaguliwa RUCU, UDOM, UDSM ila nikaconfirm RUCU sasa nimekosa mkopo awamu zote mbili.

Nimewaza kuhama chuo maana hata pesa nusu ya ada RUCU sina nawaza kama ingekuwa UDOM ningepata unafuu nikalipa nusu pengine batches zingine za mkopo zingenikuta chuoni sasa hapa nawaza inawezekana vipi hili suala na lisiathiri kupata mkopo kwa batches zinazofuata nadhani wanaojua watusaidie.
 
Au katika uandishi wa barua za maombi ya transfer.

Wakuu hapa msaada unahitajika kumsaidia walengwa husika? Sababu zipi sana sana zinazohitajika katika mfano, hali ngumu ya kifedha kwa ajili za ada.
 
Gonzalo Miguel,

Kwanza napenda nikupongeze Gonzalo Miguel kwa kuchaguliwa kuingia chuo kikuu, hiyo ni hatua ya mafanikio na ni matumaini yangu kwamba utaitendea haki hii nafasi adhimu uliyoipata.

Naomba kujua Bodi ya mikopo walikupa sababu gani za wewe kukosa mkopo iwapo unaenda kusoma kozi ya BA Education? Ninavyojua katika kutoa mikopo wanafunzi wa Education wanapewa kipaumbele, kwanini wewe hukupewa mkopo? Je ulisoma A-Level shule ya Private?

All the best.

Ahsante
 
Mwaka huu watu watashindwa kwenda chuo wengi kwa sababu ya ada hasa hii batch ya 2 watu wamepewa asilimia ndogo.
 
Gonzalo Miguel,

Kama ulisoma Private A-Level wana-assume waliokulipia huko wana uwezo hivyo hawawezi shindwa kulipa Ada ya BA Education (Ada ya A-Level Private School kwa mwaka ni kubwa kulipo ile BA Education kwa Mwaka).

Ahsante
 
Naomba Gonzalo Miguel uniruhusu kuuliza wadau hasa wale mliosoma miaka ya hivi karibuni.

Watoto wa mashemeji zangu kutoka huko "Madongo kuinama" ambao wanaingia Dar kwa mara ya kwanza, wanaanza first year mwaka huu hapo Muhimbili na IFM na wazazi wao (uwezo mdogo & madogo hawajapata mkopo) wamewaombea kwa baba zao wadogo wanaokaa Boko (wawe wanaenda na kurudi chuoni).

Mimi na Shangazi yao tumekuwa na wasiwasi kuhusu ufanisi katika masomo yao ukizingatia hali halisi ya Dar hasa usafiri.

Je wale ambao mna watoto & jamaa wanasoma chuo toka nyumbani (Dar es salaam) maendeleo yao ya kimasomo yapo vipi? Hivi kiuhalisia ukifanya Cost Analysis ya mwanafunzi toka familia yenye uwezo wa kati & chini kukaa hostel za chuo & nyumba za kupanga karibu na chuo au kukaa kwa jamaa zao mbali. Option ipi ambayo ni bora zaidi.

Ahsante

CC
Dig the EA , Bsc.ANEB , SpiderThy ,mosabiy ,Kamwene kamwene ,kat.ph
 
Hongera sana kwa kuchaguliwa ,lakini pole sana kwa kukosa mkopo.

1. Katika changamoto zako sijui huko IRDP hawana hostels hadi uone changamoto kwako kusoma hapo? Kama wanazo inakuaje iwe changamoto kwako?

2. Kwa uzoefu wangu mdogo kwa first year ambae hata hajaanza masomo kufanya transfer wala haitajiki kuripoti Chuo alichochaguliwa, anachofanya yeye ni kuchukua Admission letter yake (Vyuo vingi wanaziweka online kwenye websites zao au kwenye account uliyotumia ku-apply) then andika barua ya kuomba kuhamia Chuo chochote unachotaka, sio lazima kile ulichochaguliwa na uiambatanishe pamoja na hiyo admission letter.

Chuo unachotaka kuhamia wakiridhika na sifa zako kulingana na program unayotaka kuhamia na nafasi zilizopo wanakuhamishia tu hapo.

Kila la kheri
 
King snr,
Admission letter ni ya lazima kuonyesha kuwa ulikuwa selected Chuo kingine, lakini utaambatanisha na copies za vyeti vyako pia.
 
Nendeni vijana ila kama hujapata mkopo sawa. Kama bajeti ipo ulipo confirm kuihamisha hapo ni ishu mpaka mwaka wa 2.
 
samahanin wadau Nilkuw nje kw mda kdgo..
Niseme asanteni kwa michango yenu,imenijenga kmoyo na kiakili
Nimeamua nisome IRDP kwa hal na mali
 
Back
Top Bottom