Msaada kubadilisha comb ya form five uliyopangiwa shule za serikali.

Grena

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2016
Posts
656
Reaction score
1,557
Habari zenu wakuu,

Wizara wametoa majina ya shule na comb za waliofaulu form five.

Mdogo wangu alipata division two, ana A ya chemistry, B ya physics, biology, Geography na C ya hesabu. Masomo mengine ya arts yaliyobaki ana B.

Aliweka machaguo ya kuchagua comb chaguo la kwanza PCB, pili PCM na tatu PGM lakini Kapangiwa HGL, Makete iwawa secondary.

Kusema ukweli imekuwa siku ya huzuni Sana kwake, amelia yani hakutegemea Hilo sababu siku zote anapenda Masomo ya science.

Msaada kwa wajuzi hivi hakuna uwezekano atakavyoreport shule aombe kubadili comb iwe ya science au option ni kwenda Private tu.

NB; nimejaribu kugoogle hii shule haina comb za science option sio kubadili comb Tena Bali kubadili shule. Sijui serikalini ukiomba ubadilishe shule waliyokupangia Kama inawezekana.
 
Jaribu kwenda ofisi za elimu kupata ufumbuzi zaidi(labda wanaweza mbadilishia)
 
Samahani mkuu ofisi za Elimu kwa ngazi gani. Wilaya, mkoa au wizaran
 
Kama katika hiyo shule sliyopangiwa zipo hizo combi anazozitaka aingie tu darasani asome atoe tu taarifa kwa academic master

Ila kama hakuna hizo PCM , PCB na PGM basi nahisi aende wizarani watampangia shule husika
 
Asante Sana mkuu. Inabidi tufanye uchunguzi Kama hizo comb zipo
 
Kama katika hiyo shule sliyopangiwa zipo hizo combi anazozitaka aingie tu darasani asome atoe tu taarifa kwa academic master

Ila kama hakuna hizo PCM , PCB na PGM basi nahisi aende wizarani watampangia shule husika
Mkuu nimejaribu kugoogle hiyo shule haina Masomo ya science. Ni arts tu HKL, HGK, HGL. Inabidi tutafute solution labda ya kwenda wizarani
 
Hii wizara ina utaratibu mbovu sana wa ku allocate combinations, hakuna umuhimu wa kujaza zile fomu za machaguo.

Mwambie aende wizarani wambadilishie kabla shule hazijafunguliwa!!!
 
Kwahiyo inabidi niende wizarani Dodoma?
 
Inawezekana ,tena uwahi kabla ya wakati wa kuripoti na uwe umechagua kabisa shule ya kwenda yenye combination anayoitaka.
 
Jitahidi ukienda huko wizarani uchagur shule nzuri hasahasa kwenye michepuo ya science. Na pia kijana awe serious. Maana ukikosea kidogo tu, kijana atamaliza six af matokeo yakiwa mabov inabidi arudi diploma so anakua kama kapoteza muda. Kila la kheri kwako na kwake
 
Shukrani kwa ushauri mkuu
 
Back
Top Bottom