MSAADA... Kuandika Kitabu.... "Record.. Book Written by Most Authors"

VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,194
1,355
Wanajamvi nataka tuvunje rekodi kwa kutunga story ambayo wanajamvi wote tutachangia...

Taanza kwa Sentensi moja, na kila mtu akitaka kuchangia anaweza akapost sentensi yake ambayo itakuwa muendelezo wa sentensi iliyopita mpaka tuone mwisho wa hii hadithi mtu anaruhisiwa kuchangia as many times as possible lakini please short and clear alafu hakikisha story inaendelea from the last sentense

Please dont post neno CRAP sababu atakayefatia itabidi aendeleze kutokea kwenye hilo neno CRAP.....

May the Story Begin......
 
Jamani maisha gani haya…., Ndio kwanza mwanzo wa mwezi na sina hata Senti…,
 
Mama mwenye nyumba nae sijamlipa miezi mitatu sasa. Ingawa ananitamani lakini siwezi kumsaliti mke wangu na watoto kijijini, ambao nao hii wiki ya pili sijawatumia pesa.... ama kweli maisha ya mjini ni kazi....
 
Nitaukabili vipi tena mwaka huu, ikiwa kipato changu hakijaongezeka na mahitaji yanazidi, watoto shuleni, mke wangu kijijini..ikiwa hivi nitaweza hata kuwaona, au nitaendelea kuwa mlowezi hapa mjini..?
 
Nilidhani hii sura yangu nzuri ni baraka kutoka kwa mungu, ila umbe ni mkosi.... kazi nne nimefukuzwa sababu ya wake za matajiri zangu kunitaka. Mimeweza kuepuka na kuwakataa wote mpaka sasa, lakini naona hii njaa uzalendo utanishinda.
 
Nifanye vipi ili niweze tuma walau chochote kwa mama na watoto kama maisha yenyewe ndiyo haya........
 
Nilimwacha mama mwenye nyumba anachinja kuku, hii njaa niliyonayo na deni la nyumba analonidai sidhani kama leo taweza kumuepuka, nina uhakika hata nikimuomba pocket money hawezi kuninyima. Ila tatizo nikiingia kwenye huu mchezo ni vigumu kutoka.
 
Nilimwacha mama mwenye nyumba anachinja kuku, hii njaa niliyonayo na deni la nyumba analonidai sidhani kama leo taweza kumuepuka, nina uhakika hata nikimuomba pocket money hawezi kuninyima. Ila tatizo nikiingia kwenye huu mchezo ni vigumu kutoka.

Nikiwa sina hili wala lile mitaa ya Posta, mara likaja gari, vioo vikashushwa, kutazama ni mrembo alieonekana kana kwamba ananifahamu au tumewahi kuonana au tumesoma pamoja huko kijijini...
 
mara nikasikia sauti toka kwenye gari....."wewe kaka nadhani tunafahamiana", sikuikumbuka ile sura, nikajivuta kusogea mbele ili nipate muono mzuri, yule mwanadada akazidi kutabasamu...
 
...ndani ya ile gari muziki toka kwa mwanadada Lady Jay Dee "Siku hazigandi" ulisikika, nilivuta mawazo nyuma kuangalia yote yaliyonikuta na ambayo bado yananikuta, lakini bado siku zinazidi na visa vinazidi....
 
Nikamwangalia yule dada vizuri, hivi nilimwona wapi? Looh ya mungu makubwa..... Huyu dada ndio yule aliyekuwa ananipenda tangia tulipokuwa shule, kwakweli watu hubadilika..., yaani amekuwa mrembo kiasi hiki?
 
Yule dada akatoa business card yake akaniomba nimpigie baadaye, sikuamini.
 
Nilichukua ile business kadi yake huku mawazo yakinipeleka mara ya mwisho nilipomuona huyu dada, nakumbuka alihama shule ghafla tukapotezana. Kipindi kile sababu ya ujana wangu nakumbuka nilishawahi kutoka nae siku moja baada ya party na vinywaji. Ingawa baada ya hapo sikuendelea na urafiki nae wa karibu na nilikuwa ninamuepuka, mpaka alipohama. Baada ya kuweka ile kadi mfukoni ninapiga jicho kiti cha nyuma... Mungu wangu!!!???, Kidogo nianguke kwa kizunguzungu..... ni kama nilikuwa natazama kwenye kioo, yaani mtoto kadri ya miaka saba ananifanana utafikiri ninatazama picha yangu....
 
Je inawezekana... Siku ile na vile vinywaji haya ndio mazao yake?, Je inawezekana kipindi kile huyu dada ananifatafata, nikadhani anajigonga labda alikuwa anataka kuniambia kuwa nina kiumbe chake?, Je hizi ni baraka au Mkosi?......
 
Sauti ya dada yule ilinistua katika mawazo yangu......, unaelekea wapi nikupeleke?, Kabla sijamjibu nikamkumbuka mke wangu kijijini. Ni mimi ambaye sababu ya kumpa mimba ndio ilisababisha akaacha shule na kukatisha masomo yake, ni kweli nilimpenda lakini labda isingekuwa mimi angekuwa na maisha mazuri na sio haya matatizo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom