Msaada kisheria kwa tukio la ajali hii

tofalikazi

New Member
Nov 24, 2020
3
2
Habari wana JF,

Naomba msaada kueleweshwa juu ya jambo hili kuna ajali iliyo husisha bajaji 2 za kubeba abiria moja ikiwa inatokea upande A na nyingine upande B, zilipokuwa zimesogeleana kupishana iliyo kuwa ikitoka upande B ikapata ajali ya kugonga punda na kumrusha mpaka upande wa pili wa bajaji A hivyo kusababisha bajaji A nayenyewe kuparamia punda na kupinduka na abiria wa bajaji A kuumia vibaya kwa kuvunjika mkono na miguu yote miwili.

Baada ya kufatilia madereva wote wa bajai hawakuwa na leseni.

MSAADA WA MAWAZO KISHERIA

Ni mmiliki yupi anayetakiwa kumhudumia abiria mpaka kupona kisheria na nifidia ipi kwa mgojwa atatakiwa kulipwa baada ya kuwa amepona.
 
Kosa la kwanza huna leseni ya kuendesha bajaji.

Hata kama ulikuwa na bima, hulipwi hela ya matengenezo.

Kosa la pili, bajaji B kaendesha bajaji bila kuzingatia watumiaji wengine wa barabara.

Kuhusu kutibu, ninadhani Bajaji aliyegonga punda ndiye anawajibika.

Ila kutokuwa na leseni ni mbaya Sana maana unaweza ukawa makini usigonge, ila ukigongwa lazima traffic akija aulizie leseni zenu
 
sawa mkuu kwa jinsi nilivyo kuelewa unamaanisha hawa wote A&B wana makosa siyo,
na wanawajibika na kumtibia mgojwa siyo,
bila wao kutengenezewa vyombo vyao na bima makampuni ya bima zao,
na mgonjwa baada ya kuwa kapona wanapashwa kumlipa fidia siyo
 
Kwanza hapo wakumtibu mgonjwa kisheria za mtaa wangu, ni yule aliyembeba abiria huyo.

Kwakua wote hawana leseni, watashtakiwa kwa makosa ya uharibifu wa mali na kusababisha kujeruhi Binaadam na kumuua Punda... so kama wapo waanzage kujificha.

Bima hailipi uzembe labda tuu kama hizo bajaj zilikua zimeibiwa.. so mmiliki wa bajaj A alipe punda na Mmiliki wa Bajaj B amtibu mgonjwa.
 
Back
Top Bottom