Msaada; kipi ni bora kati ya afya na uhandisi

Msaada; kipi ni bora kati ya afya na uhandisi

Nakushauri soma Kozi za afya future ipo kuliko hizo engineering
 
Ushauri Wangu:

AFYA ( CO )
Faida
1.Ajira Ni Uhakika ( Serikalini & Private )
2.Miaka 3 Diploma, Na 2 Cheti

3.Ina Hadhi ( Title ) Katika Jamii
4.Uwezekano Wa Kuwa Boss Ni Mkubwa Katika Kituo Chako
5.Mshahara Wake Unaanza Na TGHS Kwa Diploma Mshahara Ambao Bachelor Degreewa Educ Ndio Anaanza Nao

6. Unapata Vijiwe Au Kujiajiri
HASARA
1.Ni Kujiendeleza, Na Ukitaka Kujiendeleza Mlolongo Ni Mrefu ( From Diploma, AMO ( 5 Years ) To MD ( 5 Years )
3. Ni Gharama Kubwa Kusoma ( Kwenye Private Unis Na Serikalini Competition Ni Kubwa

MECHANICAL ENGINEER
FAIDA
1. Cheap Kusoma ( Vyuo Vya Serikali )
2.Miaka 3 Diploma
3.Unaweza Kupata Vijiwe Au Kujiajiri
4. Unaweza Kujoin Jeshini Kama Unasifa ( Rafiki Yangu Kafanikiwa Kufanya Na Yuko Poa Tu, Analipiwa Ada Na Jeshi Kusoma Aircraft Eng Kwa Sasa NIT )

HASARA
1.Kazi Unapata Kwa Tochi
2.Vibarua Utaburuzwa Sana Na Kuwa Mchafu Sana Kwenye Magereji Bubu

Kazi Kwako , Ushauri Zaidi Ukitaka Uliza Tu
Nachokiwaza hapo ndo icho icho pale pa kuja kijiendeleza itajanichukua muda mwingine na gharama nyingi kwa upande wa afya
 
Nachokiwaza hapo ndo icho icho pale pa kuja kijiendeleza itajanichukua muda mwingine na gharama nyingi kwa upande wa afya
Soma Afya Kama Huna Nia Ya Kuhangaika Sana, Na Usiji- Limit Sana Kwenye CO Unapotaka Afya
 
Nataka taaluma pia maslai ya taaluma nitakayoipata,
Nikiwa na taaluma alafu maslai yakawa madogo itakuwa haina maana tena, maana wengi nimewaona wana taaluma nzuri tuu ila wapo mtaani tangu naanza form one paka Leo ni zaid ya miaka mitano hawana ajira ndio maana lazima niangalie na manufaa nitakayo yapata kutokana na taaluma nitakayoipata
Mi navyoona unahitaji maslah zaid ya taaluma,Ila yte sawa mi namawazo tofauti na wenzangu,,,Ntakuambia
 
Soma unachokipendaa .afu huo sio ufaulu wa juu sana kama unavyojipambanua wee ni survival tyuu ilaa hongera mtu chake umejitahd
Sawa Naelewa mkuu ila kwa upande Wang na mazingira niliyosomea ni ufaulu wa juu hapo ni kwa masomo ya sayansi mengine yaliyobakia nilifanya vizur kuliko hayo yote ya sayansi
 
Kivipi mkuu
Bongo utapga msuli kufa then practical utakuwa shalo halafu + kutafuta kazi za uhandisi n mateso dunia kuliko kazi za afya pia kujiajili afya n rahis zaid kama laboratory pharmacy watu kila siku wanaumwa
 
Ajira kwa sasa si za uhakika kwa afya kama watu wanavyodhani, kuna intake kama mbili hivi kitaa hazijaajiliwa. Think about three/four years to come!!! Chagua kitu cha kusoma kwa kuangalia uwezekano wa kujiajili na wala si kuajiliwa
 
Nenda kasome Marine Engineering .
Alafu baadae ukabobee kwenye offshore engineering .hapo utalamba dume
 
Nenda kapige CIvil engineering itakujengaaaa kaz zake hazifi dunia kila siku inajengekah
 
Mimi binafsi nakushauri ukasome ualimu wa sayansi na hisabati kuliko kwenda kusomea mambo ambayo yanaweza kukupa shida mbeleni, na siyo fani zote za afya mbeleni zitaendelea kuwa na soko kwa mfano ufamasia kwa siku za usoni upepo wake wa ajira hatutakuwa mzuri sana, kumbuka maisha ni kuchagua
 
Chagua diploma moja kati ya hizi
Diagnostic Radiography
Biomedical engineering
Optometry
Medical lab
Clinical medicine

Lakini nakushauri zaidi uchague Diagnostic radiography kwa sababu
-Fani ina watu wachache na hao wachache 90%+ ni diploma kwa iyo ukiwa na diploma tu na ukawa competent unasumbua mtaani na ukifanikiwa kupata degree ukirudi utashangaa umekuw mkuu wa department

-Ni fani nzuri kwa sababu teknolojia za uchunguzi wa magonjwa kila siku zinabadilika na kuongezeka uhitaji wa wataalamu unazidi kuwa mkubwa

-Unaweza kuchagua fani nyingi za
kusomea degree kama udaktari na fani nyengine haswa za afya

Cha kuongezea lazima ufanye kazi sehemu yenye umeme
 
Ushauri Wangu:

AFYA ( CO )

HASARA
1.Ni Kujiendeleza, Na Ukitaka Kujiendeleza Mlolongo Ni Mrefu ( From Diploma, AMO ( 5 Years ) To MD ( 5 Years )

Kutoka CO kwenda MD sio lazima upitie AMO, na pia AMO ni miaka miwili sio mitano
 
Angalia unachokipenda zaidi kati ya hayo uende kusoma. Ni rahisi zaidi kupata mafanikio pale unapofanya kitu ukipendacho.
 
Mimi binafsi nakushauri ukasome ualimu wa sayansi na hisabati kuliko kwenda kusomea mambo ambayo yanaweza kukupa shida mbeleni, na siyo fani zote za afya mbeleni zitaendelea kuwa na soko kwa mfano ufamasia kwa siku za usoni upepo wake wa ajira hatutakuwa mzuri sana, kumbuka maisha ni kuchagua

Kwanini unadhani ufamasia ajira zake mbeleni zitasumbua mkuu?
 
Back
Top Bottom