Naona wengi mnamkatisha tamaa, mimi binafsi nimesoma Bachelor's Degree ya Computer Engineering (hapa nchini) na Master's Degree ya Software Engineering (nje ya nchi).
Hii fani kama unaipenda na ukiwa na bidii ya kusoma zaidi ya yale unayofundishwa darasani basi inalipa possibly kuliko fani nyingine zozote unazoweza kufikiria, wakati ninaanza kusoma watu wengi walinikatisha tamaa na kuniambia nitaishia kuburn cd mtaani na kuua virus kwenye computer za ndugu zangu lakini kutokana na juhudi zangu binafsi nilianza kutengeneza hela wakati bado nipo chuoni, binafsi niliacha kutegemea boom (mkopo) nilipofika mwaka wa 2 chuo.
Nakushauri kama ulianza kujifunza programming kabla hata ya chuo una mwelekeo mzuri na unaweza kufanikiwa sana katika fani hii ukiendelea na juhudi zako.
Wengi unaowaona wababaishaji katika sekta hii ni wale ambao walikimbilia fani bila kujua ni nini hasa wanatakiwa kufanya ili kufanikiwa.
View attachment 430114