Msaada kimawazo nataka nihame civil niende computer engeneering

Msaada kimawazo nataka nihame civil niende computer engeneering

Wewe hama tu ..usitishwe na watu humu JF ...kwanza civil haina ajira ..tenda wanapewa wachina .wabongo kwa wabongo hatuaminiani....soma kitu roho inapenda sio unakomaa na civil kishingo upande
 
jamani wakubwa heshima zenu... Mimi nimechaguliwa diploma in civil ila nataka niamie computer engeneering kwasabab naipenda computer kutoka moyoni lakini watu wananikatisha tamaa wanasema nafanya kitu cha ajabu... Naombeni msaada kimawazo
Hauko peke yako! Mm Nina Diploma ya Electrical & Electronics Engineering but naenda kupiga Degree ya computer Engineering &,IT na sitaki ushauri wa mtu nishaamua! Sasa wewe unataka watu wakuamulie wakati Darasani utakuwa peke yako, kazi utatafuta mwenyewe, mitihani utafanya peke yako wana jf kila mtu anavuta kwake! Nakushauri Heshimu hisia zako kama umependa kitu usiache kasome hata Ualimu wa chekechea ilimradi tuu unapenda huwezi jua Ya Mungu mengi! HAMA CIVIL
 
Soma zote kama unaona shida mkuu. Sijui huku ila nje wanafanya huo mchezo.
 
Follow your dreams,live your dream.
Moja kati ya vitu wengi hatufanikiwi ni kutamani kuwa fulani na mwisho wa siku hauiwi, kuna sababu nyingi zinazopelekea hilo kutoke, Mazingira, ushawishi wa ndugu/jamaa marafiki lakini pia Mategemeo yetu kwa baadaye. Miongoni mwa mambo ambayo huwa ninayaogopa ni kuangalia jambo huku ukilenga/au kutarajia mafanikio ya kiuchumi/kipato kupitia fani husika. Hilo limewapoteza wengi baada ya kuwa na matarajio afu wakakuta ndivyo sivyo, Hilo linatokana na ukweli kwamba dunia inapitia mabadiliko katika kila sekunde ya uhai wake. Binafsi niliipenda Civil nilipokuwa darasa la tatu, Ni katika akili ya utoto nilidhamiria kuwa Civil Engineer, Kilichonisukuma ni Passion ya ukarabati wa Mabanda ya mifugo kama Ng'ombe, Mbwa, utengenezaji wa mabomba ya Nyumbani nk. Ni vitu nilivyokuwa nikivipenda sana hata leo. Nilipoanza kuwa mkubwa tamaa iliongezeka siku hadi siku huku nikiona magorofa na mimi nikitamani kuyajenga actually katika kuchezea maudongo nilijenga sana, Maisha yangu hadi sasa yametawaliwa na ukarabati,ujenzi na ufundi ufundi tu. Japo sikuwahi kuwa smart sana darasani ila ndicho nilichokipenda na Mungu alinisaidia hadi sasa niko katika hatua za Mwisho za kutimiza ndoto yangu, Ni kweli Civil Engineering Kwa case ya opportunity ni kweli zipo za kutosha hii inatokana na maendeleo hafifu ya nchi yetu, na fani husika kuwa moja ya hitaji la msingi kabisa la mwanadamu malazi(shelter) hivyo inapelekea kuwa ni fani endelevu yenye fursa zisizoisha sababu binadamu wanazaliana na mahitaji yao yanaendelea kuwa yasio na ukomo.

Follow your dream, Moja kati ya vitu vinavyoweza kuongeza tija na ufanisi katika utendaji wa jambo lolote lile ni pamoja na upendo/dhamira ya ndani ya moyo ya kweli ya muhusika katika kutenda jambo fulani. Kuna uwezekano mkubwa sana tija ya mtu asiyependa jambo fulani katika moyo kuwa hafifu ikilinganishwa na yule anayelipenda bila ya kuzingatia vipato wanavyoviingiza. Nafasi ya kuwa na ubunifu wenye tija na hali ya kujifunza vitu vipya katika fani husika ni kubwa sana kwa mtu anayependa kile anachofanya kuliko yule anayefanya ili apate fedha. Ndivyo ilivyo, Mapenzi katika vitu hutafanya tuvifanye kwa umakini na umaridadi bila ya kuzingatia kile ambacho tutaingiza, kufanya kazi iliyo maridadi na yenye kuleta faida kwa wengi huwa ndio farijiko la moyo.

Kwa mitazamo mingi ya watanzania utaambiwa nenda Civil, Kwa sababu wengi tumelenga tutapata nini na sio tutafanya nini ili tupate hicho tunachokitaka na wengi huwa hatujali kabisa kujifikirisha negative side za uamuzi tunaochukua, kwa mtazamo wa wenzetu, Industry ya Communication na Science ya kompyuta kwa ujumla inakua siku hadi siku, Shida ni pale ambapo tunasoma ili mradi tuhitimu na cheti na sio tuwe competent at world level, Wengi tunasoma tukijifunga kuzitumia taaluma zetu hapa hapa nyumbani, brother nachoweza kukwambia ukiwa smart utafanya kazi duniani mahali popote tu, Ukiona unang'ang'ania hapa hapa kwetu basi jiweke katika kundi lile ambao elimu zao zinatoa tija ya kawaida sana na ni zile zinazoogopa challenge, Nzito sana kujifunza vitu vipya na zipo ili kujaza nafasi na sio kutatua changamoto. Kama unakuwa granted na Muumba akupe uishi Miaka 40 ijayo Kozi unayoitamani haitakuwa kama unavyofikiria ndani ya miaka 10 ijayo mark my Word samahani kwa kuandika Marefu
Dah jamaa unauwezo mkubwa sana wa kupambambanua mambo "great thinker"
 
jamani wakubwa heshima zenu... Mimi nimechaguliwa diploma in civil ila nataka niamie computer engeneering kwasabab naipenda computer kutoka moyoni lakini watu wananikatisha tamaa wanasema nafanya kitu cha ajabu... Naombeni msaada kimawazo
Fwata ushauri wa @cannibus ambaye ni comp engineer na Major mtendwa ambaye ni civil engineer mtarajiwa!!

Nb: Soma kitu unapenda...umeonyesha unapenda maswala ya i.t...hii ni asset namba moja uliyonayo...!!! Wengi hawafanyi vizuri kwenye it kwasababu waliisoma kama wewe unavyotaka kusoma civil kwa kuangalia soko na sio passion!!! Kasome unachopenda mkuu na sio kwa kuangalia soko nakushauri kama kaka ako!!!
 
Back
Top Bottom