Msaada; Kifaa gani hiki?

Msaada; Kifaa gani hiki?

ni kifaa cha kupimia pombe ya Moutai(aina ya pombe ambayo ni maarufu sana nchini China) ili kuikagua kama ni pombe ya kweli au bandia.
Asante Bakari kwa kuitikia wito,vipi hio pombe ina gharimu kiasi gani?
 
Asante Bakari kwa kuitikia wito,vipi hio pombe ina gharimu kiasi gani?
bei yake hutegemea muda wa kuanzia ilipotengenezwa. Pombe hii yenye umri zaidi ya miaka 50 itachukua RMB20000(TSH milioni 7.16). hata yenye umri wa miaka 3 huchukua zaidi ya RMB1000(TSH laki 3)
 
sawa mkuu tutawasiliana PM huko nitakutafuta
sawa unakaribishwa wakati wowote.
sasa ni saa 5:18 hapa. kesho tutafanya mtihani wa mwisho unaohusu fasihi ya kiswahili, kwa hivyo nahitaji kulala mapema, naomba msamaha wako sitaweza kuzungumza nawe kwa muda mrefu sana. Jumatano baada ya mitihani yote kumaliza nitakuwasilisha ujumbe kwa PM au hata kwa Wechat.
 
sawa mkuu hakuna Tatizo nitumie ujumbe siku ya jumatano PM
 
bei yake hutegemea muda wa kuanzia ilipotengenezwa. Pombe hii yenye umri zaidi ya miaka 50 itachukua RMB20000(TSH milioni 7.16). hata yenye umri wa miaka 3 huchukua zaidi ya RMB1000(TSH laki 3)
Aisee,bei ghali sana
 
Wakuu,
Nimekuta hiki kifaa ndani ya begi la mtumba ambalo nilienda kumnunulia dogo leo.

Nimeshindwa kujua ni kifaa gani na kina kazi gani,maana hata manual yake imeandikwa kichina,nilikuta pia earphone ambazo zimeharibika;

Maelezo yake;

[emoji736]Ni kifaa kidogo ukubwa wa kiberiti au zaidi

[emoji736]Kwa upande wa nyuma kina sehemu ya betri mbili ndogo
[emoji736]Kina matundu kwa pembeni juu,la upande mmoja dogo lingine kubwa,katikati kuna kioo,Ukipeleka mbele mfuniko wa nyuma kinawasha taa

Nilichodhania mwanzoni;
[emoji818]Mwanzoni nilifikiri ni music player kama IPod kutokana na kuwepo pia earphone lakini nikagundua sio kutokana na kutokuwepo sehemu ya kuchomeka earphone, wala spika au sehemu yoyote ya kuweka SD card
[emoji818]Pia nikafikiri ni tochi lakini ukiangalia mwanga wake sio mkali halafu hata mwanga mwenyewe ni unatengeneza duara dogo ukimulika karibu na linakuwa kubwa jinsi unavyosogeza nyuma kama picha mojawapo inavyoonyesha

Kwa anyejua kichina anaweza kusoma hapo au ameshawahi kukiona na anakifahamu anisaidie nijue

Ahsante.

View attachment 1673770View attachment 1673771View attachment 1673772View attachment 1673773View attachment 1673774View attachment 1673775View attachment 1673776View attachment 1673777View attachment 1673778View attachment 1673780View attachment 1673781
Jaribu kufanya google search kwa picture na kuhusu maelekezo tumia google translater kupata translation kwa pic catcher
 
Mhe. Mwalimu Nyerere aliwahi kuzuru China mara kadhaa. Kila alipofika, waziri mkuu wetu Zhou Enlai alikuwa humzawadia pombe hii. Ilipendezwa sana na Mwalimu Nyerere.
Aisee safi sana,kumbe Baba wetu wa Taifa alikua anapenda MAOTAI
 
Back
Top Bottom