Msaada: Kibali cha kumiliki silaha

Msaada: Kibali cha kumiliki silaha

usatz

Member
Joined
Sep 4, 2016
Posts
96
Reaction score
45
Hapa mimi ndo sielewi au, Maana naambiwa kabla sijapata kibali cha kumiliki silaha natakiwa niinunue kwanza, na ibaki dukani ndo nifuatilie kibali

Je, nikinyimwa hicho kibali si inakula kwangu?

Au kuna namna naweza fuatilia kibali kwanza ndo nikalipie silaha baada ya kupata kibali?
 
Kuna rafiki yangu alilipia silaha kwenye moja ya maduka ya serikali almaarufu mizinga leo ni miaka14 kuichukua imeshakua hadithi za Bunuas, kupata kibali ni changamoto ndugu vikao vya kamati ya ulinzi vina mlolongo sana, sheria zetu za umiliki wa silaha bado ni ya kikoloni
 
Hichi ndo kinanitisha sana Mimi
 
Lazima ununue kwanza ili Watoa KIBALI wajue ni silaha gani unayoiombea. Ukinyimwa KIBALI utarudishiwa silaha yako ila utalipia STORAGE CHARGES
Mimi naona, Tuanze Kuomba Kibali upate kibali,
 
Kama ndo hivyo hapo kuna mambo hayapo sawa... sheria ibadilishwe!

Wangeweza kusema ukachague silaha husika upewe details zake dukani kisha upeleke tu sampo kwenye ofisi zao wakuandalie kibali ndipo kisha ukanunue silaha husika
 
Kuna rafiki yangu alilipia silaha kwenye moja ya maduka ya serikali almaarufu mizinga leo ni miaka14 kuichukua imeshakua hadithi za Bunuas, kupata kibali ni changamoto ndugu vikao vya kamati ya ulinzi vina mlolongo sana, sheria zetu za umiliki wa silaha bado ni ya kikoloni
Lazima kuwe na gun control huoni marekani wanavo lia sasa hivi
 
Nililipiaga Bastola Tsh. 2,700,000 pale Tanganyika Arms mwaka 2015 mwanzoni ,process zinakaanza mpaka kwenye Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kinondoni kipindi kile DC Alli Happi na RC Makonda mwaka 2016 huo nikahojiwa vizuri tu, ghafla nikatakiwa kwenda kusoma nje kwa miaka 4 PhD duuuh!!!

Nikajiuliza sasa itakuwaje hii Silaha?? Nikafunga safari mpaka dukani Tanganyika Arms pale Stesheni nikamkuta Meneja wa Duka nikamsomesha,uzuri ni mchanga hakuwa na noma, akaniuliza tu utaniachaje, nikamwambia nipe ml.2 hiyo Laki Saba pata ya Chai, akachukua ile Risiti yangu akaniambia baada ya saa moja muamala utasoma nikasema poa, ndani ya Nusu saa tu akawa amenitumia 2ml, nikamshukuru mambo yakawa yameisha hivyo
 
Hapa mimi ndo sielewi au, Maana naambiwa kabla sijapata kibali cha kumiliki silaha natakiwa niinunue kwanza, na ibaki dukani ndo nifuatilie kibali

Je, nikinyimwa hicho kibali si inakula kwangu ?

Au kuna namna naweza fuatilia kibali kwanza ndo nikalipie silaha baada ya kupata kibali ?
Sheria ni kwamba unatakiwa kununua kwanza silaha then ndo ufatilie kibali,

Hii imewekwa ili wajue ni aina gani ya silaha unayotaka kumiliki na je ni kwa matumizi yapi so kwenye kununua hapa inabid uwe makini kidogo

Mwisho kupata kibali andaa tu mpunga wa usumbufu kwa wazee ili jambo lako liende kiwepesi
 
Hii nchi kila kitu kinawezekana na kwa wakati.....RUSHWA....... yaani bila RUSHWA .........hupati kitu......ni kamchakato ka kishenzi.....kenye mlolongo wa RUSHWA...... ila ths day ni lazima uwe mtoa taarifa........zozote zenye miendendo mibovu.......so watamfuatilia mpaka ex wako...mchepuko wako kama unaye......baa maid unayepunguzia uzito...kijiwe unachovutia bange.....pusha wapo..............NA rushwa juu......inaweza kufupisha safari ya ufuatiliaji........
 
Hapa mimi ndo sielewi au, Maana naambiwa kabla sijapata kibali cha kumiliki silaha natakiwa niinunue kwanza, na ibaki dukani ndo nifuatilie kibali

Je, nikinyimwa hicho kibali si inakula kwangu ?

Au kuna namna naweza fuatilia kibali kwanza ndo nikalipie silaha baada ya kupata kibali ?
Sheria ni kwamba unatakiwa kununua kwanza silaha then ndo ufatilie kibali,

Hii imewekwa ili wajue ni aina gani ya silaha unayotaka kumiliki na je ni kwa matumizi yapi so kwenye kununua hapa inabid uwe makini kidogo

Mwisho kupata kibali andaa tu mpunga wa usumbufu kwa wazee ili jambo lako liende kiwepesi
 
Nililipiaga Bastola Tsh. 2,700,000 pale Tanganyika Arms mwaka 2015 mwanzoni,process zinakaanza mpaka kwenye Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kinondoni kipindi kile DC Alli Happi na RC Makonda mwaka 2016 huo nikahojiwa vizuri tu,ghafla nikatakiwa kwenda kusoma nje kwa miaka 4 PhD duuuh!!!nikajiuliza sasa itakuwaje hii Silaha??nikafunga safari mpaka dukani Tanganyika Arms pale Stesheni nikamkuta Meneja wa Duka nikamsomesha,uzuri ni mchanga hakuwa na noma,akaniuliza tu utaniachaje,nikamwambia nipe ml.2 hiyo Laki Saba pata ya Chai,akachukua ile Risiti yangu akaniambia baada ya saa moja muamala utasoma nikasema poa,ndani ya Nusu saa tu akawa amenitumia 2ml,nikamshukuru mambo yakawa yameisha hivyo
Sas Dr umerud je huitaji Tena kumiliki silaa
 
Hapa mimi ndo sielewi au, Maana naambiwa kabla sijapata kibali cha kumiliki silaha natakiwa niinunue kwanza, na ibaki dukani ndo nifuatilie kibali

Je, nikinyimwa hicho kibali si inakula kwangu ?

Au kuna namna naweza fuatilia kibali kwanza ndo nikalipie silaha baada ya kupata kibali ?
Kwa nini unataka kumiliki silahaa!!??
 
Kuna rafiki yangu alilipia silaha kwenye moja ya maduka ya serikali almaarufu mizinga leo ni miaka14 kuichukua imeshakua hadithi za Bunuas, kupata kibali ni changamoto ndugu vikao vya kamati ya ulinzi vina mlolongo sana, sheria zetu za umiliki wa silaha bado ni ya kikoloni
mkuu bia ukilipia tu unapewa haraka,ila silaha hapana kwakweli lazima watu wajiridhishe.

angalia huko marekani mtoto wa miama 17 anakwenda dukani anauziwa silaha anakwenda kulipua watoto wa miaka 6 kisa walimzomea,huu ni ufala wala sio usasa.
 
Kama ndo hivyo hapo kuna mambo hayapo sawa... sheria ibadilishwe!

Wangeweza kusema ukachague silaha husika upewe details zake dukani kisha upeleke tu sampo kwenye ofisi zao wakuandalie kibali ndipo kisha ukanunue silaha husika
Hapa sawa, wakuandikie aina ya unayotaka kununua
 
mkuu bia ukilipia tu unapewa haraka,ila silaha hapana kwakweli lazima watu wajiridhishe.

angalia huko marekani mtoto wa miama 17 anakwenda dukani anauziwa silaha anakwenda kulipua watoto wa miaka 6 kisa walimzomea,huu ni ufala wala sio usasa.
Sure lakin, Concern yangu ni kuwa, Angalau Kuwe na Ombi la kibali, alafu likipita ndo upewe ukanunue Silaha. Sio kulipia usichokuwa na uwakika kama utakipata
 
Niliporudi kutoka masomoni Cheo kikapanda mara dufu ofisini,so nilitumia short cut tu kuipata fasta japo mlolongo wa kuanzia Serikali ya Mtaa,Kata nk niliufanya lakini ka-Cheo kapya kalisaidia mchakato kwenda haraka tofauti na awali
Hongera sana Dr.
 
Back
Top Bottom