Kichankuli
JF-Expert Member
- Dec 18, 2008
- 887
- 189
JF DR. au mdau mwingine yeyote wa JF tafadhali nieleze iwapo kuna dawa inayoweza kutibu Sagamba (mipasuko ya kwenye visigino)
Wadau mbona kimya, hakuna mwenye kujua habari za tiba ya sagamba?
Ikena nashukuru ngoja nikaisakanye madukani
unaongelea sagamba kama ugonjwa au sagamba kama hali inayoweza kumpata mtu asiyeangalia miguu yake?
Ili kuzuia sagamba nakushauri uwe na kawaida ya kuiloweka miguu yako kwenye maji ya uvuguvugu na sabuni kisha uisugue na jiwe au brashi ( pumice stone).Kisha kausha na upake mafuta.Pia pendelea kulala na soksi baada ya kupaka mafuta hadi hali iwe ya kuridhisha.Endelea kuwa unaisugua unapooga.Miguu yako itabaki soft bila mipasuko.
Nimejaribu kupitapita kwenye maduka ya hapa Dodoma nimekosa, na kuna duka moja walitaka kunichomekea kunipa mbadala kwa mantiki kuwa zote ni anti-fungus. Unaweza kunieleda jina la duka (Dar) ambalo naweza kwenda straight nikapata hiyo dawa tafadhalMafanikio mema,, ila uhakikishe unaipata dawa yenyewe kwani maduka mengi wakikosa dawa hiyo wanakutafutia substute.
Boksi la dawa hiyo ni kama la zambarau na picha ya mtu mwenye sagamba nyayoni imeonyeshwa hali kadhalika mtu mwenye fungus/ukurutu pia imeonyeshwa.
JF DR. au mdau mwingine yeyote wa JF tafadhali nieleze iwapo kuna dawa inayoweza kutibu Sagamba (mipasuko ya kwenye visigino)
Hili tatizo analo mai waifu, na sidhani kuwa linasababishwa na kutoijali miguu/visigino, kwani mwenyewe huwa anaviosha na kuvisugua kwelikwweli. Labda kwa suala la kutovaa viatu vya kufunika visigino hilo naweza kubaliana nalo kwani mara nyingi huvaa viatu vya wazi.
Lakini kitu kingine ambacho kinanitatiza ni kuwa, hata mimi nimekulia kijijini na nakumbuka kutovaa viatu vya kufunika nadhani hadi nilipojiunga na kidato cha kwanza lakini sijawahi kupasuka visigino. Katika familia yetu Mama na dada zangu wawili walikuwa na tatizo la kupasuka visigino. Lakini nakumbuka pia kuna dada mmoja tulikuwa tunasomo shule moja ya msingi, yeye visigino vyake vilikuwa vinatoka unyevunyevu mwingi kiasi kwamba tulikuwa tunamshangaa kweli. Je kuna uwezekano wa upasukaji wa visigino kuwa ni suala la kibayolojia kama ilivyo kuota ndevu, sharafa au gadern love?
Habari zenu madaktari wooote?,
Naombeni utatui wa tatizo hili, maana naita tatizo sababu awali sikuwa hivi lakini tangu nihamie Singida kikazi mpaka najionea huruma.
Nimesha haribu net yangu na mashuka, naona mpaka aibu kuvaa sandalz mtaani, da!
Masaada jamani, kipi cha kufanya...
mFICHA MARADHI KIFO HUMUUMBUA!!!as mbona hujasema kama una magaga kama una fungus kama ni funza sasa tutakusaidiaje ?