Msaada: Ipi dawa asilia na ya haraka ya kuondoa mipasuko unyayoni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada: Ipi dawa asilia na ya haraka ya kuondoa mipasuko unyayoni?

Discussion in 'JF Doctor' started by Kichankuli, May 7, 2009.

 1. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  JF DR. au mdau mwingine yeyote wa JF tafadhali nieleze iwapo kuna dawa inayoweza kutibu Sagamba (mipasuko ya kwenye visigino)
   
 2. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Wadau mbona kimya, hakuna mwenye kujua habari za tiba ya sagamba?
   
 3. I

  Ikena JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2009
  Joined: Oct 24, 2007
  Messages: 482
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 60
  Kuna dawa ya cream inaitwa Fungnil ni nzuri sana, ni maalum kwa fungasi na hayo magaga/sagamba.
   
 4. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Ikena nashukuru ngoja nikaisakanye madukani
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  unaongelea sagamba kama ugonjwa au sagamba kama hali inayoweza kumpata mtu asiyeangalia miguu yake?
  Ili kuzuia sagamba nakushauri uwe na kawaida ya kuiloweka miguu yako kwenye maji ya uvuguvugu na sabuni kisha uisugue na jiwe au brashi ( pumice stone).Kisha kausha na upake mafuta.Pia pendelea kulala na soksi baada ya kupaka mafuta hadi hali iwe ya kuridhisha.Endelea kuwa unaisugua unapooga.Miguu yako itabaki soft bila mipasuko.
   
 6. D

  Dina JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2009
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Pia upunguze 'rate' ya kuvaa viatu vya wazi...tatizo linakuja kama pia una matatizo ya fungus za vidoleni, manake nazo zinachachamaa ukikazana kuzifunika!
   
 7. I

  Ikena JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2009
  Joined: Oct 24, 2007
  Messages: 482
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 60
  Mafanikio mema,, ila uhakikishe unaipata dawa yenyewe kwani maduka mengi wakikosa dawa hiyo wanakutafutia substute.

  Boksi la dawa hiyo ni kama la zambarau na picha ya mtu mwenye sagamba nyayoni imeonyeshwa hali kadhalika mtu mwenye fungus/ukurutu pia imeonyeshwa.
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mi nijuavyo hali ile inatokana na mara nyingi kutoijali sana miguu.

  Mimi nikiwa nimekulia vijijini, nilishambuliwa sana na hayo makenya, lakini ilikuwa inatokana na kutovaa viatu almost muda wote, na ile hali ya baridi sana. Mara baada ya kuhamia mijini na kuanza kuvaa viatu fully, hali hiyo ilipotea na haijarudi tena.

  Unless kama hiyo hali ni special ambayo kwa mimi sijaizowea. Fuata ushauri wa hiyo cream kama ulivyoshauriwa na dada WoS.
   
 9. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Hili tatizo analo mai waifu, na sidhani kuwa linasababishwa na kutoijali miguu/visigino, kwani mwenyewe huwa anaviosha na kuvisugua kwelikwweli. Labda kwa suala la kutovaa viatu vya kufunika visigino hilo naweza kubaliana nalo kwani mara nyingi huvaa viatu vya wazi.

  Lakini kitu kingine ambacho kinanitatiza ni kuwa, hata mimi nimekulia kijijini na nakumbuka kutovaa viatu vya kufunika nadhani hadi nilipojiunga na kidato cha kwanza lakini sijawahi kupasuka visigino. Katika familia yetu Mama na dada zangu wawili walikuwa na tatizo la kupasuka visigino. Lakini nakumbuka pia kuna dada mmoja tulikuwa tunasomo shule moja ya msingi, yeye visigino vyake vilikuwa vinatoka unyevunyevu mwingi kiasi kwamba tulikuwa tunamshangaa kweli. Je kuna uwezekano wa upasukaji wa visigino kuwa ni suala la kibayolojia kama ilivyo kuota ndevu, sharafa au gadern love?
   
 10. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #10
  May 8, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Nimejaribu kupitapita kwenye maduka ya hapa Dodoma nimekosa, na kuna duka moja walitaka kunichomekea kunipa mbadala kwa mantiki kuwa zote ni anti-fungus. Unaweza kunieleda jina la duka (Dar) ambalo naweza kwenda straight nikapata hiyo dawa tafadhal
   
 11. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,186
  Likes Received: 679
  Trophy Points: 280
  Mafuta ya vaselini ni dawa tosha. Safisha miguu vuzuri paka mafuta ya vaselini. Tumia mafuta ya vaselini kila wakati na tatizo la sagamba halitajirudia tena.
   
 12. I

  Ikena JF-Expert Member

  #12
  May 11, 2009
  Joined: Oct 24, 2007
  Messages: 482
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 60

  Mkuu hilo ni swala la kurithi na wakati mwingine ni la mazingira.
  Mi ni wa huko dom, ila kwasasa sipo dom. Nami nilikuanayo hayo masagamba kabla ya kutoka dom.Miezi ya kwanza baada ya kutoka dom ni nilianza kuona mabadiliko katika nyayo zangu na hasa baada ya kutumia fungnil.
  Siku hizi situmii kabisa na visigino vimekua kama vya mtoto mchanga.
  Nikienda maeneo flan flan na hasa huko dom sagamba zinarudi upya.
  So actually ni hali ya hewa au tuseme mazingira yanachangia sana. Nauhakika kuna mazingira ambayo favourable kwa waifu wako.

  Endelea kumshauri kuosha miguu, kupaka mafuta na kuvaa viatu vya kufunika kama ulivyoshauriwa na wanajamii.
   
 13. ruston8919

  ruston8919 Member

  #13
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 68
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  wakuu mambo vp, naomba msaada kwa anayefahamu dawa ya kuzuia kupasuka kwa miguu ktk unyayo, na nipo kwenye barid irnga pia sifany shughuli inayofanya nikanyage maji. msaada plz.
   
 14. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #14
  Aug 9, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Subiri kidogo watakuja wenyewe. Pole sana
   
 15. vena

  vena JF-Expert Member

  #15
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 314
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  uana vaa viatu au unatembea tu bila viatu?
  unapo oga unakumbuka kunawa miguu na nyao vizuri na kukausha kabla ya kuvaa viatu?
  je unatumia aina gani ya sabuni...ina cloro au sodium nyingi?
  naomba unjibu hayo maswali then tuendelee...
   
 16. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #16
  Aug 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]MATUNZO ya miguu ni jambo muhimu kwa mwanamke yeyote. Miguu isiyotunzwa vizuri humfanya mtu asiwe huru kuvaa mavasi na viatu vya ina falani hata kama anavipenda.
  Magaga
  (Kupasuka kwa nyayo) miguuni ni tatizo linalowakumba watu wengi na kuwafanya wasiwe huru kuvaa baasdhi ya nguo na aina za viatu.
  Miguu inahitaji matunzo, hewa ya kutosha ili iwe mikavu ili kuepeukana fangasi na maambukizi mengine kama magaga.

  Ili miguu yako iwe na muonekano mzuri, ni vizuri kama utashiriki mazoezi ya kutosha kwa kutembea, kuruka kamba, kuibonyezabonyeza,

  kuinyoosha, kufanya mazoezi ya kukimbia, au mazoezi ya viungo yatakayo jumuisha na miguu.
  Ili kuzuia miguu yako kupasuka, hakikisha unaisafisha mara kwa mara.

  Tumia scrubs kusugua miguu yako kuanzia juu hadi chini,ukishasugua vizuri safisha na maji ya uvuguvugu kisha paka mafuta ya Zaituni ‘Olive Oil’ au mafuta ya Nazi au mafuta yako ya kila siku , lakini yasiwe na kemikali zinazoweza kuzidisha tatizo.

  Ukiwa na magaga au nyayo ngumu, hakikisha unaiosha mara kwa mara na kuisugua kwa kutumia kifaa maalum. Ikiwezekana nenda duka la vipodozi uulizie kifaa cha kukwangulia nyayo na kununua krimu au losheni maalum za kulainisha miguu yako .

  Njia rahisi ya kuosha miguu ukiwa nyumbani, loweka miguu kwenye maji ya uvuguvugu yenye chumvi, baada ya hapo sugua kwa kifaa maalum cha kusugulia miguu kuondoa seli zilizokufa, kisha paka losheni.

  Kuna dawa zinapatikana sadalia zinaitwa 'cracket heels'. Hizi zinasaidia kiasi. Pia iwapo utaloweka miguu katika maji ya moto kiasi kisha kuikausha kwa taulo na kupakaa mafuta ya vaseline. Mafuta haya hutelezesha miguu kwahiyo ni bora kupakaa usiku wakati wa kulala kisha kuvaa soksi ili usichafue matandiko.Jaribu hivyo kisha unipe Feedback Mkuu.@ruston8919

   
 17. ruston8919

  ruston8919 Member

  #17
  Aug 10, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 68
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  poa brother
   
 18. PistolGang

  PistolGang JF-Expert Member

  #18
  Oct 31, 2013
  Joined: Jan 16, 2013
  Messages: 361
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Habari zenu madaktari wooote?,
  Naombeni utatui wa tatizo hili, maana naita tatizo sababu awali sikuwa hivi lakini tangu nihamie Singida kikazi mpaka najionea huruma.
  Nimesha haribu net yangu na mashuka, naona mpaka aibu kuvaa sandalz mtaani, da!
  Masaada jamani, kipi cha kufanya...
   
 19. C

  Chemwali JF-Expert Member

  #19
  Oct 31, 2013
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 400
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  mFICHA MARADHI KIFO HUMUUMBUA!!!as mbona hujasema kama una magaga kama una fungus kama ni funza sasa tutakusaidiaje ?
   
 20. D

  Deborita Member

  #20
  Oct 31, 2013
  Joined: Sep 10, 2013
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jaman kasema mipasuko kwny miguu/unyayo,ndo magaga ynyw
   
Loading...