msaada juu ya utokaji wa mirath? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

msaada juu ya utokaji wa mirath?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Kazakuku, Oct 28, 2012.

 1. Kazakuku

  Kazakuku JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 262
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Ndugu wanajamii forum naombeni ushauri juu ya namna mirathi hutolewa na upokeaji wake,hapa namaanisha kwamba pesa ya mirathi hutolew namna gani mahakamani......
   
 2. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  Unataka urithi au kurithisha?
   
 3. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2012
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Mimi si mwanasheria wala mtaalamu, lakini nimekwishasimamia mirathi kama mara mbili. Kwa uzoefu wangu huo mdogo,

  Iwapo una maana kuna ndugu yenu amefariki na suala ni kushughulikia/kugawanya mali zake:

  (a)Fanyeni kikao cha ndugu za marehemu mchague/kupendekeza msimamizi wa mirathi. Kikao hiki pia kinaweza kusaidia kuorodhesha mali na madeni ya marehemu na pia kutoa mwongozo wa ugawaji wa mali na kushughulikia madeni;
  (c) Ni muhimu kufuatilia na kupata cheti cha kifo (RITA) mapema, kwani kitahitajika sana mahakamani na kufuatilia mali za marehemu sehemu kama benki, mashirika ya mafao ya jamii, kwa mwajiri, nk
  (d)Shauri la mirathi lifunguliwe mahakama ya mwanzo - ambako kumbukumbu ya kikao cha wanandugu itahitajika, pamoja na cheti cha kifo na uthibitisho wa serikali za mitaa kuhusu kifo, makazi ya marehemu, nk; Iwapo marehemu alikuwa na ukwasi mkubwa shauri litahamishiwa mahakama ya juu zaidi.

  (e) Mahakama itamthibitisha msimamizi wa mirathi iwapo itamwona anafaa (baada ya kufuata taratibu zake);
  (f) Baada ya kupata hati ya mahakama ya usimamizi wa mirathi, msimamizi afanye kazi ya kukusanya/kuorothesha mali zote za marehemu, ashughulikie madeni na kugawa mali inayobaki kwa warithi halali kulingana na wosia halali wa marehemu (kama upo), mwongozo wa vikao vya wanandugu, desturi, dini, sheria, nk.
  (g) Mahakama husimamia ugawaji mali za marehemu na inapobidi kutoa miongozo - na mara nyingi taarifa ya ugawaji wa mali inabidi ipelekwe mahakamani zoezi linapokamilika.

  NB - Sio lazima msimamizi wa mirathi awe miongoni mwa warithi - bali awe mtu anayekubalika/kuaminiwa na wanandugu/warithi watarajiwa.
   
 4. Kazakuku

  Kazakuku JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 262
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Sitaki urithi!!!!!!ni msimamizi nataka njue taratibu zote ili wasije chakachua pesa ya hawa vijana
   
 5. Kazakuku

  Kazakuku JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 262
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Aksante kwa maelezo yako mkuu hapo nimekupata....pia napenda kukkliza ni taratibu gani hutumika kupokea fetha za malipo toka ktk mifuko ya jamii,ni kupitia katika akaunti ya msimamizi au?huja kwa mfumo wa cheki na hiyo cheki mnaenda nayo benki,au ni vip?ushauli haraka....
   
 6. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2012
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Kwangu ilivyokuwa ni kwamba mafao yalilipwa mahakama - ndivyo mahakama ilivyowaelekeza benki na NSSF, na mahakama baada ya kupokea malipo ndiyo iliandika cheki mbalimbali kwa warithi kulingana na mgawo uliopangwa. Ni process iliyochukua muda kiasi.
   
 7. Kazakuku

  Kazakuku JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 262
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  endapo mahakama inapofanya kitendo cha ugawaji bila ya cheki ni makosa au?ni lwamba fedha imelipwa lakini hawajatuonesha cheki ila wanaonesha barua tu....hapo kunaharufu ya uchakachuaji au?
   
 8. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2012
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Mkuu, kama barua imetoka benki au popote mfano NSSF, PSPF nk, ukiwa msimamizi wa mirathi na una mashaka waweza kwenda kuthibitisha huko iwapo kiasi kilichoandikwa ni sahihi ili kupata uhakika kwamba hakuna kinachopotea. Hii nchi yetu mambo mengi yanawezekana - hivyo kupata uhakika ni muhimu.
   
Loading...