MSAADA JUU YA KUSOMA CPA(T)

MSAADA JUU YA KUSOMA CPA(T)

just-imagine

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2015
Posts
373
Reaction score
449
Hello wana JF mliotukuka ...mimi nina shida moja
Nataka nilipie mitihani ya CPA(T) nina mpango wa kufanya mitatu sasa sijapanga kusoma tuition yoyote ile(nataka nipige msuli wa peke yangu) lakini inaniwia vigumu kwan pale kwenye form lazima ujaze tuition centre unayosoma na muhuri ikibidi.....kuna yeyote anaweza kunisaidia kupata muhuri au anajua wanapotoa huduma hii(bila kulipia fee ya somo lolote) labda kama atanicharge fee ya muhuri....
Pleaseee msaada wenu wandugu
 
Moja ya Masomo au topic zinazofundishwa kwny CPA review classes ni ethics , sasa wewe kuanza tu unaanza kuwaza kugushi mihuri kuwa Makini kijana usipoachana na Maisha ya ujanja ujanja utafungwa kwa jambo la kijinga sana, hata ukiipara hiyo CPA mtu akaamua kukuharibia kufichua hiyo unafutiwa CPA yako.
Vijana huko tunapoelekea achaneni na Maisha ya ujanja ujanja hujui utaumizwa wapi.

Kuna Kijana mmoja kakosa nafasi ya uteuzi kwa kuwa tu alighushi cheti cha Computer (Tally & Quick book) japokuwa ana MBA na ACCA yake hiko cheti cha Computer ali submit zamani wakati anaomba kazi akiwa na Diploma tu 2006 kadri alivyojiendeleza alisahau kuwa kwy file lake la ajira kuna hicho kibomu chake ambacho maadui zake wamekitumia kumsambaratisha kuwa si Muadilifu
 
Kijan kwanza upo wapi ili nijue nakusaidiaje....pili katika hiyo form unaweza kujaza kama private candidate inaruhusiwa bt lakin kwa sasa wamebana kidogoo kwan NBAA wanataka watu waliokwenda review na kufundishwa ili utoke uwe nondo na kumbuka walimu wote tanzania nzima huwa wanaitwa na board kupew seminar jinsi ya kufundisha na vitu gani muhimu so nivizuri usome review hata somo moja na mengine kama B3 na B6 unaweza kusoma mwenyew
 
unataka usome mwenyewe?? kwann hautaki wenzako??
Sikumaanisha uliloliandika hapa na nna imani maana halisi unaijua ila unafanya makusudi ili watu wacheke All in all haina shida
Have big "like" b'se that is all you need
 
Acha short cut nenda darasani. Alafu kukamua mwenyewe lazima uwe kichwa sana otherwise utapiga mark time hadi uhisi umelogwa.
...sio kwamba sipendi kusoma tuition ila uwezo wa kifedha ndo mdogo, umenihukumu haraka sana hii ni elimu kama nyinginezo ukiwa hauna uwezo wa kusoma shule za high quality kama FEZA unajaribu kilicho cha uwezo wako.....kiufupi nmepata pesa kama 600k sasa hapo usajili ni kama 310k inayobaki haiwezi kumudu tuition na examination fee....ndo maana naona nilipie mitihani halaf msuli ntajikaza kama mwanaume.......kama unaweza kunishauri wap pa kupata it's ok kama huwez fresh pia ....i can still do something worthwhile in a life...
 
Jaza form then submit hivyo hivyo watakuweka kwenye kundi la private candidate. Kwa Maelezo zaidi wapigie through this no.. 0737218031 mida ya Kazi tu utaeleweshwa
 
Jaza form then submit hivyo hivyo watakuweka kwenye kundi la private candidate. Kwa Maelezo zaidi wapigie through this no.. 0737218031 mida ya Kazi tu utaeleweshwa
Asante sana mkuu MUNGU akubariki
 
Watu kibao wamejaza kama private na matokeo yao yametoka fresh kabisa. B6(governance,..) na Auditing na hata tax unaeza jisomea mwenyewe na ukatoboa tu Mkuu.
 
...sio kwamba sipendi kusoma tuition ila uwezo wa kifedha ndo mdogo, umenihukumu haraka sana hii ni elimu kama nyinginezo ukiwa hauna uwezo wa kusoma shule za high quality kama FEZA unajaribu kilicho cha uwezo wako.....kiufupi nmepata pesa kama 600k sasa hapo usajili ni kama 310k inayobaki haiwezi kumudu tuition na examination fee....ndo maana naona nilipie mitihani halaf msuli ntajikaza kama mwanaume.......kama unaweza kunishauri wap pa kupata it's ok kama huwez fresh pia ....i can still do something worthwhile in a life...
Mi nakuelewa Mkuu, I've been through those hustles. Somo nililolipia lilikua ni Management accounting by then, mengine yote niligonga mwenyewe na nikatoboa fresh tu. Nichek Pm kama vp nikupe mbinu kali za kupiga msuli mwenyewe
 
Watu kibao wamejaza kama private na matokeo yao yametoka fresh kabisa. B6(governance,..) na Auditing na hata tax unaeza jisomea mwenyewe na ukatoboa tu Mkuu.
Asante kwa mwanga ulionipa MUNGU akubariki mkuu.Nashukuru
 
Back
Top Bottom