Msaada: Jinsi ya kujitambulisha ukweni

Msaada: Jinsi ya kujitambulisha ukweni

Roho Mbaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
777
Reaction score
677
Habari wana jukwaa,

Kama kichwa cha habari inavyooelezea nimezamilia mwaka huu kujitambulisha ukweni na nashidwa pa kuanzia, kwa wale wazoefu nisaidieni nataka mwaka huu usipite niishi na jiko langu nikiwa na amani, pia na baraka za pande zote mbili.


Naombeni msaada
 
Kwani unajitambulisha kama nani? kwani wee ukweni unajipeleka? kwani anaekupeleka yuko wapi? kwanini asikutambulishe yeye na ujitambulishe wewe, we unajitambulishaje ?
 
Badilisha jina upokelewe kwa upendo, maana jina ulilonalo likikuandama unaweza kukosa mke
 
Andaa wazee uwatume wakajitambulishe wao kuwa kijana wao kaona ua hapo kwao, then ikishakubalika ndipo watakubaliana uje wakufahamu sio kujitambulisha kiwnyeji, hela kidogo ya wazee wataoenda huko uandae
 
Wewe zama tu ukweni kwako ukishafika tulia tu then watakuja wenyewe na kukupa mwongozo kupitia maswali watakayokuuliza cha msingi demu wako awape taarifa kwao pia ujue taratibu zao kwan wanaweza hitaji barua, hela kidogo, nguo n.k
 
Mi naona naona inategemea na MTU mwenyewe ni wa pande zipi, make makabila mengine bado yanashikilia mila na desturi zake,labda ungekuwa muwazi kwa hilo,but all in all wakati mwingine haya mambo hayana formality.

Lambda cha msingi ungemuuliza Hugo mchumba wako in mambo/vitu/taratibu gani za kuzingatia wakati wa kukamilisha hilo suala huko kwao,then rudi humu wazoefu watakuwa wamesharudi!
 
andaa wazee uwatume wakajitambulishe wao kuwa kijana wao kaona ua hapo kwao, then ikishakubalika ndipo watakubaliana uje wakufahamu sio kujitambulisha kiwnyeji, hela kidogo ya wazee wataoenda huko uandae

Zingatia huu ushauri .tafuta mshenga .tumia wazee wa ukoo wenu wakujuze zaidi .na pia nakupongeza kwa hatua nzuri uliyofikia
 
Ndg.zingatia ushauri niliousapoti hapo juu.wengine humu bado watoto watakupoteza . mambo haya yanahitaji mwongozo na busara za wazee usitake kukurupuka ukajipeleka bila mshenga utaumbuka na kumdhalilisha mchumba wako kwa kuonekana ulikotoka huna watu wazima wa kukuelekeza taratibu za kuzingatia . Istoshe humu si mahala sahihi sana kujadili jambo hili peleka kwa wakubwa zako watakupa picha kamili
 
Andaa wazee uwatume wakajitambulishe wao kuwa kijana wao kaona ua hapo kwao, then ikishakubalika ndipo watakubaliana uje wakufahamu sio kujitambulisha kiwnyeji, hela kidogo ya wazee wataoenda huko uandae

Asante kwa ushauri mzuri, kwa mawazo yangu nilidhani hata mimi mwenyewe naweza kwenda
 
Kwani unajitambulisha kama nani? kwani wee ukweni unajipeleka? kwani anaekupeleka yuko wapi? kwanini asikutambulishe yeye na ujitambulishe wewe, we unajitambulishaje ?

Najitambukisha ukweni, sina uzoefu ndo maana nimeomba ushauri ni vyema pia kujua anasitahili kunitambulisha
 
kuna mila na desturi though sio wote ambao wanafuata utaratibu wa zamani huo ila cha kufanya
1.tafuta wazee wa kabila la mzaa chema ili kama kutakuwa na mamo yoyote ya mila itakuwa easy
2.tafuta hao wazee wenye status zinazofanana na baba mkwe wako ,mfano kama dr.mfanyabashara,mchungaji nk
3.then mnatoa taarifa (jiko anapashwa kuwapa taarifa kuwa kuna ugeni waje lini utaambiwa)
mzee mtawaambiwa na jiko lako
 
Mi naona naona inategemea na MTU mwenyewe ni wa pande zipi, make makabila mengine bado yanashikilia mila na desturi zake,labda ungekuwa muwazi kwa hilo,but all in all wakati mwingine haya mambo hayana formality. Lambda cha msingi ungemuuliza Hugo mchumba wako in mambo/vitu/taratibu gani za kuzingatia wakati wa kukamilisha hilo suala huko kwao,then rudi humu wazoefu watakuwa wamesharudi!

Mpenzi ni mkurya, sijajua mila vizuri za ukuryani maana mimi ni msukuma, na mara nyingi huwa nikimueleza kuhusu kujitqmbulisha anasema swala lipo chini yangu
 
Ndg.zingatia ushauri niliousapoti hapo juu.wengine humu bado watoto watakupoteza . mambo haya yanahitaji mwongozo na busara za wazee usitake kukurupuka ukajipeleka bila mshenga utaumbuka na kumdhalilisha mchumba wako kwa kuonekana ulikotoka huna watu wazima wa kukuelekeza taratibu za kuzingatia . Istoshe humu si mahala sahihi sana kujadili jambo hili peleka kwa wakubwa zako watakupa picha kamili

Asante kwa ushauri
 
Roho Mbaya

Ongea na huyo mpenzi wako kwanza propose na kama akikubali umuowe yeye ndio atakwenda kuongea na familia yake na wakikubaliana (hapa inategemeana na familia) unaweza kukaribishwa kwao ili wakuone then baada ya hapo wewe na mpenzi wako ndio mtakaa mjadiliane ni lini aiandae familia yake kwa kumpokea mshenga ambaye atapeleka barua ya ushenga.

Barua ikishapokelewa na kujibiwa then kazi kwako kupanga ni lini mnapeleka mahari siku ya mahali ndio unakwenda kumvisha pete ya uchumba na mtajadiliana tarehe na mwezi wa harusi hili pande zote mbili zipate muda mzuri wa maandalizi, na kwa kipindi hicho unakuwa tayari familia inakutambuwa unakula mzigo kwa uhuru bila kunyatia unamfata kwao unabeba mzigo na unamrudisha kwao.
 
Last edited by a moderator:
Ndg.zingatia ushauri niliousapoti hapo juu.wengine humu bado watoto watakupoteza . mambo haya yanahitaji mwongozo na busara za wazee usitake kukurupuka ukajipeleka bila mshenga utaumbuka na kumdhalilisha mchumba wako kwa kuonekana ulikotoka huna watu wazima wa kukuelekeza taratibu za kuzingatia . Istoshe humu si mahala sahihi sana kujadili jambo hili peleka kwa wakubwa zako watakupa picha kamili

Acha kukariri wazee kama Samwel Sitta na Kingunge wana busara gani?
 
Back
Top Bottom