Jina linabadilishwa kwa kufanya yafuatayo;
(1) Tengeneza document inaitwa Deed Poll na zalisha nakala kama 6 au zaidi.
(2) Deed Poll ishuhudiwe na Kamishna wa Viapo ambaye aghlabu ni wakili, hakimu na Jaji.
(3) Deed Poll isajiriwe kwa msajiri wa Nyaraka ambaye yuko Wizara ya Ardhi.
(4) Deed Poll italipiwa ada ya usajiri kwa ofisi ya msajiri wa Nyaraka
(5) Baada ya kusajiri Deed Poll basi hiyo Deep Poll ichapishwe kwenye Gazeti la Serikali N.B. Maombi ya kuchapisha deed poll kwenye Gazeti la Serikali yanafanyika Wizara ya Utumishi wa Umma.
Kwa kufanya haya utakuwa umekamilisha mchakato.