Msaada: Jina la mafuta maalumu kwa watu wenye ualbino

kikaniki

JF-Expert Member
Nov 20, 2014
508
962
Habari wakuu!!

Kuna jamaa mlemavu wa ngozi (Albino) ameomba nimnunulie mafuta ya kupaka (maalumu kwa ngozi za wenye albinism).

Nilipomuuliza jina la mafuta hayo, akasema hafahamu jina lake.

Kwa wenye kujua, ninaomba mnitajie jina la mafuta hayo ili niweze kununua na kumsaidia mhitaji huyu.
 
Nenda ktk maduka makubwa ya dawa waeleze kama ulivyoandika hapa watakusaidia.....mara nyingi yanakuwa yameandikwa 'sun protection au sun creamy'ila hayo mafuta yana grade zake kulingana na ngozi ya muhusika,kwa hiyo ni vizuri akafaham ngozi yake ni daraja gani ingawa wengi hawalifanyi hilo....Km upo Dar,pale Mlimani City au Farbek-Manzese nk.
 
Inaitwa suntan lotion ama sunblock. Kazi yake kuzuia mionzi ya jua isipige sana kwenye ngozi. Hasa ya aina ya ultraviolet. Pharmacy kubwa wanauza kwasababu wazungu wanaokuja kutalii africa na maeneo mengine ya tropics wanahitaji kupaka kila wanapotoka juani.
 
Back
Top Bottom