Msaada: Je sheria inayatambua mabaraza ya kimila?

moghaka

JF-Expert Member
May 16, 2011
252
143
Wakuu,

Naombeni kujua kama pana sheria zinazoyatambua mabaraza ya ukoo na kimila katika shughuli zake na utekelezaji wa hukumu zake katika jamiii?

Mfano: Bibi kizee ananyanyaswa na mwanae wa kumzaa, anatukanwa, hata kumpiga, huyo bibi anakimbilia kwenye ukoo/mila mtuhumiwa anahojiwa mbele ya ukoo wote na ushahidi kutolewa wa kutosha kabisa na kumtia hatiani, kifuatacho huyo binti ni kupewa adhabu tu na adhabu kwa kadri ya mila na desturi mojawapo ni kupigwa viboko hadharani imetumika tangu babu na mababu kasheshe imejitokeza HAKI ZA BINADAMU n.k

Mbaya zaidi ukoo unaingia hatiani, kudhalilishwa, n.k huku ni kujenga JAMII au kuibomoa?

Je, kuna namna yeyote ya baraza la kimila kutoa hukumu ya adhabu na ikatekelezwa na dola? Kama vile kupokelewa gerezani akafungwa miezi 6 ?
 
Hayo mabaraza hata kama yatatambulika kisheria...mwenye kutoa adhabu ni jamhuri tu

(Mawazo yangu tu)
 
Back
Top Bottom