Msaada jamani Kuhusu kutoa pesa Western Union

Msaada jamani Kuhusu kutoa pesa Western Union

Tujisahihishe Tz

Platinum Member
Joined
Nov 17, 2011
Posts
3,061
Reaction score
1,367
Nimetumiwa hela jamani kwa njia ya western Union nikiwa Marekani, Kwa bahati mbaya sana wakati hela inatumwa nikapata dharura ya kurudi nchini, kwa kifupi nikapishana na hela, je naweza kuitoa nikiwa hapa nchini?

Naombe msaada wenu katika hilo wanaJF

Natanguliza shukrani
 
Fika ofisi za Western Union Posta Bank inawezekana haina shida
 
Ahsante Mkuu, posta nasikia wana process ndefu kuliko mabenki mengine ni kweli?

Huduma ya western union haingiliani au kuhusiana na huduma benki ya posta.

Western union wanadirisha la kujitegemea na mfumo wa huduma unafanana katika matawi yote ya western union.
 
Huduma ya western union haingiliani au kuhusiana na huduma benki ya posta.

Western union wanadirisha la kujitegemea na mfumo wa huduma unafanana katika matawi yote ya western union.

So Mwl.RCT kupokea nitaweza kupokea bila shida? Ahsante kwa ufafanuzi mkuu
 
Last edited by a moderator:
So Mwl.RCT kupokea nitaweza kupokea bila shida? Ahsante kwa ufafanuzi mkuu
  • Inawezekana kupokea bila tatizo
  • Inatakiwa uwe MTCN Number na Utambulisho wako - Mfano kitambulisho, Passport au leseni. Yaani document yeyote ya kuthibitisha wewe ndiye mtu husika uliyelengwa.
 
mwambie sender aende kwa western union agent yoyote wamfanyie refund na atapewa pesa yake kisha atakupatia ila tu charges ndo hamuezipata
 
Back
Top Bottom