Mimi nina mke na mtoto mmoja, kwa bahati mbaya mke wangu anaishi mbali na mimi mikoa tofauti, tunaishi hivyo kwa kuwa yeye ni mwajiriwa wa serikali na mimi ni mfanyabiashara, hivyo bado hajapata uhamisho wa kunifata mimi. Tumefunga ndoa na ndoa yetu ina mwaka na miezi 6 huwa tunatembeleana kila panapopatikana nafasi... Lakini cha kushangaza ni kwamba ninapomtembelea mke wangu huyo huwa hapendi kabisa kutembea na mimi! Kwa mfano siku za jumapili ukimwambia twende kanisani haendi!. Lakini nikiwa sipo anaenda ukimuuliza hana sababu. Hata pengine anaenda sehemu hawezi kamwe kukubali muende pamoja, katika mazungumzo yetu sametime ananiambia sijui kusalimia, mara hawezi kwenda na mimi popote! Tena anaapia! Kwa kweli kimshiko mimi kabla ya kufunga nae ndoa nilikuwa vizuri kwani hata nnyumba nimejenga, lakini kutokana na mambo fulani biashara imekata sana, hivyo sametime hunipiga tafu hasa upande wa familia... TATIZO LINGINE ALILONALO NI MTU ANAENUNA KWA JAMBO DOGO SANA! Tukiwa pam
hataki muongozane? nimestuka sana " ukosee kujenga nyumba kuliko kukosema kuoa"