Msaada: Huyu ni tapeli au sio wakuu?

french

JF-Expert Member
Aug 2, 2017
3,525
3,649
Kuna mtu nimekutana nae kwenye Linkedin na kujinasibu kuwa yupo Israel. Anafanya kazi kwenye kampuni ambayo huwa inafanya investment na kuprovide fund for investment.

Sasa alikuwa anataka kuja ku invest Tanzania. Akaomba ushauri maeneo amabayo anaweza kuwekeza. Nikampa ushauri na amependa kuwekeza kwenye Tanzanite.

Sasa anataka kutengeneza mkataba wangu na wake ili alirelease fund kwani nilimwambia inabidi kwanza tufungue kampuni na kufungua kampuni kuna gharama kidogo.

Sasa kinachonipa wasiwasi ni kwanini anasema anataka kurelease fund so fast. Hajaniomba account namba yangu wala hela. Info anayohitaji ndio hiyo hapo chini.

Naombeni msaada wakuu kuna info yoyote hapo inaweza msaidia kunipiga hela? Maana naogopa sana technology.

Screenshot_2020-01-17-09-42-27-1.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo jina Mbona kama tajiri mmoja wa Italy miaka ileeeee


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
  • Thanks
Reactions: amu
Ilinikuta nikiwa Chuo Mlimani mwaka wa kwanza. Binti mzuri anadai ni mtoto wa marehemu John Garang. Mshua wake kamuachia midolali anatafuta mtu kutoka nchi yenye amani ahamishie hizo pesa. Alikuwa kaahidi parcent kwenye mgao. Nilichanganyikiwa baada ya kupiga hesabu ya mgao. Nikajisemea dili likitiki naacha chuo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka hao ni wanaijeria !! Unavutwa uje udanganywe ulipie hela .....ili akutumie bitu au pesa achana nao mwambie ....ukweli wewe ni tapeli faster anakublock

sent from toyota Allex
 
Hakuna kitu hapo ni scamers! Pesa ngumu watu wanakesha kutafuta hao Funders hawawapati! Hio kitu ishanitokea mara nyingi sana ila unaweza kumripoti LinkedIn wako very smart.

Niliwahi kukesha naandika business proposal siku tatu nzima last minute nikaamua nipige simu maana mshkaji alikua very smart yaani aliweza kutengeneza hadi email ya kampuni!

Ila roho yangu ikawa nzito nikaingia kwenye website yao nikaenda contact Us nikapata namba ya simu nilikua na vocha! Lahaulaaaa jamaa wakasema huyo scammer ni hatari na wanaendelea kumtafuta.
 
french,
Tapeli kaka. Please usiendelee kuwasiliana naye wala kumpa details zako. Kimbia mbio za Usain Bolt. Tumekupa tahadhari ukiliwa juu yako. Huo ni utapeli wa kizamani sana wa wanaijeria. Wanakimbilia Africa sasa..
 
Back
Top Bottom