Msaada Huawei Modem E220

Msaada Huawei Modem E220

BabaDesi

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2007
Posts
6,228
Reaction score
4,197
Shalom Wataalamu. Nimerudi tena kwa matumaini kuwa safari hii huenda nitafanikiwa baada ya kushindwa huko nyuma kwa zaidi ya mara tatu.

Nina Modem ya Vodacom ya Huawei model E220 HSDPA. Shida yangu ni namna ya kuichakachua ili iweze pia 'kubeba' Airtel, Tigo ba kadhalika kutokana na ugumu wa kumiliki Modem kwa kila mtandao.

Nimeihsjaribukulileta tatizo hili zaidi ya mara tatu hapa ukumbini lakini mara zote maelezo niliyopewa hapa hayakujitosheleza ama pengine uelewa wangu kwa maelezo hayo ulikuwa hafifu. Nakumbuka pia kuna mtaalamu moja alisema kuwa aina hiyo ya Modem Haichakachuliki. kwa wakati huo!

Nitashukuru sana kama kuna muungwana atanipa maujanja ya ukweli ya kuweza kuchakachua modem yangu ili nifaidi pia Vifurushi vya Airtel na tiGO. Shukurani Zimetangulia.
 
...Wataalamu wapo Likizo wakuu??:A S 39:
 
Back
Top Bottom