Msaada: Hoja ya kuoa wake wawili au zaidi

Gazaniga

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2015
Posts
1,051
Reaction score
361
Habarini wadau,

Wakristo wengi wanaamini kuoa mke mmoja ndiyo sahihi kulingana na imani yao lakini biblia hiyohiyo inasomeka dhahiri jinsi Suleimani na Daudi waliokuwa vipenzi wa Mungu walivyooa wake wengi sana.Si hao tu ila wapo wengine pia.

Ni wapi Mwenyezi Mungu alipolazimisha uoaji wa mke mmoja tu? Yeye Muumba hajui kuwa idadi ya wanawake kubwa sana kuliko wanaume? Je ni dhambi kuoa wake wawili au zaidi ikiwa naweza kuwahudumia vyema? Hili si ni bora zaidi kuliko kufanya zinaa na michepuko? Tujadiliane

Msaada wenu nauhitaji.
 
kanisa gani litakuwa tayari kukufungisha ndoa ya pili?labda udanganye tu au huyo wapili mweke hawara yako mzini vizuri na kama ungekuwa mkristo na unaijua dini yako na biblia vizuri tangu sunday school sidhani kama ungeuliza huu utumbo hapa.nna mashaka we sio mkristo au ni wale mwaka mzima unawapita bila kushika bible! upuuzi mtupu!!!
 
“Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na “Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.”—Mwanzo 2:24. Hapa andiko linasema mkewe halisemi wakeze.

“Acheni kila mwanamume awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe.” (1 Wakorintho 7:2) Hapa pia ni mkewe na mumewe na mumewe na mkewe na si wake.

1 Timotheo 3:2 Kwa hiyo mwangalizi anapaswa kuwa asiyelaumika,+ mume wa mke mmoja, mwenye kiasi+ katika mazoea, mwenye utimamu wa akili,+ mwenye utaratibu,+ mkaribishaji-wageni,+ mwenye sifa za kustahili kufundisha,+

Tito 1:6 ikiwa kuna mwanamume yeyote asiye na shtaka,+ mume wa mke mmoja,+ mwenye watoto wanaoamini ambao hawako chini ya shtaka la kuwa wapotovu wala la kuwa watundu.+
 
pole pole bibie yeye anauliza tu au anataka mass balance
kanisa gani litakuwa tayari kukufungisha ndoa ya pili?labda udanganye tu au huyo wapili mweke hawara yako mzini vizuri na kama ungekuwa mkristo na unaijua dini yako na biblia vizuri tangu sunday school sidhani kama ungeuliza huu utumbo hapa.nna mashaka we sio mkristo au ni wale mwaka mzima unawapita bila kushika bible! upuuzi mtupu!!!
 
Hao waliokuwa na wake wengi ni tamaa zao na wengi walipata matatizo...mfano Suleimani wake zake walimgeuza kutoka kwenye ibada ya kweli na hata yeye mwenyewe alijuta kuwa na wake wengi.
 
Kuna hoja inajengwa kuwa Mungu aliumba MTU Mume na mke, kwa maana hiyo inampasa mtu kuoa mke 1.Lakini Yesu aliwahi kuulizwa "mbona sheria ya Musa(torati) iliruhusu wake wengi?".

Akasema ni kwa sababu ya mioyo yenu migumu. Paulo mtume anasema "MTU akitamani Kazi ya uaskofu yampasa kuwa mume wa mke 1." Kwa misingi hiyo nakubaliana na utamaduni wa mwafrika wa kuoa wanawake kwa kiasi/mapenzi ya nafsi yako.

Maana iweje ning'ang'anie kuoa mke 1wakati sijawahi tamani Kazi ya uaskofu. Au iweje nioe wake wengi kama mtume... wakati maisha ya Leo si rafiki kwa jambo hilo.Suala hili ni vyema likabaki kuwa utashi wa MTU binafsi.
 
Wewe ni Muislamu, fuata isemavyo kuruani, BASI! Waislamu wenye wake wanne wana michepuko kibao, acha mtazamo huo!
 
Hao waliokuwa na wake wengi ni tamaa zao na wengi walipata matatizo...mfano Suleimani wake zake walimgeuza kutoka kwenye ibada ya kweli na hata yeye mwenyewe alijuta kuwa na wake wengi.

Ndio maana Yesu alikuja kukamilisha torati, akaleta agano jipya. Ya suleimani alikuja kuyakataza na agano jipya!
 
kanisa gani litakuwa tayari kukufungisha ndoa ya pili?labda udanganye tu au huyo wapili mweke hawara yako mzini vizuri na kama ungekuwa mkristo na unaijua dini yako na biblia vizuri tangu sunday school sidhani kama ungeuliza huu utumbo hapa.nna mashaka we sio mkristo au ni wale mwaka mzima unawapita bila kushika bible! upuuzi mtupu!!!

Mbona Mengi ana mke na akaoa mwingine
 
Wewe ni Muislamu, fuata isemavyo kuruani, BASI! Waislamu wenye wake wanne wana michepuko kibao, acha mtazamo huo!

Kidunia, ratio ya wanaume kwa wanawake ni 47-49% dhidi ya 51-53% ya wanawake. Hii maana yake ni kuwa kwenye watu 100, kuna wanawake 3 watakuwa wako wapweke. Je wazini au wafanyaje? Au wawe bar maid na dada poa ndiyo raha? Mimi naamini tafsiri sahihi za neno mwili mmoja linatakiwa tafakari kubwa kwamba ili maanisha nini?
Naamini Mungu kamwe hakuumba dada na mama zetu wakose waume na hivyo wakajiuze na kuangukia kuwa barmaid ambapo huchezewa ovyo na walevi.
Kwa Uislam uliliona hilo ikaruhusu kuoa zaidi ya mke mmoja, ila kwa uadilifu. Sasa suala la uadilifu ndilo linawashinda watu wengi, ila naamini Uislam ulitafakari suala la idadi ya kila jinsia,wanaoshindwa sasa ni watu wenyewe kwa kukosa uadilifu!

Pia nakubaliana na uislam suala la kwamba endapo mume na mke mumeshindwana ipo haja ya kuachana kiroho safi kuliko kuwekeana sumu! Ingawa Mungu anachukizwa katika Uislam( nakubali kusahihishwa) mambo ya talaka lakini kuna mazingira fulani fulani yameruhusu kuachana!
 
“Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na “Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.”—Mwanzo 2:24. Hapa andiko linasema mkewe halisemi wakeze.

“Acheni kila mwanamume awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe.” (1 Wakorintho 7:2) Hapa pia ni mkewe na mumewe na mumewe na mkewe na si wake.

1 Timotheo 3:2 Kwa hiyo mwangalizi anapaswa kuwa asiyelaumika,+ mume wa mke mmoja, mwenye kiasi+ katika mazoea, mwenye utimamu wa akili,+ mwenye utaratibu,+ mkaribishaji-wageni,+ mwenye sifa za kustahili kufundisha,+

Tito 1:6 ikiwa kuna mwanamume yeyote asiye na shtaka,+ mume wa mke mmoja,+ mwenye watoto wanaoamini ambao hawako chini ya shtaka la kuwa wapotovu wala la kuwa watundu.+

YOHANA 4:16-18
16 „Yesu akamwambia, Nenda kamwite mumeo, uje naye hapa. 17 Yule mwanamke akajibu, akasema, Sina mume. Yesu akamwambia, Umesema vema, Sina mume. 18 Kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako; hapo umesema kweli.
 
Kidunia, ratio ya wanaume kwa wanawake ni 47-49% dhidi ya 51-53% ya wanawake. Hii maana yake ni kuwa kwenye watu 100, kuna wanawake 3 watakuwa wako wapweke. Je wazini au wafanyaje? Au wawe bar maid na dada poa ndiyo raha? Mimi naamini tafsiri sahihi za neno mwili mmoja linatakiwa tafakari kubwa kwamba ili maanisha nini?
Naamini Mungu kamwe hakuumba dada na mama zetu wakose waume na hivyo wakajiuze na kuangukia kuwa barmaid ambapo huchezewa ovyo na walevi.

Kwa Uislam uliliona hilo ikaruhusu kuoa zaidi ya mke mmoja, ila kwa uadilifu. Sasa suala la uadilifu ndilo linawashinda watu wengi, ila naamini Uislam ulitafakari suala la idadi ya kila jinsia,wanaoshindwa sasa ni watu wenyewe kwa kukosa uadilifu!

Pia nakubaliana na uislam suala la kwamba endapo mume na mke mumeshindwana ipo haja ya kuachana kiroho safi kuliko kuwekeana sumu! Ingawa Mungu anachukizwa katika Uislam( nakubali kusahihishwa) mambo ya talaka lakini kuna mazingira fulani fulani yameruhusu kuachana!

CHAZA;
Nataka nitofautiane na weye kuhusu kuoa wake wengi ati kuwasaidia dada zetu na mama zetu wasiwe dada poa au mama poa. Nisamehe kwa kulitumia neno hili hapa; Nasema huu ni ufedhuli wa kupindukia. Nenda K'ndoni makaburini, nenda Ohio, nenda kule beach baharini, na sehem yeyote wanayoikaa hao madada poa.

Kama utawahesabu vizuri, si Darisalama tu hadi Dodoma, zaidi ya 60% ni kina Asha, Amina etc. Christina na Mary ndo walio baki. Sasa iweje hao walioruhusiwa kuolewa wa pili na wa tatu na wa nne ndo wanajikita kwenye hiyo biashara ya maudhi.
Labda tuseme basi Uadilifu wenu umekwisha!! Kulikuwa na mkakati wa kuwaona wanawake wa Kikristo na kuwa Silimisha mbona mkakati umebuma?

Mkristo atakaye oa mke mwingine, huyo anazini na mwisho wa wazinzi wote huyo Mkristo anaujua. Michepuko ni utashi wa mtu akisukumwa na tamaa zake mwenyewe.

Ushauri wangu, Kama umeoa, baki njia kuu. Mke mmoja tu. Ulimkuta msichana, ukamtoa usichana wake, leo kwa kukosa matunzo anaonekana ati kazeeka! We ni wa ajabu saana unaye anga,ia visichana hivyo usijue kuwa mkeo naye alikua hivyo. Mtunze sana mkeo, utamfaidi hata uzeeni. Ng'ombe hazeeki maini......Loh! Mmenikumbusha yule wangu mmoja tu. Hazeekiiiii
 
kanisa gani litakuwa tayari kukufungisha ndoa ya pili?labda udanganye tu au huyo wapili mweke hawara yako mzini vizuri na kama ungekuwa mkristo na unaijua dini yako na biblia vizuri tangu sunday school sidhani kama ungeuliza huu utumbo hapa.nna mashaka we sio mkristo au ni wale mwaka mzima unawapita bila kushika bible! upuuzi mtupu!!!

Hivi kinachokufanya uniite mpuuzi ni nini na hayo mengine yote?
 
Hujakosea ndugu yangu yoote nimeafiki ila tatizo linalokuja hata kutoa hiyo elimu kuna taabu nyingi,uelewa wa watu unatofautiana na wengi wa wenye kuelewa haraka hawapo ktk nafasi muhimu za kuweza badili njia.Sasa waliobaki ni wale walioktk tabaka la walionazo na walio na influence.

Hatuna ujanja hapa tunatakiwa kulijua soko kwa haraka sana, haraka inayozidi hii haraka ya ubadilikaji wa mambo ili tuweze kuikuta dunia na kuanza kwenda nayo. Na pia hatutoweza fika kwa pamoja nchi nzima na wengine hatutofika kabisa.

Ndio maana ninasema elimu sahihi na kuachia time iamue tutakuwa wapi.Tutakuwa uchochoro wa wenzetu kwa kipindi kwani hatuna ujanja. Cha msingi ni kujaribu punguza madhara ya kupokonywa vyote kabla hatujazibuka. Yaani hata hao vipofu wakitupwa mjini wengi kama watafuata njia tofauti ipo chance baadhi wakapona pengine wataanguka ktk rescue team, wengine wataanguka mashimoni wengine watagongwa, etc.

Hapa kidogo nataka elezea kidogo concept ya adapatability na evolution kwa maan isiyo ya kibayojoa sana. Yaani wapo watakaojifunza mazingira na kuweza jua watakavyojibadili na kuweza yatumia kwa faida ya upande wao. Ila bado hatutafika pamoja na mwishowe tutakuwa na ugonjwa mwingine wa kutibu yaani kuwa na watu wachache walioshikilia uchumi uliokuwa km ilivyo kwa nchi km India, South Africa etc. Si muda mrefu utakuta watu chini ya 10% wakishikilia 99.999% ya uchumi wa nchi inayoweza itwa imepiga hatua. Pengine tutakuwa tumerusha rocket anga za juu, tunauza bidhaa na elimu, tuna neuclear na mengine wanayoweza angalia nayo nguvu ya taifa. Ila yote yakabaki kwa vigogo.

Bado ni bora hata hao wachache waokoe kila kitu then baadaye tuanze fanya mabadiliko ya ndani km dilution ili kupata mchanganyiko safi na baadaye kuweza poteza hii sumu ya ujinga.

Nashukuru sana mkuu
 
Hao waliokuwa na wake wengi ni tamaa zao na wengi walipata matatizo...mfano Suleimani wake zake walimgeuza kutoka kwenye ibada ya kweli na hata yeye mwenyewe alijuta kuwa na wake wengi.

Na je ilihesabika kuwa ni dhambi?
 
Back
Top Bottom