Msaada: Hoja ya kuoa wake wawili au zaidi

Msaada: Hoja ya kuoa wake wawili au zaidi

Ndio maana Yesu alikuja kukamilisha torati, akaleta agano jipya. Ya suleimani alikuja kuyakataza na agano jipya!

Alisema sikuja kuitangua torati bali kuitimiliza...soma Mathayo 5
 
Topic ya kiswahili kingereza cha nini? au unataka tujue na wewe unakijua.

Hilo neno nililoliwekea wino mwekundu ni la kiingereza au kiswahili? umeliweka ili tujue na wewe unakijua kiingereza au?

aidha hujielewi au huelewi unachoandika ndugu
 
kumbukumbu la torati 21:15-16
iwapo mtu yu na wake wawili mmoja hampendi mwingine ywampenda na wote wamemzalia wana isije ikatokea huyu ambae hapendwi akanyimwa mtoto wake urithi wa mzaliwa wa kwanza.

maneno siyo rasmi ila nimeona biblia inatambua ndoa ya wake wengi. labda kwa anayetaka kuwa askofu

mkuu umechanganya kati ya kuruhusiwa kufanya kitu na treatment ya mtu iwapo umeshafanya kitu...kuna dini nyingine zinakataza kumuingilia msichana bila kumuoa..still zinasema "kama mwanamme atamharibia usichana wake binti ambaye si mkewe basi na amtolee mahari na kumchukua awe mke wake" ..unataka kusema hicho kipengele cha pili kinamruhusu mtu mume kumuingilia kimwili msichana ambaye si mkewe au kinadeal na situation mahali ambapo kosa limeshafanyika?...like wise katika mfano wako mkuu
 
YOHANA 4:16-18
16 „Yesu akamwambia, Nenda kamwite mumeo, uje naye hapa. 17 Yule mwanamke akajibu, akasema, Sina mume. Yesu akamwambia, Umesema vema, Sina mume. 18 Kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako; hapo umesema kweli.

kwanza point ni mwanamume kuwa na wake wengi and not the other way
pili mwanamke alitambuliwa kuwa ni mzinzi ...for what she had done kwa kupitia kwa wanaume watano was pure sin
 
kanisa gani litakuwa tayari kukufungisha ndoa ya pili?labda udanganye tu au huyo wapili mweke hawara yako mzini vizuri na kama ungekuwa mkristo na unaijua dini yako na biblia vizuri tangu sunday school sidhani kama ungeuliza huu utumbo hapa.nna mashaka we sio mkristo au ni wale mwaka mzima unawapita bila kushika bible! upuuzi mtupu!!!

Hakikaaa n upuuziii mtupuuuu mkuu
 
Huwa sipendi mambo kama haya .... Kila mtu ashikirie imani yake sio kuanza kudadisi ya mwenzio unaamini wake wengi haya ... Mke mmoja haya sipendi kweli uchokozi tu.
 
Mungu alipomuumba Adamu na kumfanyia msaidizi wake... Alitoa ubavu mmoja kwa Adamu au alitoa mibavu?

Afu suala la imani ni kila mtu anavoamini huo ni uchokozi kabisa we amin unavoamini kwa imani yako inavyokuruhusu na sie tuamini kwa imani yetu.
Habarini wadau,

Wakristo wengi wanaamini kuoa mke mmoja ndiyo sahihi kulingana na imani yao lakini biblia hiyohiyo inasomeka dhahiri jinsi Suleimani na Daudi waliokuwa vipenzi wa Mungu walivyooa wake wengi sana.Si hao tu ila wapo wengine pia.

Ni wapi Mwenyezi Mungu alipolazimisha uoaji wa mke mmoja tu? Yeye Muumba hajui kuwa idadi ya wanawake kubwa sana kuliko wanaume? Je ni dhambi kuoa wake wawili au zaidi ikiwa naweza kuwahudumia vyema? Hili si ni bora zaidi kuliko kufanya zinaa na michepuko? Tujadiliane

Msaada wenu nauhitaji.
 
Salaam wakuu,

Samahanini kama hapa sio mahala pake. Mimi ningependa kujua biblia inazungumziaje juu ya swala la kuoa/kuwa na wake zaidi ya mmoja maana kuna wengine wanasema biblia inasupport watu kuoa zaidi ya mmoja wengine wanasema imekataza. Je, ukweli ni upi?

Kwa anayefahamu atujuze.

Asanteni
 
Mambo mengine hata huna sababu ya kujichosha kupost humu sabab hujalazimishwa kuoa hao wanawake na pia ni uelewa wako tu unatakiwa ukuongoze.
 
Back
Top Bottom